WANAWAKE WASISITIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA.

 


Na Hamida Ramadhani, Tanganyika.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewataka Wanawake wa Wilaya ya Tanganyika kujibu upotoshaji mitandaoni unaojaribu kuvuruga amani na mshikamano wa nchi kwa kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025.



Akizungumza baada ya kuwasili wilaya Tanganyika leo tarehe 10 Oktoba 2025, ikiwa ni muendelezo wa kampeni amesema watu hao hawapaswi kujibiwa kwa maneno bali ni kwa kuipa ushindi CCM ili  kuendelea kubaki madarakani.



Katika mkutano huo pia alimuombea kura za ndio mgombea  wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja, kumnadi mgombea wa ubunge  Ndg.Moshi Selemani Kakoso, na Wagombea nafasi ya Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Tanganyika.















Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.