Machapisho

WANANCHI WA KATEMBE, MWALONI MULEBA WAONDOKANA NA ADHA YA BARABARA

Picha
*Ni kiunganishi cha wafanyabiashara wa Rwanda, Burundi na Uganda* Na Mwandishi Wetu, Muleba.  UJENZI wa barabara ya lami ya Katembe -Mwaloni inayounganisha Barabara kuu ya kutoka nchi za Uganda, Rwanda na Burundi katika wilaya ya Muleba  Mkoani Kagera  uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 400 umeleta ahueni kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na wafanyabiashara wa samaki kutoka katika visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria kwenda ndani na nje ya Nchi. Kiongozi wa mbio za Mwenge  wa uhuru Kitaifa Ndugu Ismail  Ussi ameridhisha na viwango vya mradi huo na kuwapongeza TARURA kwa utekelezaji wa mradi wenye viwango ambao unaendeleaa kuwasaidia wananchi . Alisema kuwa Ili wanachi wapate huduma bora na nguvu ya kuzalisha wanahitaji Barabara nzuri zenye viwango na kupitia umma wa wananchi ameshukuru usimamizi wa mradi huo na namna Halmashauri ya Muleba ulivyotoa mapato ya ndani kujenga Barabara imara inayoweza  kuchochea uchumi na kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara...

WAZIRI WA HABARI ZANZIBAR ANUNUA TIKETI 100 MCHEZO WA NIGER NA TANZANIA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh: Tabia Maulid Mwita, amenunua Tiketi 100, kwa ajili ya Mashabiki, Kushuhudia Mchezo Kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Niger. #tabiamwita #r.hmwinyi #wizara_ya_habari_zanzibarz #Tanzania #Niger

TRA YAKARIBISHWA MAKANISANI KUTOA ELIMU YA KODI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro.  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro imealikwa kutoa elimu ya kodi kwa Wanachama wa ELCT SACCOS katika kikao cha mwaka cha taasisi hiyo.  Mafunzo hayo yamefanyika jana tarehe 06.09.2025 katika Kanisa  la KKKT ushirika wa Majengo , katika manispaa ya Moshi, Mwika na Hai  mkoani Kilimanjaro ambapo mada  zilizowasilishwa ni pamoja na Usajili wa biashara mtandaoni, Dawati maalumu la uwezeshaji biashara na uwasilishaji wa ritani za kodi na ulipaji wa kodi kwa hiari. Akiwasilisha mada, Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi, Bw. Odupoi Papaa amewasisitiza wanachama kuwasilisha ritani za kodi na kufanya ya kodi kwa wakati pamoja na kutoa na kudai risiti za kielektroniki.

MAKAMU MWENYEKITI WA ACT WAZALENDO TANZANIA BARA AKAMATWA NA POLISI

Picha
MAKAMU Mwenyekiti ACT Wazalendo   Bara, Ndugu Isihaka Mchinjita   amekamatwa na Polisi muda huu akiwa Lindi baada ya uzinduzi wa kampeni. Ukamatwaji wake ulihusisha na upigwaji wa mabomu ya machozi ili kusambaratisha watu.

RAIS MWINYI AHUDHURIA MAULID YA KITAIFA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa Kiislamu katika Maulid Makuu ya Kitaifa ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Mnazi Mmoja. Maadhimisho hayo yametimiza miaka 99 tangu kuanzishwa mwaka 1926, yakihusisha wananchi na waumini kutoka sehemu mbalimbali za Zanzibar. Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Mama Mariam Mwinyi, pamoja na viongozi wa dini.

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AZINDUA SOKO LA KISASA CHUINI ZANZIBAR

Picha
  RAIS wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua soko la kisasa la wafanyabiashara Chuini, lililopo Wilaya ya Magharibi A. Soko hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 43 na lina uwezo wa kutoa ajira kwa wananchi 4000 na kuchangia ukuaji wa uchumi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa soko hilo, Rais Mwinyi amesema malengo makuu ya serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira mazuri ya kufanya biashara, huku wakichangia maendeleo ya kiuchumi na kutengeneza fursa za ajira kwa jamii.  Ameahidi kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miradi inayoongeza tija na ustawi wa wananchi.

MRADI WA MAJIKO BANIFU WATAMBULISHWA KIGOMA

Picha
*Majiko banifu 8,424 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Kigoma *Wilaya Sita kunufaika na mradi.  *Kila Wilaya kupata majiko 1,404.  Na Mwandishi Wetu, Kigoma.  WAKAZI wa Kigoma waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia Wito huo umetolewa leo Septemba 04, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Simon Nyakoro Sirro wakati akipokea mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu unaosimamiwa na kuratibiwa  na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) . "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama katika kutunza mazingira na kuboresha Afya za wananchi" amesema Mkuu wa mkoa Mhe. Sirro, alipokuwa akipokea mradi huo. Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa, Mhandisi wa Miradi kutoka wakala wa Nishati Vijijini (REA), Raya Majallah amesema, “Mradi huu unalenga kusambaza majiko banifu ili kukuza upatikanaji wa Nishati safi na...

MRADI WA TACTIC KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA

Picha
Sekta ya uvuvi nayo yaguswa.  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  UJENZI wa Barabara ya Buhongwa-Igoma yenye urefu wa Km 14 kwa kiwango cha lami inayojengwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza inatajwa kuwa ndio mwarobaini wa changamoto ya msongamano wa magari jijini humo.  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba wakati akielezea hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Jiji la Mwanza kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji na Majiji Tanzania (TACTIC)  na manufaa yake kwa wananchi. Amesema barabara hiyo inayounganisha Kata nne ambazo ni Buhongwa, Lwanhima, Kishiri na Igoma ilikuwa na changamoto kubwa hali iliyopelekea magari yote yaliyokuwa yakitoka Buhongwa kwenda Igoma au Igoma kwenda Buhongwa kulazimika kuingia katikati ya jiji hivyo kuongeza msongamano wa magari.  Wakili Kibamba ameongeza kuwa  ujenzi wa barabara hiyo utasaidia kupunguza msongamano huo kwa kiasi kikubwa kwani magari yote yaliyokuwa yanatoka maeneo ...

HELKOPTA YAPOTEA NA WATU NANE

Picha
HELKOPTA yenye watu wanane imepotea kwenye kisiwa cha Borneo, Indonesia, na juhudi za uokoaji zimeanza, kwa mujibu wa maafisa wa uokoaji. Kiongozi wa shirika la uokoaji Banjarmasin, I Putu Sudayana, amesema helikopta hiyo ilikuwa na marubani wawili na abiria sita, na wanatarajia kuwapata wote wakiwa salama ndani ya siku saba za utafutaji. #indonesia #borneo #banjarmasin #indonesiahelicopter

CCM YAJIVUNIA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO, YA AHAIDI KUBORESHA ELIMU, MAJI NA VIPAJI VYA VIJANA

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema mafanikio ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini ni kielelezo cha dhamira yake ya kweli katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, na kwamba kinaendelea kujipanga kuimarisha huduma muhimu za kijamii katika kila sekta. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jiji la Dodoma, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, amesema pamoja na mafanikio ya miradi kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, na barabara kuu za lami, CCM ina mpango kabambe wa kuwekeza zaidi katika elimu, maji, miundombinu ya afya na kukuza vipaji vya vijana. “Huduma bora kwa wananchi ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli. Tutaendelea kupeleka umeme kwenye vijiji vilivyobaki, kuboresha miundombinu ya shule na zahanati, na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama,” amesema Mavunde. Ameeleza kuwa serikali kupitia CCM inaendelea kutekeleza programu maalum za kuibua na ...

ISRAELI YADUNGUA KOMBOLA KUTOKA YEMEN

Picha
WAASI wa Houthi wameapa kuiwajibisha #Israel baada Waziri Mkuu wao Ahmed Ghaleb Nasser Al-Rahawi na maofisa wengine 11 wa ngazi ya juu kuuawa katika shambulio la wanajeshi wa Israel wiki iliopita katika Mji wa #sanaa. #HouthiRebels Jeneza la Waziri Mkuu wa Houthi Ahmed al-Rahawi Sept. 1, 2025. 

WAAJIRI WATAKIWA KULIPA STAHIKI ZA MADEREVA KWA WAKATI

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka waajiri wa taasisi za umma kuhakikisha wanalipa stahiki za madereva kwa wakati, kutoa mafunzo ya mara kwa mara, kutekeleza ipasavyo miundo ya ajira na kuwapa motisha ili kuongeza tija katika utendaji kazi wao. Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST), Waziri Mkuu amesema madereva wa Serikali wana mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali na hivyo wanapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa. "Waajiri mnapaswa kuhakikisha madereva wanalipwa stahiki zao kwa wakati, wanapewa mafunzo stahiki na kuzingatiwa katika motisha mbalimbali. Hii itawajengea morali na kuongeza ufanisi katika kazi zao," amesema Majaliwa. Aidha, amesisitiza kuwa madereva wanawajibu wa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kuhakiki usalama wa vyombo vya usafiri, abiria, mizigo na nyaraka za Serikali. “Madereva mnatakiwa kufanya...