Machapisho

NDEGE YA KIVITA YAANGUKA MAZOEZINI

Picha
NDEGE aina ya F-16 imeanguka wakati wa mazoezi ya maonyesho ya ndege mjini Radom, katikati ya Poland, August 28.2025 Rubani alifariki kwa mujibu ya msemaji wa serikali #Poland #mazoeziyakijeshi #ndegeyavita

RAIS MWINYI AISHUKURU SERIKALI YA QATAR

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameshuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kiuchumi katika sekta mbalimbali yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 10. Hafla hiyo imefanyika Ikulu leo tarehe 29 Agosti 2025, ambapo kwa upande wa Qatar mkataba huo ulisainiwa na mmoja wa Wanafamilia ya Kifalme wa Qatar, Mhe. Sheikh Mansour Bin Jabor Bin Jassim Al Thani, ambaye pia ni Mmiliki wa Kampuni ya Al Mansour Holding itakayotekeleza miradi hiyo.  Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, utiaji saini uliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Ndg. Khamis Mwalim Suleiman. Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Qatar kwa kuonesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na Zanzibar katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayohitaji uwekezaji mkubwa. Rais ...

JKT YATOA THANK YOU KWA YAKOUB SULEIMAN

Picha
JKT Tanzania🇹🇿  yaachana rasm na Golikipa Yakoub Suleiman na kuumtakia maisha mema katika majukumu yake mapya. #yakoub_suleiman_ #WajengaNchi #KichapoChaKizalendo

REA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Picha
📌 *Majiko banifu 5,176 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Iringa*  📌 *Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 14,300 tu* . Na Mwandishi Wetu, Iringa.  WAKATI Taifa likiwa kwenye mkakati wa kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi na salama ya kupikia, Wakala wa Nishati Vijijini umekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa  majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku yanayotumia kuni na mkaa mchache sana na yenye ufanisi mkubwa katika matumizi yake. Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa, Mhandisi Kelvin Tarimo amesema, Mradi huu umekuja kwa lengo la kuimarisha utunzaji wa Afya za wananchi na Mazingira, kukuza upatikanaji wa Nishati Safi na Endelevu, kupanua usambazaji wa nishati mbadala katika maeneo ya Vijijini na zaidi kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupitia teknolojia za kisasa na bora za kupikia. Mhandisi Tarimo ameendelea kwa kusema, Serikali kupitia wakala wa Nishati Vijijini umeandaa mpango huu wa usambazaji na uuzaji wa m...

MAAFISA NA ASKARI WA MAGEREZA WAUNGANA NA VYOMBO VINGINE VYA ULINZI MARA KATIKA MAZOEZI YA PAMOJA

Picha
MAAFISA na Askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mara, leo tarehe 29 Agosti 2025 wameshiriki mazoezi ya pamoja ya vyombo vya ulinzi na usalama.

ACP. BAYNITY AWAVISHA VYEO VIPYA ASKARI 15 GEREZA MAWENI TANGA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tanga.  KAIMU Mkuu wa Gereza la Maweni, ACP Nade Slaa Baynity, ameongoza hafla ya kuwavisha vyeo Askari 15 kutoka cheo cha Sajenti (Sgt) kuwa Staff Sajenti (SSgt) wa Magereza.  ACP. Baynity amewapongeza askari hao kwa juhudi na uadilifu waliouonesha kazini, hali iliyowafanya kustahili kupandishwa vyeo na amewataka kuwa viongozi bora kwa wale walio chini yao, wakizingatia kuwa vyeo walivyopata vinaambatana na majukumu mapya hivyo waongeze bidii katika utendaji. Kwa niaba ya Askari waliopandishwa vyeo, SSgt Neema Oswad Mkumbange ametoa shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, CGP Jeremia Yoram Katungu, kwa kuwaamini na kuwapa heshima ya kupandishwa vyeo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kulijenga taifa. #MagerezaTanzania #Wizarayamamboyandani

LEBANON YAZIDI KUHAMISHA SILAHA.

Picha
LEBANON jana ilifanya awamu ya pili ya kuhamisha silaha kutoka kambi za Wapalestina nchini humo hadi kwa jeshi la Lebanon, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Lebanon na vyanzo vya Palestina. Awamu ya pili, ikiwa ni pamoja na malori manane yaliyosheheni silaha za bunduki, roketi za B7, na maguruneti kutoka kambi za Rashidieh, el-Buss, na Burj Al-Shemali, ilifanyika katika kambi ya Kikosi cha Pili cha Kikosi cha Kuingilia Kati cha jeshi katika eneo la Shawakir katika jiji la Tire, kusini mwa Lebanon, Shirika rasmi la Habari la Lebanon liliripoti. Subhi Abu Arab, mkuu wa usalama wa taifa wa Palestina nchini Lebanon, aliuambia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika kambi hiyo ya kijeshi kwamba "silaha zilizokabidhiwa leo na (harakati ya Wapalestina) Fatah (harakati) wa jeshi la Lebanon ni pamoja na, pamoja na silaha nyepesi, mabomu ya ardhini na maroketi ya ardhini ya Grad." Wakati huo huo, Ramez Dimashkieh, mkuu wa Kamati ya Mazungumzo ya Lebanon na Palestina, ameuam...

DKT ASHA -ROSE MIGIRO AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUMTEUA KUWA KATIBU MKUU WA CCM

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma KATIBU Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt, Asha-Rose Migiro, amemshukuru kwa dhati Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumteua kushika nafasi hiyo muhimu ndani ya chama. Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo katika viwanja vya Makao makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (whitehouse) Dodoma Dkt, Migiro amesema uteuzi huo ni heshima kubwa na dhamana ya kuendeleza misingi ya uongozi wa chama, huku akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa weledi, bidii, na uaminifu mkubwa. “Ninatoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuniamini na kunipa jukumu hili ni heshima kubwa kwangu, na naahidi kulitumikia chama chetu kwa moyo wangu wote,” amesema Dkt. Migiro. Aidha amewataka wanachama hao kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu unaotaraji kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.  Pmoja na haya amewashukuru wanachama wa CCM kwa mapokezi mazuri aliyoyapata, akisema kuwa ni ishara ya mshi...

AKILI UNDE YATAWALA MKUTANO WA KAHRDC NA FAC

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  MKURUGENZI wa Masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Mwesigwa Felician akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Kamati ya Utawala (HRDC) na Fedha (FAC) ya Shirika la Wasimamizi wa Huduma za Mawasiliano wa Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (CRASA), tarehe 25 Agosti, 2025 jijini Dar es Salaam.  Katika ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe wameshiriki majadiliano kuhusu matumizi ya Akili Unde kwa wataalamu wa rasilimali watu “ Artificial Intelligence for Human Resources Professionals”.   Mkutano huo unaoratibiwa na TCRA unafanyika kuanzia Agosti 25 hadi 29, katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Serena. #tcratz #digitaleconomy #crasa #regionalintegration #uchumiwakidijiti #hrdc #fac

MAANDALIZI YA KUELEKEA MIAKA 64 YA MAGEREZA YAKAMILIKA.

Picha
MAANDALIZI yamekamilika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 64 ya Jeshi la Magereza Baada ya Uhuru, ambayo yatafanyika Agosti 26, 2025 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga Dar Es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.