UPENDO WELLA AONYA UBADHIRIFU KWENYE MIRADI




Na Allan Kitwe, Tabora

MKUU wa Wilaya ya Tabora Upendo Wella amewataka Wataalamu, Watendaji na Madiwani wa Halmashauri ya manispaa Tabora kuongeza umakini kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kujiepusha na vitendo vya ubadhirifu.

DC ametoa onyo hilo juzi alipokuwa akiongea na Wakuu wa Idara, Watendaji na madiwani wa halmashauri ya manispaa hiyo ambapo aliwataka kuhakikisha miradi yote inasimamiwa ipasavyo ili ilete tija.

Amedokea kuwa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi sana kwa ajili ya utekelezaji miradi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Ametaja baadhi ya miradi inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita katika manispaa hiyo kuwa ni ujenzi wa stendi mpya ya kisasa, soko kuu, barabara za lami za mitaa zenye urefu wa km 10 na mingineyo.

‘Simamieni ipasavyo miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yenu ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, kinyume na hapo tutakuwa na mashaka na weledi wenu’, ameeleza. 

Wella amedokeza kuwa miradi yote inayotekelezwa na serikali ni ya wananchi, hivyo ikitekelezwa chini ya kiwango viongozi waliopewa dhamana kusimamia miradi hiyo watawajibika.

‘Ili miradi hii ikamilike kwa wakati, madiwani, wataalamu na watendaji hamna budi kushikamana, kinyume na hapo mtalaumiana na kuazimiana kwenye vikao vya baraza’, amesema.

Aidha amewataka kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ikiwemo kubuni vyanzo vipya ili kuharakisha maendeleo ya wananchi, huku akimtaka Mkurugenzi wa manispaa hiyo kutofumbia macho upotevu wa aina yoyote wa mapato.

Mbunge wa Jimbo hilo Hawa Mwaifunga ameunga mkono maelekezo hayo na kumhakikishia kuwa watafanya kazi kama timu 1 na kufuatilia kwa umakini mkubwa matumizi ya fedha zote zikiwemo zinazoletwa na serikali kuu.

Amesisitiza kuwa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) haiwezi kutekelezwa kama hakuna usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za miradi, hivyo akaitaka timu ya mapato kufanya kazi kwa weledi mkubwa.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.