Machapisho

CHATANDA - HAKUNA KUPITA BILA KUPINGWA,TWENDENI TUKAPIGE KURA ZA NDIYO OCTOBA 29,2025.

Picha
Na Hamida Ramadhani, Tanganyika. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 10 Oktoba 2025, akiwa katika Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi, ametoa wito kwa wanachama wa CCM na Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya ndiyo, licha ya uwepo kwa wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa. Aidha, Chatanda ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akieleza mafanikio makubwa yaliyofanyika Chini ya uongozi madhubuti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, alimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanganyika, Moshi Selemani Kakoso, pamoja na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo.

WANAWAKE WASISITIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA.

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Tanganyika. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewataka Wanawake wa Wilaya ya Tanganyika kujibu upotoshaji mitandaoni unaojaribu kuvuruga amani na mshikamano wa nchi kwa kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025. Akizungumza baada ya kuwasili wilaya Tanganyika leo tarehe 10 Oktoba 2025, ikiwa ni muendelezo wa kampeni amesema watu hao hawapaswi kujibiwa kwa maneno bali ni kwa kuipa ushindi CCM ili  kuendelea kubaki madarakani. Katika mkutano huo pia alimuombea kura za ndio mgombea  wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja, kumnadi mgombea wa ubunge  Ndg.Moshi Selemani Kakoso, na Wagombea nafasi ya Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Tanganyika.

CHATANDA: MSIDANGANYIKE NA WAHUNI WACHACHE WA MITANDAONI

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Katavi. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewataka wananchi wa kitongoji cha Nkumbi, kata ya Kapalala, kupuuza upotoshaji unaofanywa na watu wachache mitandaoni wanaolenga kuondoa amani na mshikamano uliopo nchini. Chatanda ameyasema hayo jana tarehe 9 Oktoba 2025, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji cha Nkumbi, kata ya Kapalala, Jimbo la Nsimbo, Mkoa wa Katavi.

CHATANDA: CCM IMETUHESHIMISHA WANAWAKE KWA KUTUPA DKT. SAMIA.

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Katavi. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewaheshimisha wanawake kwa kumteua Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa Katavi amesema kuwa hatua hiyo ni ishara ya imani kubwa inayooneshwa na chama kwa wanawake wa Tanzania hivyo amesema ni vyema wanawake nchini  kumpigia kura Dkt samia pamoja na Wabunge na Madiwani wa CCM kwa wingi ili kupata ushindi wa kushindo ifikapo Oktoba 29,2025.