JAFO AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KISARAWE
Na Mwandishi Wetu, Kisarawe. MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ameanza utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi mkuu 2025 kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akitaja barabara, maji, afya na elimu kuwa miongoni mwa vipaumbele vyake vikuu katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe, Dkt. Jafo amesema tayari amewasiliana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhusu barabara ya Kisarawe, hatua inayolenga kuhakikisha mkandarasi anaanza utekelezaji wa mradi huo kwa wakati. Katika sekta ya maji, amesema amefanya kikao na ujumbe kutoka Korea kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji utakaohusisha ujenzi wa vituo 105 vya kuchotea maji katika vijiji 17. Ameongeza kuwa ameomba kuzingatiwa kwa uwekaji wa matenki makubwa na kuangalia uwezekano wa kuvifikia vijiji vya Gwata na Dololo. “Eneo hili linahitaji matenki makubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu kufuatia uwepo wa ...