MIAKA 60 JELA KWA KOSA LA KUBAKA NA KULAWITI.




Na Mwandishi Wetu, Rufiji.

OKOTOBA 16, 2025 Mahakama ya Wilaya Kibiti Mkoa wa Pwani imesoma hukumu ya kesi ya jinai ya kubaka na kulawiti dhidi ya Shukuru Alphan Mwinjuma (22)

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kubaka na kulawiti msichana (18) ambapo tukio lilitokea Juni 8, 2025 katika Kijiji cha Bungu wilaya Kibiti.

Baada ya mahakamani kusikiliza ushahidi wa pande zote, mahakama ilimtia hatiani mshtakiwa Shukuru Alphan Mwinjuma kwa kosa la kubaka na kulawiti.

Kesi ilisikilizwa na upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanne pamoja ushahidi wa nyaraka ambao walithibitisha kosa na mtuhumiwa alikiri kosa na alitiwa hatiani kwa mujibu wa sheria.

Mbele ya Mhe. F. P. Ntulo - SRM, Mahakama imemuhukumu kosa la kwanza kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka na kosa la pili miaka 30 gerezani kwa kosa la kulawiti adhabu zote zinakwenda sambamba.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.