UJENZI WA JENGO LA UBIA KATI YA NHC NA TOSH LOGISTICS KARIAKOO.
Na Mwandishi Wetu, Kariakoo- Dar es Salaam. SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ubia na Tosh Logistics Ltd linaendelea na ujenzi wa jengo la kisasa la biashara na makazi katika eneo la Tandamti, Kariakoo – Dar es Salaam. Mradi huu unaojengwa kwenye viwanja sita (3/16 hadi 14/16) unalenga kubadilisha sura ya Kariakoo kwa kujenga majengo ya kisasa yenye matumizi mchanganyiko. Jengo limegawanywa katika Block A na Block B ambapo kazi zinasonga mbele kwa kasi, block A ipo hatua ya ujenzi wa ghorofa ya pili, block B imefikia ghorofa ya sita. Mradi huu unatekelezwa kuanzia Oktoba 15, 2024 hadi Oktoba 15, 2026, ni sehemu ya jitihada za NHC kukuza miundombinu ya kisasa na kuchochea uwekezaji kwenye maeneo ya mijini kupitia ubia wa kimkakati na sekta binafsi. #NHCProjects #ToshLogistics #MajengoYaKisasa #KariakooMpya #UjenziEndelelevu #PublicPrivatePartnership #MaishaNiNyumba#CrownMedia #Ayotv