Machapisho

ROGHAT FALME ROBERT KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA CHAKULA DUNIANI UNAOTARAJIWA FANYIKA NCHINI ITALY

Picha
C  CEO wa Shirika lisilo la Kiserikali la Akili Platform Tanzania, anatarajia kuondoka hapa nchini hivi karibuni kuelekea nchini Italy kwenye Mkutano wa chakula duniani unaotarajiwa kufantika Octoba, 10 -17, 2025.

DK.MWINYI AAHIDI UWEKEZAJI MKUBWA BWAWANI NA KUIMARISHA MJI MKONGWE

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. MGOMNEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ina mpango wa kufanya uwekezaji mkubwa katika eneo la Hoteli ya Bwawani katika awamu ijayo ya uongozi wake. Akizungumza katika mkutano wa kampeni Jimbo la Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi, leo tarehe 29 Septemba 2025, Dkt. Mwinyi alibainisha kuwa eneo hilo ni muhimu kwa uchumi na utalii wa Zanzibar, na Serikali inalenga kulibadilisha kuwa mfano bora wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya awamu ijayo pia itatekeleza mpango maalum wa kuimarisha nyumba zote za Mji Mkongwe zikiwemo nyumba za wakfu, binafsi na za Serikali ili ziendelee kudumu kwa muda mrefu, kwa kutumia fedha za ndani. Kuhusu changamoto ya magari kuingia Mji Mkongwe, amesema Serikali imekamilisha mpango wa mabasi ya umeme ili kupunguza tatizo hilo na kulinda uimara wa majengo ya kihistoria. ...

DK.MWINYI AAHIDI KUJENGA MASOKO MAPYA 5 ZANZIBAR

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. MGOMBEA wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kujenga masoko makubwa mapya matano ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira bora zaidi. Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mwanakwerekwe leo tarehe 29, Septemba 2025 katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi, Dkt. Mwinyi alisema masoko hayo mapya yatakayojengwa katika maeneo ya Kinyasini, Mwera, Kibandamaiti, Kisauni na Kwahajitumbo yataleta suluhisho la kudumu kwa changamoto za wafanyabiashara. Ameeleza kuwa kukamilika kwa masoko hayo kutapunguza msongamano unaotokana na uhaba wa nafasi, pamoja na kupunguza kodi kubwa zinazowakabili wafanyabiashara hivi sasa. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kumchagua tena yeye pamoja na wagombea wa CCM katika ngazi za ubunge, uwakilishi na udiwani, ili kutimiza dhamira...

UCSAF YAKAMILISHA MINARA 734, UJENZI WAFIKIA ASILIMIA 96.83.

Picha
  UJENZI wa minara 758 ya mawasiliano unaosimamiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umefikia hatua kubwa ya mafanikio, ambapo minara 734 tayari imekamilika na inatoa huduma za mawasiliano kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya vijijini nchini. Hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 96.83, hali inayodhihirisha dhamira ya Serikali kupitia UCSAF kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za mawasiliano, hususan wale wa maeneo ya vijijini na yenye changamoto za kijiografia. Minara iliyosalia ni 24 pekee, na inatarajiwa kukamilika hivi karibuni ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika katika maeneo yote yaliyopangwa. Mradi huu ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya Serikali na kampuni za simu nchini kwa lengo la kufikisha huduma za mawasiliano vijijini, zikiwemo huduma za intaneti na simu ambazo zimekuwa changamoto katika maeneo yaliyokuwa hayana mtandao wa uhakika. Wananchi wa vijiji ambavyo minara imekamilika wameshaanza kunufaika na mawasiliano bora...

MATHIAS CANAL AONGOZA UPATIKANAJI MIL 85 UJENZI WA KANISA KIOMBOI-IRAMBA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Iramba. MWANZIRISHI na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya WAZOHURU MEDIA Ndg Mathias Canal amewaongoza Viongozi wa dini, Wadau wa maendeleo na Waumini kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania-KKKT Usharika wa St George Kiomboi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida. Katika harambee hiyo iliyofanyika jana tarehe 28 Septemba 2025 katika eneo la Ujenzi wa Kanisa Mtaa wa Lulumba, Mgeni huyo rasmi amesimamia upatikanaji wa fedha taslimu Tsh 79,407,000 ambapo ahadi ni Shilingi Milioni 4,010,000 na jumla ya fedha zote zilizopatikana ni Shilingi Milioni 85,017,000. Mgeni rasmi Ndg Mathias Canal pamoja na marafiki zake waliomuunga mkono amechangia jumla ya Tsh milioni 3,835,000 na mifuko 10 ya Saruji. Akizungumza katika harambee hiyo Mathias amesema kuwa Kanisa ni nguzo muhimu ya maisha ya kiroho, kijamii na hata kiuchumi. Kupitia kanisa waumini wanajifunza misingi ya upendo, mshikamano, uadilifu na ujenzi imara wa taifa.  "Ujenzi wa kanisa si kwa aj...

TANGAZO.

Picha
OFISI YA MKUU WA WILAYA YA IGUNGA IKISHIRIKIANA NA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA, Hospitali ya Wilaya Igunga inategemea kupokea timu ya madaktari Bingwa wa Mh.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuanzia tarehe  29/09/2025  hadi tarehe 03/10/2025. Madaktari Bingwa watakaokuwepo ni 01. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wanawake( kinamam) 02. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani (mfano kisukari,pressure nk) 03. Daktari Bingwa wa Upasuaji  04. Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinywa na meno 05. Daktari Bingwa wa watoto  06. Daktari Bingwa wa Usingizi na ganzi 07. Muuguzi mbobezi. Wananchi wote wenye uhitaji wa huduma hizo wafike Hospitali ya Wilaya Igunga. Huduma zitatolewa kwa gharama nafuu kabisa. NYOTE MNAKARIBISHWA.

TANZANIA YAENDELEZA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA ICC MEN’S T20 WORLD CUP AFRICA QUALIFIER, 2025.

Picha
  Na Mwandishi Wetu,Zimbabwe. BALOZI wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP. Suzan S. Kaganda, ameongoza maafisa wa Ubalozi kushuhudia Timu ya Taifa ya Cricket ya Tanzania katika mchezo wa mashindano ya ICC Men’s T20 World Cup Africa Qualifier 2025, uliofanyika tarehe 28 Septemba 2025, kati ya Tanzania na Uganda. Katika mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya Takashinga vilivyopo mjini Harare, Zimbabwe, Timu ya Taifa ya Cricket ya Tanzania imeibuka mshindi baada ya kuifunga timu ya Uganda kwa runs 9, hatua inayofanya timu ya Tanzania kuendelea na ushindi baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Botswana siku ya Ijumaa, tarehe 26 Septemba 2025. Ushindi huu ni mafanikio muhimu katika ICC Men’s T20 World Cup Africa Qualifier 2025. Kufuatia ushindi huo dhidi ya Uganda, timu ya Tanzania kwa sasa imefuzu kuingia hatua ya nusu fainali. Mchezo wa nusu fainali utachezwa mnamo tarehe 02 Oktoba 2025, kati ya Tanzania na Namibia kwenye uwanja uliopo mjini Harare, Zimbabwe. Ubalozi wa Tanzania unaend...

WANAFUNZI ZAIDI YA 3000 WANYWA MAZIWA KUBORESHA AFYA GEITA

Picha
  Ma Mwandishi Wetu, Geita. WANAFUNZI wapatao 3,385 wa Shule za Msingi na Sekondari mkoa wa Geita wamekunywa maziwa kwa ajili ya ustawi wa Afya Bora na Lishe. Akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni yaliyofanyika Septemba 24, 2025 katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani hapo, Mwakilishi wa Msajili Bodi ya Maziwa Tanzania, Bi. Deorinidei Mng’ong’o alisema maziwa yaliyotolewa ni Pakti 3964 ambayo ni sawa na lita 1004.6. Mng’ong’o alisema kabla ya Siku ya kilele kumekuwepo na Matukio kadhaa yaliyokuwa yanaendelea kama vile kutembelea wanafunzi wenye uhitaji maalumu ambapo zaidi ya wanafunzi 3,385 walinufaika kwakupata Maziwa ili kuendelea kuboresha Afya zao. Alisema idadi ya lita za maziwa zilizotolewa kuanzia Septemba 22 hadi Septemba 24 mwaka huu ni lita 1004.6. “Maziwa ni mlo kamili hivyo natoa rai kwa Wazazi, Walezi na Walimu kuhakikisha watoto wetu wanapata maziwa kwa lishe bora, Afya nzuri na ukakamavu wa akili”alisema. A...

TAARIFA KWA UMMA

Picha
Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF @taifastars_ @caf_online @ligikuu @bonwambura70 @ligikuu

KATIBU MKUU WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA GST KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Geita. KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametembelea Banda la GST katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita. Katika ziara hiyo, Mhandisi Samamba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo. Aidha Viongozi wengine waliotembelea banda la GST ni pamoja na Dkt. Mussa Budeba Mtendaji Mkuu wa GST,  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi.  Kupitia maonesho hayo GST Imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Madini kuhusu teknolojia  na mashine mbalimbali zinazotumika kwenye utafutaji na uchenjuaji wa madini.

MELI KUBWA MPYA YA KISASA YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  MELI ya Grande Shanghai kutoka nchini China imetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam usiku wa tarehe 20 Septemba, 2025. Meli hiyo maalum kwa ajili ya kubeba magari, ni mpya kabisa ambayo imetengenezwa mwaka 2025 inatumia nguvu ya umeme jua (solar power) ambayo ni teknolojia rafiki kwa mazingira badala ya kutumia mafuta katika uendeshaji wake. Meli hiyo ya ghorofa 14 na urefu wa mita 220 ina uwezo wa kubeba magari 9,000 kwa  wakati mmoja. Kwa sasa meli hiyo inaendelea na ushushaji wa magari 1624 katika Bandari ya Dar es Salaam. Wakizungumza wakati wa hafla fupi ya upokeaji wa meli hiyo, kwa niaba ya menejimenti ya meli hiyo, Bw. Girolamo Carignani amesema: “huu ni mwanzo kwa meli zetu kufika katika Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania." Amesema kuwa wataendelea kufanya safari za kuja nchini Tanzania ili kuboresha biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, na kuongeza kuwa hivi karibuni itaanza safari za kwenda Japan kutokea Ch...

TAARIFA KWA UMMA

Picha
 

FAHAMU KUHUSU GAZETI LA SERIKALI

Picha
 

WAASI WA M23 WAANZA KUTOZA ADA KWA SHULE MJI WA GOMA.

Picha
  SHULE ambazo hapo awali zilikuwa zinatoa elimu bila malipo katika mji wa Goma ,nchini DRC sasa zimeanza kutoza ada chini ya udhibiti wa waasi wa M23, huku walimu wakikosa mishahara kutoka serikali kuu , jambo linalozua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wazazi na walimu kuhusu upatikanaji wa elimu, wakati huu juhudi za upatanishi zinazoongozwa na Qatar zikilenga kushughulikia mzozo mpana wa eneo hilo. #M23 #drceducation #goma #drcgoma #Elimu

TBS YAONDOA TANI 42 ZA BIDHAA ZA CHAKULA ZA WATOTO ZENYE MIDOLI NDANI YAKE MAARUFU KWA JINA LA CHAMA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeondoa sokoni tani 42 za bidhaa za chakula za watoto maarufu chama zenye ‘mido li’ ndani yake.  Pia, limesema baada ya kufanya uchunguzi na kubaini uwepo wa viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo, ilipiga marufuku na kusitisha uzalishaji na uingizwaji wa bidhaa hizo sokoni.  Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa TBS, Kandida Shirima alitoa ufafanuzi huo wakati wa mkutano wa wahariri na waandishi wa habari uliofanyika jana kuelezea mafanikio ya TBS katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.  Aidha, shirika lilibaini uwepo wa baadhi ya wazalishaji wanaofunga vyakula na vitu vingine kama midoli hasa kwenye bidhaa za chakula za watoto kwa lengo la kuvutia watumiaji.  Amesema kuwa, baadaye walichukua hatua ya kutoa taarifa kwa umma na kuvifikia vi wanda vinavyozalisha bidhaa hizo na kusitisha uzalishaji wake.  “Tumefanya ukaguzi kupitia ofisi zetu za kanda nchi nzima na tum...

TANZANIA YAANDAA WATAALUMU WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Austria  TANZANIA imeanza kuandaa wataalamu wa Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kupitia vyuo vya ndani na nje ya nchi kwa lengo la kujenga uwezo wa kitaifa na kupunguza utegemezi wa wataalamu kutoka nje. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema hayo hivi karibuni jijini Vienna, Austria wakati wa kikao maalum na Mkurugenzi wa Divisheni ya Afrika wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), Dkt. Gashaw Gebeyehu Wolde, kando ya Mkutano Mkuu wa 69 wa IAEA. Katika mazungumzo yake na Theresa Wutz, Afisa Mkuu Muidhinishaji wa Miradi wa kampuni ya eee Austria, Prof. Nombo alipongeza hatua ya Austria kupitia UniCredit – Bank of Austria kuendelea kufadhili Mradi wa Elimu Kidigitali Zanzibari, akieleza kuwa msaada huo utafungua fursa za kupanua matumizi ya TEHAMA hadi shule na vyuo vya Tanzania Bara. Kukamilika kwa awamu za mradi huo kutaiwezesha Tanzania kuwa na mifumo madhubuti ya kidigitali, miundombinu imara na rasilima...

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA AALCO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kampala - Uganda.  TANZANIA ni mwanachama wa AALCO, imeshiriki katika Mkutano wa 63 uliofanyika Kampala, Uganda, ambapo ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Bi. Bibiana Kileo, na TAKUKURU ikiwakilishwa na Mchunguzi Kiongozi Msaidizi Debora Elisha Mlowe kutoka Kurugenzi ya Huduma za Sheria.  Ushiriki huu unaonesha nafasi muhimu ya Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa na urejeshaji wa mali zinazopatikana kutokana na vitendo vya rushwa. Katika mkutano huo wa siku tano, Tanzania imesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na makosa ya kimataifa yanayovuka mipaka, pia imeunga mkono juhudi za kuimarisha nyanja za urejeshaji wa mali na utaifishaji mali, hatua inayodhihirisha dhamira ya taifa katika kulinda rasilimali na kuimarisha uwajibikaji barani Afrika na Asia.

BAROZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA AKUTANA NA WAANDISHI ZANZIBAR.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  MHE. Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tone Tinnes, na ujumbe wake wamekutana na waandishi wa habari na content creators ili kusikia simulizi za mafanikio yao kupitia program ya SWIL. Kupitia mafunzo ya wanawake na uongozi, waandishi wamekuwa daraja muhimu la kusambaza habari, kuibua mijadala na kuhamasisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia.