DOROTHY SEMU: MWAROBAINI WA HUDUMA ZA AFYA NI KUICHAGUA ACT-WAZALENDO
Na Mwandishi Wetu, Kilosa -Morogoro. KIONGOZI wa Chama Cha ACT Wazalendo, Ndugu @dorothysemu leo 05 Oktoba, 2025 amefanya Mkutano wa hadhara wa kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Ndugu, Hassan Mbaruku Thabiti pamoja na wagombea Udiwani. Kiongozi wa Chama, Dorothy Semu Katika hotuba yake amewaeleza Wana Kilosa juu ya huduma za Afya muarobaini ni kuichagua ACT Wazalendo ambapo jawabu letu ni kufuta Bima ya Afya kwa wote yenye vifurushi na kuwapa watanzania Bima ya Afya kwa wote isiyo na Vifurushi. Ameongeza zaidi na kusema "Tunakataa Watanzania kubaguliwa katika mifumo ya Afya kwa uwezo wao, tunataka watu wote wajumuishwe na wapate huduma bora za Afya bila kujali tabaka lake la kipato" KC, Dorothy Semu juu ya migogoro ya ardhi amewaeleza watu wa kilosa kwamba "Uongozi wa Serikali ya CCM umeshindwa kutatua kero hii ya migogoro ya Ardhi badala yake wamezidi kuchochea na kila kona kukutana na changamoto hii. Ameongeza kuwa, "ACT Wazalendo juu ya hili tunasema tunatak...