CHATANDA - HAKUNA KUPITA BILA KUPINGWA,TWENDENI TUKAPIGE KURA ZA NDIYO OCTOBA 29,2025.



Na Hamida Ramadhani, Tanganyika.

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 10 Oktoba 2025, akiwa katika Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi, ametoa wito kwa wanachama wa CCM na Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya ndiyo, licha ya uwepo kwa wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa.



Aidha, Chatanda ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akieleza mafanikio makubwa yaliyofanyika Chini ya uongozi madhubuti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.




Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, alimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanganyika, Moshi Selemani Kakoso, pamoja na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.