ACP. BAYNITY AWAVISHA VYEO VIPYA ASKARI 15 GEREZA MAWENI TANGA


Na Mwandishi Wetu, Tanga. 

KAIMU Mkuu wa Gereza la Maweni, ACP Nade Slaa Baynity, ameongoza hafla ya kuwavisha vyeo Askari 15 kutoka cheo cha Sajenti (Sgt) kuwa Staff Sajenti (SSgt) wa Magereza. 

ACP. Baynity amewapongeza askari hao kwa juhudi na uadilifu waliouonesha kazini, hali iliyowafanya kustahili kupandishwa vyeo na amewataka kuwa viongozi bora kwa wale walio chini yao, wakizingatia kuwa vyeo walivyopata vinaambatana na majukumu mapya hivyo waongeze bidii katika utendaji.

Kwa niaba ya Askari waliopandishwa vyeo, SSgt Neema Oswad Mkumbange ametoa shukrani kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, CGP Jeremia Yoram Katungu, kwa kuwaamini na kuwapa heshima ya kupandishwa vyeo na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kulijenga taifa.









#MagerezaTanzania #Wizarayamamboyandani

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.