TAKUKURU YAKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA MBEYA.
Na Mwandishi Wetu, KATIKA juhudi za kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita inayoongzwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maboresho makubwa yaliyofanyika kwenye sekta ya afya na kuimarishwa kwa huduma zinazotolewa kwa Wananchi, Watumishi wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) leo imekabidhi mashine mbili za kisasa za huduma ya watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda, maarufu kama watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila alisema, “Hospitali zina mahitaji mengi na Serikali yetu inajukumu kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora. Hivyo ni wajibu wa kila mwananchi mzalendo wa nchi hii kuchangia ili kuimarisha sekta ya afya na huduma nyingine muhimu.” Chalamila amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo m...