Machapisho

IGP CAMILLUS WAMBURA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI KOZI NO:1/2024/2025 CCP MOSHI.

Picha
Na Lubango Mleka, Moshi. MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, leo Novemba 21,2025 amefunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Askari Polisi Kozi No: 1/2024/2025 katika Shule ya Polisi Moshi Kilimanjaro. Akifunga mafunzo hayo IGP Wambura, amewataka askari wahitimu kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza kwa kuhakikisha wanaimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu. IGP Wambura, ameendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa ajira ndani ya Jeshi la Polisi pamoja na mambo mengine ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu. Jumla ya wahitimu 4826 wakiwemo wapiga buruji wamehitimu mafunzo hayo ya awali yaliyodumu kwa muda wa miezi kumi na mbili na askari hao wahitimu wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika nchini.

DC LULANDALA AMFUTA MACHOZI MJANE SIMANJIRO

Picha
  Na mwandishi wetu, Simanjiro MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mwalimu Fakii Raphael Lulandala amemfuta machozi mjane Sion Mathayo mkazi wa kitongoji cha Mkumbi mji mdogo wa Orkesumet kwa kufanikisha kulipa Sh11 milioni ya deni la nyumba yake iliyowekwa rehani na mume wake  dereva bodaboda Mohamed Ally (Mang'ati) aliyeuawa hivi karibuni. Dereva bodaboda huyo Mohamed Ally (Mang'ati) ambaye aliuza nyumba yake ili kufidia deni alilokuwa anadaiwa, aliuawa kwa kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na watu wawili alipokuwa na pikipiki yake Oktoba mwaka 2025 kisha akafariki dunia akipatiwa matibabu. Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Lulandala akizungumza wakati akimkabidhi mjane huyo hati ya nyumba hiyo amesema wadau mbalimbali wamechanga fedha na kulipa deni hilo ili aendelee kuishi na mtoto wake kwenye nyumba hiyo, baada ya mumewe kuuawa. "Mume wake kabla hajafariki alipata masaibu na kuuza rehani nyumba yao kwa Sh11 milioni ili alipe deni analodaiwa kisha akachomwa moto na ...

TUZO ZA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) MSIMU WA 2024/2025

Picha

IGP CAMILLUS WAMBURA KUFUNGA RASM MAFUNZO YA AWALI KOZI NO:1/2024/2025 LEO CHUO CHA POLISI MOSHI.

Picha

KAMPENI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAPAMBA MOTO HANANG.

Picha
Majiko 1,583 kuuzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya Tsh 11,200. Na Lubango Mleka, Hanang. MKUU wa wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Hanang kujitokezo kwa wingi  kununua majiko banifu ambayo yameanzwa kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku. Wito huo umetolewa leo tarehe 20 Novemba, 2025 na Mheshimiwa Hazali alipofika katika Tarafa ya Katesh Kata ya Nangwa kijiji cha Nangwa kukagua na kufatilia utekelezaji wa mradi ambapo jumla majiko 1,583 yatasambzwa  na kuuzwa kwa bei ya ruzuku wilaya nzima. “Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni mwendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia”alisema Mhe. Hazali. Akizungumza wakati wa uuzaji wa majiko hayo, msimamizi wa mradi kutoka REA, Ndugu Abdulrazack Mkomi ames...

DKT. KIJAJI APOKEA RASMI OFISI WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Picha
Na Sixmund Begashe, Dodoma. WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), amekabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) tayari kwa kuiongoza Wizara hiyo yenye mchango mkubwa kiuchumi nchini.  Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Novemba 20,2025, Mhe. Dkt. Kijaji licha ya kumpongeza mtangulizi wake kwa hatua hiyo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kwenye nafasi hiyo, huku akiahidi kuwatumikia vyema nafasi hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi na  Taifa kwa ujumla. Aidha aliekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana(Mb), amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini katika ngazi mbalimbali alizozitumikia na ameahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya wa Wizara hiyo pale itakapo hitajika. Zoezi hilo la Makabidhiano limeshuhudiwa  na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad  Has...

MZIZE ASHINDA TUZO YA MFUNGAJI BAO BORA LA MWAKA 2025 YA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU AFRIKA.

Picha
MSHAMBULIAJI  wa Yanga, Clement Mzize, ameshinda tuzo ya Mfungaji wa Bao Bora la Mwaka 2025 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Mzize ametangazwa mshindi wa kipengele hicho katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo inayoendelea kufanyika Rabat, Morocco, leo Jumatano, Novemba 19, 2025. Bao lililompa tuzo hiyo ni lile alilofunga dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2024/2025, uliochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 4, 2025, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mzize ameibuka mshindi mbele ya Ghizlane Chebbak, Abdellah Ouazane, Barbra Banda, Anas Roshdy, Asharaf Tapsoba, Calvin Fely, Ibrahim Adel, Jean Claude, Ndabayithethwa Ndlonolo, Refiloe Jane, Oussama Lamlioui na Soufiane Bayazid.

TIMU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAMTEMBELEA MDAU WA UTALII MZEE GEOFF FOX.

Picha
Na Lubango Mleka, Iringa. TIMU  ya Wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Dainess Kunzugala leo Novemba 19,2025 imemtembelea mdau mkubwa  wa utalii na uhifadhi  kwa Kanda za Nyanda za juu Kusini Mzee Geoff Fox wilayani Mufindi mkoani Iringa lengo ikiwa ni kumhamasisha kuingia katika kuwania tuzo za uhifadhi na utalii za Serengeti 2025. Mzee Fox anamiliki kambi za kitalii (lodges) 7 ndani ya hifadhi na ndiye mwanzilishi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Aidha, Mzee Fox ni mwekezaji wa kwanza wa kambi ya utalii katika Hifadhi ya Taifa Ruaha na ni kinara katika uhifadhi kwa kutunza na kulinda miti ya asili.

MRADI WA MAJIKO BANIFU WATAMBULISHWA HANANG

Picha
Majiko banifu 1,583 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku TZS 11,200. Na Mwandishi Wetu, Hanang. WAKAZI wa Hanang waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia. Rai hiyo imetolewa  leo tarehe 19 Novemba, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika kutunza na kuhifadhi mazingira" alisema Mhe. Hazali. Mradi huu unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), ni mwendelezo wa  juhudi za serikali  katika kutunza mazingira na kuboresha afya za  wananchi kwa kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya umuhimu wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia. Aidha Serikali imeweke ruzuku ya asilimia 80 katika  kila j...

TUMEKUJA KUTIMIZA NDOTO YA RAIS SAMIA YA KULIJENGA TAIFA- MHE. CHANDE

Picha
Na Mwandishi wetu – Dodoma NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Hamad Chande (Mb) ameitaka menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutoa ushirikiano katika kutimiza ndoto za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulijenga Taifa. Ameyasema hayo katika kikao na menejimenti ya Wizara hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma Novemba 18,2025 mara baada ya kuripoti ofisini hapo. “Rais Samia amesema miradi tunayoihitaji kutekeleza ni mingi muda ni mchache na ndani ya siku 100 yako mambo anayotaka tuwe tumeyafikia hivyo sisi hatuwezi kuyafikia bila uwepo  wenu ninyi kwa taaluma zenu na mashirikiano yenu ya dhati kwetu” amesema Mhe. Chande. Pia ameitaka menejimenti hiyo kutekeleza falsafa ya  “Ishi vyema na watu ,Ufanye kazi kwa utu, Uwatambue watu ili na wewe uwe mtu mbele za watu."

MC PILIPILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA, POLISI DODOMA WACHUNGUZA CHANZO

Picha
Na Jasmine Shamwepu, Dodoma. JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kifo cha msanii maarufu wa vichekesho Emmanuel Mathias Matebe, maarufu kama MC Pilipili, kilichotokea Novemba 16, 2025 katika Kituo cha Afya Ilazo, jijini Dodoma, ambako alikuwa akipatiwa matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Novemba 19, 2025, Kamishna Msaidizi wa Polisi William Mwamafupa alisema kuwa MC Pilipili alifikishwa kituoni hapo akiwa katika hali mbaya na alifariki dunia majira ya saa 9:00 alasiri. Kwa mujibu wa taarifa za awali, kabla ya kifo chake, majira ya saa 8:00 mchana, msaidizi wake Hassan Ismail alipigiwa simu na mtu asiyefahamika na kuitwa mahali fulani kwa mazungumzo.  Baada ya muda, walitokea watu watatu ambao hawakufahamika wakimtumia MC Pilipili wakiwa ndani ya gari dogo jeupe na kumkabidhi kwa msaidizi wake kisha kuondoka kwa haraka. Wataalamu wa afya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamebaini kuwa marehemu alionyesha dalili za kushambuliwa sehemu mbalimba...

RAIS DKT.SAMIA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU CHAMWINO

Picha
 RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao Kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kilichofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 19 Novemba, 2025.