Machapisho

ASKARI WANAFUNZI 15 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI.

Picha
Na Lubango Mleka, Moshi.  ASKARI Wanafunzi 15 wamejeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo aina ya Fuso katika eneo la Kwasadala, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro. Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu amesema askari hao walikuwa wakitokea eneo la mazoezi ya medani za kivita la Kilele Pori, lililoko wilayani Siha, wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser lililogongana uso kwa uso na Fuso. Majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea leo Agosti 12, saa sita mchana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Hospitali ya Wilaya ya Hai. 

TCRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHII NA SALAMA YA HUDUMA YA MAWASILIANO.

Picha
MENEJA wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Ofisi ya Zanzibar, Bi. Esuvatie-Aisa akitoa dondoo muhimu kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano katika kipindi maalumu cha Kituo cha Crown FM Zanzibar tarehe 12 Agosti, 2025 Unguja - Zanzibar.  TCRA inaendelea kutoa elimu kwa umma ikisisitiza matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano na kukumbusha wajibu wa watumiaji wa kusambaza taarifa za ukweli na uhakika na kufuta na kutosambaza ujumbe au taarifa zinazochochea upotoshaji, uzushi, chuki na uvunjifu wa amani. #tcratz #elimukwaumma #futadeletekabisa

WACHIMBAJI WADOGO 25 KATIKA MGODI WA NYANDOLWA WAMEFUKIWA NA KIFUSI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.  JUMLA ya wachimbaji wadogo 25 katika mgodi mdogo wa Nyandolwa uliopo kijiji cha Mwongozo Halmashauri ya Shinyanga, wamefukiwa na kifusi baada ya mgodi kutitia. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wachimbaji katika eneo hilo wamefanya juhudi za kuwaokoa wachimbaji hao na tayari wachimbaji wawili wameokolewa. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro amesema kuwa wachimbaji hao walikuwa katika mashimo matatu tofauti, ikiwemo shimo la duara namba 106 lenye watu 6, 103 lenye watu 11, na duara namba 20 lenye watu 8. Juhudi za uokoaji bado zinaendelea. Tukio la kutitia kwa mgodi huo limetokea Agosti 11, 2025 saa nne asubuhi, wakati shughuli za matengenezo ya maduara hayo zikiendelea. Mtatiro amewasihi wachimbaji kuwa watulivu wakati jitihada za kuokoa uhai wa walioko chini zikiendelea.

VIWANGO VYA KUBADIRISHIA FEDHA ZA KIGENI HAPA NCHINI.

Picha

RAIS MWINYI:SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MASLAHI YA WALIMU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia walimu kuwa Serikali itaendelea kuimarisha maslahi na mazingira ya ufundishaji na kujifunza kwa dhamira ya kuboresha elimu zaidi.  Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 12 Agosti 2025, katika kongamano la kumpongeza lililoandaliwa na Shirikisho la Walimu Zanzibar kufuatia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu nchini katika kipindi cha uongozi wake. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa, katika kuongeza motisha kwa walimu, Serikali imeboresha maslahi yao kwa kuongeza mishahara, posho za likizo na ufiwa, pamoja na kulipa malimbikizo mengine. Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali  imeajiri walimu wapya 5,265 na kuwapatia mafunzo mbalimbali ili kuongeza ufanisi wao. Ameeleza kuwa kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kimetumika katika mwaka wa ...

JESHI LA POLISI LATAKIWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WADAU WA UCHAGUZI NCHINI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Moshi.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema ni muhimu Jeshi la Polisi kuimarisha ushirikiano wa karibu na wadau wote wa uchaguzi, hatua ambayo itasaidia kuhakikisha kila mdau anatendewa haki, na kuondoa tofauti zinazoweza kusababisha migongano.   Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) Moshi Mkoani Kilimanjaro. Amesema Baadhi ya maeneo muhimu ya ushirikiano ni pamoja na kuhakikisha mikutano ya kampeni inafanyika kwenye maeneo yaliyoruhusiwa na ndani ya muda uliopangwa,  Kuzuia maandamano yasiyo na kibali, kuimarisha ulinzi wa wagombea na viongozi wa vyama vya kisiasa, bila kujali vyama vyao au itikadi zao pamoja na kudhibiti misongamano mikubwa ya watu ili kuhakikisha shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi zinaendelea bila usumbufu.   Pia Makamu wa Rais amelitaka Jeshi la Polisi ku...

RAIS MWINYI ATEMBELEA ENEO LA OFISI ZA MJI WA SERIKALI NA LINALOJENGWA UWANJA MPYA WA AFCON

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi mkubwa wa uwanja wa AFCON pamoja na miundombinu mbalimbali inayojengwa Fumba, hivyo ni muhimu kubaini mapema maeneo yatakayotumika kwa mradi huo ili kuepusha mwingiliano wa matumizi ya ardhi katika eneo hilo kati ya taasisi husika. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 11 Agosti 2025, katika kikao maalum na mawaziri mbalimbali akiwemo Mhe. Rahma Kassim Ali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mhe. Shariff Ali Shariff, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mhe. Tabia Maulid Mwita, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, pamoja na Taasisi ya Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB), kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja kuhusu matumizi sahihi ya ardhi katika maeneo ya uweke...

MADEREVA, ABIRIA WAPATIWA ELIMU YA USALAMA BARABARANI NA MATUMIZI SAHIHI YA VYOMBO VYA KUZIMIA MOTO IGUNGA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga.  MADEREVA na Abiria katika Kituo cha Mabasi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora wamepatiwa Elimu ya Usalama Barabarani na Mabalozi wa Usalama Barabarani Wilaya ya Igunga (RSA) yenye lengo la kuendelea kuwakumbusha Madereva na Abiria kufuata sheria za usalama barabarani ili kunguza ajali zitokanazo na ubovu wa magari na uzembe wa Madereva.  Elimu hiyo imetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la Road Safety Ambassadors (RSA) kwa kushirikiani na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani na Jeshi la Zimamoto wilaya ya Igunga ambapo wametoa Elimu ya Usalama Barabarani, Wajibu na Haki za Abiria, Elimu ya tahadhari  ya majanga ya Moto pia imbeambatana na zoezi la ukaguzi wa magari, vifaa vya kuzimia moto na ukaguzi wa leseni kwa madereva.  Akitoa Elimu ya tahadhari ya majanga ya moto Koplo Shadrack Mweya kutoka Jeshi la Zimamoto amewataka madereva kuhakikisha magari yao yanakuwa na vifaa vya kuzimia moto ambavyo havijaisha muda wa matumizi, milan...

RAIS MWINYI:SMZ ITAENDELEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA USAJILI KIDIJITALI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya usajili kidijitali wa matukio ya kijamii kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya nchi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 10 Agosti,  2025 katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Usajili Barani Afrika yaliyofanyika katika Ukumbi wa Idrissa Abdulwakil, Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi. Ameeleza kuwa hatua hiyo itaongeza ufanisi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi unaofanywa na Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) katika usajili wa vizazi, vifo, talaka, ndoa na vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi. Rais Dkt. Mwinyi amesema hakuna maendeleo ya kweli bila usajili wa utambulisho wa wananchi katika mifumo imara inayotambulika kisheria na inayotumia teknolojia ya kisasa ya kidijitali. Aidha, Dkt. Mwinyi ametoa rai kwa ZCSRA kuanzisha kampeni maalum kwa kushirikiana na masheha kuha...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Picha