WAANDISHI WA HABARI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
Na Lubango Mleka, Tanga.
WAANDISHI wa habari wa Jiji la Tanga wamejengewa uwezo kuhusu namna sahihi ya kutumia nafasi yao kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto katika jamii ili kuwa na jamii bora.
Kupitia elimu hiyo, waandishi wa habari wamekumbushwa umuhimu wa kutumia vyombo vya habari katika kupaza sauti za kupinga ukatili wa kijinsia, kuelimisha jamii kuhusu madhara yake, na kuimarisha ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama, amani na ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.
Elimu hiyo imetolewa Oktoba 16, 2025 na SP Mwambigiri, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga, akishirikiana na INSP Neema Samson Ndorosi, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Tanga, pamoja na Sajenti Ruth, Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Tanga, katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Chakula Duniani.




Maoni