Machapisho

TAKUKURU YAKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA.

Picha
Na Mwandishi Wetu,  KATIKA juhudi za kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongzwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye sekta ya afya na kuimarishwa kwa huduma zinazotolewa kwa Wananchi, Watumishi wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) leo imekabidhi mashine mbili za kisasa za huduma ya watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda, maarufu kama watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila alisema, “Hospitali zina mahitaji mengi na Serikali yetu inajukumu kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora. Hivyo ni wajibu wa kila mwananchi mzalendo wa nchi hii kuchangia ili kuimarisha sekta ya afya na huduma nyingine muhimu.” Chalamila amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo m...

MAKALA MAALUMU YA WANAWAKE WACHIMBAJI WA MADINI CHUNYA

Picha
WANAWAKE CHUNYA WACHANGAMKIA UCHIMBAJI, WATOA UZOEFU, OMBI KWA SERIKALI NA TAASISI ZA FEDHA. Na Mwandishi Wetu, Chunya. SEKTA ya Madini nchini Tanzania inaendelea kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii na sasa inajulikana kama Sekta jumuishi inayotoa nafasi sawa kwa wote, wanaume, wanawake na vijana kushiriki kikamilifu. Wanawake Wilayani Chunya ni ushahidi wa mabadiliko haya, wakivunja dhana ya zamani kuwa madini ni kazi ya wanaume pekee. Wakizungumza hivi karibuni, baadhi ya wanawake hao wameeleza jinsi wanavyoshiriki katika kila hatua ya mnyororo wa madini, wapo wanaomiliki leseni za uchimbaji mdogo, wachimbaji mahiri, wapondaji wa mawe na wafanyabiashara.  Wanasema shughuli hizo zimewawezesha kupata kipato, kulea familia, kuanzisha miradi ya maendeleo na kujenga makazi bora, ushuhuda wao unaonesha wazi kuwa sekta ya madini inayoendeshwa kwa usawa wa kijinsia inaweza kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa jamii na taifa kwa ujumla. Mwenyekiti wa Kikundi cha Wa...

TAULO ZA KIKE 9500 ZAGAWIWA KWA WANAFUNZI 600 KATIKA SHULE TATU DADOMA

Picha
Na Hamida Ramadhani, Dodoma. MJUMBE wa Bodi ya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Action Girls Foundation (AGF), Dk Hawa Mkwela alisema kuwa taulo hizo zilikabidhiwa katika kueleke Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani katika shule hizo, ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 11  duniani kote. Akuzungumza wakati wa ugawaji wa taulo hizo kwenye shule ya sekondari ya Chunyu alisema kuwa hayo jana wakati wa ugawaji wa taulo za kike kwenye shule ya Sekondari ya Chunyu aliwataka wanafunzi hao kutumia taulo hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa. Alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakitumia taulo hizo vibaya kwa kuzimwagia pombe na kuzivaa ili walewe  "Suala la matumizi ya taulo za kike  vibaya Kwa kuziwekea pombe Kali na kulewa,lilibainika katika semina iliyoandaliwa na wizara ya afya ikiwahusisha wahadhiri na wakufunzi wa vyuo vikuu na kati wakati wakijadili changamoto za vijana zilizopo vyuoni zinazotokana na matumizi mabaya ya p2, vitendo kama gangsex na ulevi ," alisema...

VIJANA SASA KUJIFUNZA UFUNDI KWA URAHISI KUPITIA PROGRAM YA VSOMO KUTOKA VETA.

Picha
Na Mwandishi Wetu,Mbeya. MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeendelea kutumia teknolojia ya kisasa kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa VSOMO, unaowawezesha wanafunzi kujifunza kwa kutumia simu janja (smartphone) wakiwa mahali popote nchini. Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Vijana yanayoendelea mkoani Mbeya, Ofisa Habari na Uhusiano wa VETA, David Mpondyo, alisema mfumo huo utasaidia kutoa fursa kwa watu wengi kupata mafunzo ya ufundi stadi bila kulazimika kuwepo darasani. “Mwanafunzi anapakua programu ya VSOMO kupitia Play Store, kisha anaanza kujifunza kwa nadharia kupitia simu yake janja. Baada ya kukamilisha sehemu ya nadharia, hufanya mafunzo kwa vitendo (practical) katika chuo cha VETA kilicho karibu na anapomaliza hupewa cheti kinachotambulika sawa na wale waliopo darasani,” alisema Mpondyo. Alibainisha kuwa mfumo huo umetumika kwa zaidi ya miaka tisa na umeendelea kuboreshwa ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira, huku ji...

ZAINABU AFANYA KAMPENI MLANGO KWA MLANGO KUSAKA KURA ZA UBUNGE JIMBO LA KIVULE.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. MGOBEA Ubunge Jimbo la Kivule, Ilala, Dar es salaam, kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Bi. Zainabu Ham Abdul, ameahidi kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia Wananchi, atahakikisha anaboresha huduma mbalimbali za kijamii katika jimbo hilo akiangazia utoaji wa fursa kwa watu wenye ulemavu na makundi maalum, huduma bora za afya, elimu, upatikanaji wa maji safi na uboreshaji wa miundombinu ya barabara. Bi. Zainabu anaefanya kampeni zake mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, kijiwe kwa kijiwe amesema kuwa, iwapo atapewa dhamana ya kuliongoza jimbo hilo, pamoja na mambo mengne atahakikisha anashirikisha jamii kupitia fursa za kiuchumi kwa vijana, wanawake, ikiwemo kuwasemea watu wenye ulemavu ili kila mmoja aweze kunufaika na rasilimali zilizopo kwa usawa na uwazi. Naye Meneja wa Kampeni wa mgombea huyo, Bw. Komein Rwihula, amewaomba wananchi kumchagua mgombea wao, ili akafungue ukurasa mpya wa maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la Kivule na kusisitiza umu...

TUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU KWA WINGI - NYARI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani  MKURUGENZI wa Glisten Pre & Primary school iliyopo mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Justin Nyari ameisihi jamii kushiriki kwa wingi uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu wa 2025 kwa kujitokeza kupiga kura ili kuwachagua viongozi bora. Nyari ameyasema hayo kwenye mahafali ya tano ya wahitimu wa darasa la saba ya shule ya awali na msingi Glisten iliyofanyika shuleni hapo. Ameeleza kwamba akiwa mwana jamii anakumbusha kuwa Oktoba 29 mwaka 2025 kutafanyika uchaguzi mkuu hivyo watu washiriki zoezi hilo kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura. "Nikiwa mwana jamii, nawakumbusha kuwa Oktoba 29 mwaka 2025 Taifa letu litafanya uchaguzi, naomba tushiriki kupiga kura kwa amani na utulivu, ili tuendelee kuwa mfano bora kwa watoto wetu katika kulinda umoja na mshikamano wa Taifa," amesema Nyari. Ameeleza kwamba dunia imeona namna uongozi wa miaka minne wa Rais Samia Suluhu Hassan ulivyokuwa madhubuti na wenye kuwatum...

NENDENI MKAWASILIZE WANANCHI WA SONGWE- CHATANDA

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Songwe. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania Taifa (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), ametoa wito kwa Wagombea wa Ubunge na Udiwani kuhakikisha wanatimiza dhamira zao za kuwatumikia wananchi mara baada ya kuteuliwa na kuaminiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara leo, uliofanyika Kata ya Msangano, Jimbo la Mombo, mkoani Songwe, Chatanda amesisitiza kuwa Wananchi wanahitaji kusikilizwa, kutembelewa na kuungwa mkono katika kutatua changamoto zao na kuinua Maendeleo katika maeneo yao.

WANA MOMBA WAAHIDI KUICHAGUA CCM KWA KISHINDO MBELE YA CHATANDA

Picha
  Na Hamida Ramadhani,Songwe. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 11 Oktoba 2025 katika Wilaya ya Momba, Kata ya Kamsamba, Mkoani Songwe. Ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, Huku akiwaomba Wananchi Kukichagua Chama Cha Mapinduzi ifikapo Oktoba 29,2025. Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, amemuombea Kura za Heshima Mgombea wa Nafasi ya Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Momba, Ndg. Condester Sichalwe na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo sambamba na hilo Wananchi wa Momba wamemuahidi Chatanda kuwa Watapiga Kura za Kishindo kwa Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM ili kuitimiza furaha yao kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

UTAFITI MIAMBA BONDE LA EYASI WEMBERE WATHIBITISHA UWEZEKANO WA UPATIKANAJI MAFUTA

Picha
 *Dkt Mataragio akagua shughuli za utafiti na kutoa maelekezo kwa TPDC na AGS*   *Awamu ya  pili ya utafiti kukamilika Aprili 2026.*   *Asilimia 90 ya wanaotekeleza mradi ni watanzania*  Na Mwandishi Wetu, Arusha. UTAFITI unaofanyika katika  mradi wa kimkakati wa  Eyasi Wembere unaolenga kutafuta mafuta na gesi katika bonde la ufa la Afrika  Mashariki umeonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa Mafuta na Gesi katika bonde hilo. Hayo yamebainika wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa  mradi huo mkoani Arusha wilaya ya Karatu.  “Kazi za utafiti wa mradi huu zimeanza mwaka 2015,  tumekuwa tukikusanya data mbalimbali zinazohusiana na uwepo wa mafuta na gesi ambapo baada ya ukusanyaji, data hizo zilitumika kubainisha miamba tabaka ambayo ina mafuta na tukajiridhisha kwamba katika eneo hili la bonde  ipo miamba ambayo inaweza ikahifadhi m...

IGUWASA YATATUA KERO YA MAJI SHULE YA MSINGI CHIPUKIZI B IGUNGA.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA) imefanikiwa kutatua tatizo sugu la maji katika Shule ya Msingi Chipukizi B iliyopo eneo la Mtaa wa Sanzura, Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora. Zaidi ya Wanafunzi 200 pamoja na Walimu na Wakazi wanaozunguka Shule hiyo  wameanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama, hatua inayotarajiwa kusaidia kudhibiti milipuko ya magonjwa na kuboresha mazingira ya kujifunzia. Wananchi waliozungumza na blogu ya Habari Kamili wakati wa zoezi la uchimbaji mtalo kwa ajili ya kulaza bomba la maji wamesema huduma hiyo ni faraja kubwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu. Maria Luhende, Rajabu Juma, Aisha Mussa, Elias Kishiwa na Paul Joseph, ni baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sanzura waliojitokeza katika zoezi la uchimbaji wa mtalo wameipongeza IGUWASA kwa kufanikisha mradi huo. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Stoo, Phabian Lushindika, amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa na amehamasisha wananchi kushiriki katika kulinda m...