KATIBU MKUU AMWAGA PONGEZI KWA UWT TABORA
Na Allan Kitwe, Tabora. JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Tabora imepongezwa kwa kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Pongezi hizo zimetolewa jana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa Suzane Kunambi alipokuwa akiongea na mamia ya Viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo kutoka Wilaya zote 7 za Mkoa huo na vikundi vya wanawake wajasiriamali. Ameeleza kuwa umoja na mshikamano unaoendelea kuoneshwa na akinamama wa UWT Mkoani hapa na wanaCCM wote ni ishara tosha kuwa wagombea wote wa CCM watapata ushindi wa kishindo. ‘Wanawake wa Tabora hongereni, kazi yenu ni njema sana, naamini Oktoba 29 mwaka huu, mtajitokeza kwa wingi zaidi na kumpigia kura za kishindo mgombea Urais kupitia CCM, wabunge na madiwani, CCM Oyeee’, amesema. Kunambi amesisitiza kuwa ni wajibu wa wana UWT kushiriki kikamilifu katika kampeni zinazoendelea sasa hapa nchini na kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kumsemea Dk Samia Su...