UTAFITI MIAMBA BONDE LA EYASI WEMBERE WATHIBITISHA UWEZEKANO WA UPATIKANAJI MAFUTA
*Dkt Mataragio akagua shughuli za utafiti na kutoa maelekezo kwa TPDC na AGS* *Awamu ya pili ya utafiti kukamilika Aprili 2026.* *Asilimia 90 ya wanaotekeleza mradi ni watanzania* Na Mwandishi Wetu, Arusha. UTAFITI unaofanyika katika mradi wa kimkakati wa Eyasi Wembere unaolenga kutafuta mafuta na gesi katika bonde la ufa la Afrika Mashariki umeonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa Mafuta na Gesi katika bonde hilo. Hayo yamebainika wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo mkoani Arusha wilaya ya Karatu. “Kazi za utafiti wa mradi huu zimeanza mwaka 2015, tumekuwa tukikusanya data mbalimbali zinazohusiana na uwepo wa mafuta na gesi ambapo baada ya ukusanyaji, data hizo zilitumika kubainisha miamba tabaka ambayo ina mafuta na tukajiridhisha kwamba katika eneo hili la bonde ipo miamba ambayo inaweza ikahifadhi m...