Machapisho

CHATANDA AWAHAMASISHA WANAKIGAMBONI OKTOBA 29, 2025 KWENDA KUPIGA KURA NA KUMCHAGUA DKT. SAMIA

Picha
Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam. MENYEKITI wa UWT Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameambatana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC). leo tarehe 18 Oktoba, 2025, katika Viwanja vya Tungi Mnadani, Wilaya ya Kigamboni, amewaomba wananchi wa Kigamboni kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura Oktoba 29, 2025, na kuhakikisha wanapiga kura kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wagombea wa Ubunge na Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Aidha, Chatanda amewahimiza wananchi, hususani vijana wa Jimbo la Kigamboni, kutobabaishwa na Wagombea Wengine kwasababu Dkt. Samia amejipambanua kwa Kazi zake. Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kushiriki Bonanza la Mazoezi ya Kutembea (Jogging) na Michezo Mbalimbali lililoandaliwa na Ofisi ya  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Ndg. Dalmia Mikaya.

VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA IGUNGA WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI VYAMA VYA USHIRIKA.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga - Tabora. KATIKA kuhakikisha kuwa vyama vya ushirika vinaendeshwa kwa weledi na kuzingatia sheria, Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Tabora (IGEMBENSABO) kimeandaa mafunzo ya siku nne kwa viongozi wa vyama vya ushirika wilayani Igunga. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora, Jerude Juma Magubiko, amewataka viongozi hao kufuata sheria, kanuni na misingi ya ushirika katika kuendesha vyama vyao. Kwa upande wao, viongozi wa IGEMBENSABO waliowezesha mafunzo hayo wametoa wito kwa washiriki kuyachukulia kwa uzito mkubwa ili wawe mabalozi wa mabadiliko ndani ya vyama vyao. Washiriki wa mafunzo hayo kutoka vyama mbalimbali vya ushirika (AMCOS) wilayani Igunga wameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo, wakisema yatawasaidia kuimarisha utendaji wa kila siku. Huku baadhi yao wakitoa maoni yao ni pamoja na Adelina Blazi (Katibu Meneja Balimi AMCOS), Maria Ramadhani Makamu Mwenyekiti  Mwamapuli AMCOS...

CHATANDA AWAOMBA WAJASIRIAMALI NA MAKUNDI MAALUM KUMPIGIA KURA DKT. SAMIA

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 17 Oktoba 2025, ameshiriki Mkutano wa Makundi Maalum ya Wajasiriamali Mkoa wa Dar es Salaam, amewataka kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan ifikapo Oktoba 29, 2025, ili aendelee kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025–2030. Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa,  Chatanda amepongeza uongozi wa Dkt. Samia  kwa mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ya kimkakati, nchini tanzania.

WAWILI WAHUKUMIWA MAISHA JELA KWA KOSA LA KULAWITI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tanga. MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga imewahukumu Hamisi Jamali Mkufya (22) na Abdallah Sebo (20), wakazi wa Mbugani, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kulawiti msichana mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Mikanjuni, Wilaya ya Tanga. Tukio hilo lilitokea mnamo 26 Desemba 2023 katika eneo la Mikanjuni, Wilaya ya Tanga. Baada ya tukio, taarifa ziliporipotiwa Kituo cha Polisi Tanga, watuhumiwa walikamatwa na upelelezi kuanza mara moja. Mnamo 27 Desemba 2023, watuhumiwa walifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Tanga kujibu kesi ya jinai, kabla ya jalada hilo kuhamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga chini ya kesi namba CC No. 27880/2024, mbele ya Mheshimiwa Jaji Kobelo, ambapo walikana mashitaka yao. Baada ya ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka kusikilizwa, mnamo 16 Oktoba 2025, Mahakama iliwakuta watuhumiwa wote na hatia na kuwahukumu kifungo cha maisha jela.

AKO TANZANIA YASAIDIA JAMII LOSOITO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro  SHIRIKA lisilo la kiserikali la Ako Tanzania Community Support limesaidia jamii ya wakazi wa kijiji cha Losoito kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwa kujenga madarasa matatu shule ya msingi Losoito, kumalizia zahanati ya kijiji na kuwawezesha wanawake kupitia mradi wa lishe wa kilimo cha mbogamboga. Mkurugenzi wa shirika la Ako Tanzania Community support, Hilda Kimathi ameeleza kwamba wamesaidia jamii ya eneo hilo kwa kujenga madarasa, kumalizia zahanati na kuwezesha vikundi vya wanawake wanaolima mboga mboga. Kimathi amesema walipokea ombi toka Losoito na wakajenga chumba cha wanafunzi wa darasa la kwanza na sasa wanajenga madarasa mengine mawili ambayo yatazinduliwa hivi karibuni yakikamilika. "Tunawashukuru partners wetu, Tansania hilfe, Ingrid Miertsch na Hubert kupitia shirika la Aktionskreis Ostafrika e. V. Germany kwa kufanikisha ujenzi wa madarasa hayo matatu ya shule ya Losoito," amesema Kimathi. Amesema watoto wache...

MIAKA 60 JELA KWA KOSA LA KUBAKA NA KULAWITI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Rufiji. OKOTOBA 16, 2025 Mahakama ya Wilaya Kibiti Mkoa wa Pwani imesoma hukumu ya kesi ya jinai ya kubaka na kulawiti dhidi ya Shukuru Alphan Mwinjuma (22) Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kubaka na kulawiti msichana (18) ambapo tukio lilitokea Juni 8, 2025 katika Kijiji cha Bungu wilaya Kibiti. Baada ya mahakamani kusikiliza ushahidi wa pande zote, mahakama ilimtia hatiani mshtakiwa Shukuru Alphan Mwinjuma kwa kosa la kubaka na kulawiti. Kesi ilisikilizwa na upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne pamoja ushahidi wa nyaraka ambao walithibitisha kosa na mtuhumiwa alikiri kosa na alitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria. Mbele ya Mhe. F. P. Ntulo - SRM, Mahakama imemuhukumu kosa la kwanza kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kosa la pili miaka 30 gerezani kwa kosa la kulawiti adhabu zote zinakwenda sambamba.

WAANDISHI WA HABARI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Picha
  Na Lubango Mleka, Tanga. WAANDISHI wa habari wa Jiji la Tanga wamejengewa uwezo kuhusu namna sahihi ya kutumia nafasi yao kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto katika jamii  ili kuwa na jamii bora. Kupitia elimu hiyo, waandishi wa habari wamekumbushwa umuhimu wa kutumia vyombo vya habari katika kupaza sauti za kupinga ukatili wa kijinsia, kuelimisha jamii kuhusu madhara yake, na kuimarisha ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama, amani na ustawi wa familia na jamii kwa ujumla. Elimu hiyo imetolewa  Oktoba 16, 2025 na SP Mwambigiri, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga, akishirikiana na INSP Neema Samson Ndorosi, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Tanga, pamoja na Sajenti Ruth, Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Tanga,  katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Chakula Duniani.

JWTZ YALIDHISHWA NA HALI YA USALAMA NCHINI KATIKA KIPINDINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OCTOBA 29,2025

Picha
 

KINYEREZI YAFURIKA WANANCHI KWENYE MKUTANO WA KAMPENI CHATANDA AKIOMBA KURA ZA CCM.

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam. MRATIBU wa Kampeni za CCM Jijini DSM, na Mwenyekiti waJumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) Leo tarehe 16 Oktoba, 2025, afanya Mkutano wa Kampeni kwenye kata ya Kinyerezi Jimbo la Segerea na kuwaomba Wananchi kujitokeza kwa Wingi Oktoba 29, 2025 kwa Kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumchagua Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, pamoja na Madiwani wote wa Kata ndani ya Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Chatanda ameyasema hayo wakati akinadi Ilani ya CCM 2025/2030 na kuwaambia Wananchi kuwa Dkt. Samia anatosha na anafaa kuliongoza Taifa hili kwa kuwa ametekeleza kwa vitendo ilani ya CCM 2020/2025 kwa kukamilisha miradi Mbalimbali ya Kimaendeleo na kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya Mfano kwa Mataifa Mbalimbali Duniani. Akimuombea kura Mgombea Ubunge Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, pamoja na Madiwani wa...