VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA IGUNGA WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI VYAMA VYA USHIRIKA.
Na Lubango Mleka, Igunga - Tabora.
KATIKA kuhakikisha kuwa vyama vya ushirika vinaendeshwa kwa weledi na kuzingatia sheria, Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Tabora (IGEMBENSABO) kimeandaa mafunzo ya siku nne kwa viongozi wa vyama vya ushirika wilayani Igunga.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora, Jerude Juma Magubiko, amewataka viongozi hao kufuata sheria, kanuni na misingi ya ushirika katika kuendesha vyama vyao.
Kwa upande wao, viongozi wa IGEMBENSABO waliowezesha mafunzo hayo wametoa wito kwa washiriki kuyachukulia kwa uzito mkubwa ili wawe mabalozi wa mabadiliko ndani ya vyama vyao.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka vyama mbalimbali vya ushirika (AMCOS) wilayani Igunga wameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo, wakisema yatawasaidia kuimarisha utendaji wa kila siku.
Huku baadhi yao wakitoa maoni yao ni pamoja na Adelina Blazi (Katibu Meneja Balimi AMCOS), Maria Ramadhani Makamu Mwenyekiti Mwamapuli AMCOS), Kisena Ikobya (Mwenyekiti, Jilabela AMCOS), Olingo Sombe (Mwenyekiti, Balimi AMCOS) na Diana Jisena (Mjumbe, Yegagihagi AMCOS), ambao kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa elimu ya mara kwa mara kwa viongozi wa vyama vya ushirika.
Maoni