Machapisho

WAKAZI USUNGA WAFURAHIA MRADI WA MAJI

Picha
  Na Allan Kitwe, Sikonge.  WAKAZI wa Kijiji Cha Usunga, Kata ya Usunga Wilayani Sikonge Mkoani Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea mradi wa maji safi na salama ya kunywa. Wametoa shukrani hizo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 58 tangu kuanzishwa kwa Kijiji hicho zilizofanyika jana kwenye uwanja wa CCM (Centre) na kueleza bayana kuwa serikali imemaliza kilio chao cha muda mrefu. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho James Mgulu ameeleza kuwa mradi wa maji katika Kijiji hicho umeleta neema, furaha na shangwe kwa wananchi kwa sababu familia zao zilikuwa zinapata shida sana kwa kukosa maji safi na salama. ‘Tuna kila sababu ya kuishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu wa maji na miradi mingine ya maendeleo, wananchi sasa wana amani tele, na maisha yao yamekuwa bora zaidi’, ameeleza.  Ameongeza kuwa wanapoadhimisha sherehe hiyo kila mwaka wanalenga kudumisha mila, utamad...

MIUNDOMBINU CHUO CHA NYUKI TABORA YABORESHWA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  CHUO Cha Ufugaji Nyuki (BTI) Tabora kimeendelea kuboresha miundombinu yake kwa kujenga jengo jipya la kisasa la mihadhara linalogharimu zaidi ya shilingi milioni 500, utekelezaji mradi huu umefikia zaidi ya asilimia 48. Hayo yameelezwa jana na Mkuu wa Chuo hicho Semu Daud alipokuwa akiongea na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake, ambapo ameeleza kuwa jengo hilo litaboresha ufundishaji wa wakufunzi na kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa chuoni hapo. Amefafanua kuwa ujenzi wa jengo hilo unafadhiliwa na Mfuko wa Misitu Tanzania (TAFF) ambao wametoa kiasi cha shilingi milioni 500 sawa na asilimia 82 huku shilingi milioni 92 sawa na asilimia 20 zikitoka kwenye mfuko wa chuo. Ukumbi huo utakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 kwa wakati mmoja hivyo kukamilika kwake kutatoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kujiunga na fani ya ufugaji nyuki. Mkuu amedokeza kuwa kupitia mradi huo mbali na wanafunzi kuongezeka chuoni hapo pia utasaidia kufa...

WILAYA YA LUSHOTO YAPOKEA MRADI WQ USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MITUNGI YA GESI KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Lushoto - Tanga.  WANANCHI wa Wilaya ya Lushoto wamepata fursa mpya ya kunufaika na nishati safi ya kupikia baada ya wilaya hiyo kupokea rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).  Mradi huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mheshimiwa Zephania Sumaye, kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuhakikisha nishati safi ya kupikia inawafikia Watanzania wengi zaidi. Hafla ya mapokezi ya mradi huo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, maafisa kutoka REA pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Manjis Logistics Limited, ambayo imepewa jukumu la kutekeleza mradi huo kwa kushirikiana na REA. Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na REA nchini kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa nishati safi na salama kwa wananchi, kupunguza utegemezi wa kuni ...

ZAIDI YA WAKULIMA 200 WA ZAO LA PAMBA WAFUNGUA AKAUNTI IGUNGA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Igunga.  ZAIDI ya wakulima 200 wa zao la pamba kutoka vijiji vya Mwahalanga, Bukama, Mwabakima, Jogoya na Jilelabalimi vilivyopo katika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora, wamefungua akaunti za benki na kusajili laini za simu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupokea malipo ya mazao yao kwa njia ya kidijitali, hatua inayolenga kuongeza uwazi, usalama na uharaka wa malipo. Wakulima hao wamefungua akaunti kupitia Benki ya NMB pamoja na kusajili laini kupitia Mtandao wa simu wa Mixx by Yas, hatua ambayo itawawezesha kupokea fedha zao kwa urahisi kupitia mifumo ya benki na simu za mkononi. Ufunguzi wa akaunti hizo na usajili wa laini za simu unatekelezwa kufuatia maelekezo ya waraka wa Mrajis wa Vyama vya Ushirika unaozitaka AMCOS za wakulima wa pamba kuhakikisha malipo ya wakulima yanafanyika kupitia akaunti za benki na huduma za fedha kwa njia ya simu, badala ya kutumia mfumo wa malipo ya fedha taslimu (cash).  Lengo la hatua hiyo ni kuongeza uwazi, usalam...

TANZANIA NA UTURUKI KUIMARISHA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA

Picha
  Na Lubango Mleka.  WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga, akiwa katika ziara ya kikazi nchini Uturuki Juni 06, 2026, Jijini Istanbul amefanya mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Teknolojia wa Uturuki, Mehmet Fatih Kacır pamoja na Waziri wa Biashara wa Uturuki, Ömer Bolat, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na viwanda kati ya nchi hizi mbili. Mazungumzo na Waziri Kacır yamejikita katika kukuza maendeleo ya viwanda vya kimkakati, kuimarisha matumizi ya teknolojia, pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda rafiki kwa mazingira. Mhe. Kapinga ameeleza dhamira ya serikali ya kutumia ushirikiano huo kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya mwaka 2050 ya kuwa nchi ya kipato cha kati cha juu kupitia mageuzi ya sekta ya viwanda, huku Uturuki ikiahidi kuendeleza ushirikiano wa kiufundi, kiteknolojia na ubunifu kwenye sekta hiyo. Kwa upande wa biashara, mazungumzo na Waziri Bolat yamejikita katika kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji na kuongeza kiwango cha ...

CSP na VI AGROFORESTRY WAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI 1,200

Picha
  Na Mwandishi wetu, Babati  SHIRIKA lisilo la kiserikali la Civic Social Protection Foundation (CSP) na Vi Agroforestry wameadhimisha siku ya mazingira duniani kwa kupanda miti 1,200 na kufanya shughuli mbalimbali za uhifadhi wa mazingira Mjini Babati, Mkoani Manyara. Mwanasheria wa CSP Eliakim Paul, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ameeleza kuwa shirika hilo hiyo limeendelea kushirikiana na jamii katika juhudi za kulinda mazingira kupitia upandaji miti, elimu ya mazingira na shughuli za usafi. Eliakim amesema katika maadhimisho ya mwaka huu wa 2026 wamepanda miti 1,200 ya matunda, mbao na kivuli kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo shule ya msingi Malangi, zahanati ya Malangi, shule za sekondari FT Sumaye na Himiti na ofisi ya kijiji cha Himiti.  Amesema pia wamegawa miti hiyo kwa mtu mmoja mmoja ili kuhamasisha utunzaji wa mazingira katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla. "Sambamba na zoezi la upandaji miti, shughuli za usafi wa mazingira zimefanyika katika shule ...

WAKAZI USUNGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora.  WAKAZI wa Kijiji Cha Usunga, Kata ya Usunga Wilayani Sikonge Mkoani Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea mradi wa maji safi na salama ya kunywa. Wametoa pongezi hizo jana kwenye shamra shamra za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 58 tangu kuanzishwa kwa Kijiji hicho ambacho kimekuwa mfano wa kuigwa kwa kudumisha mila, utamaduni, mshikamano na ulinzi wa jadi. Akizungumza na wananchi kwenye shamrashamra hizo zilizopambwa na ngoma, burudani, chakula cha asili na vinywaji, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho James Mgulu ameishukuru serikali kwa kumaliza kero ya maji katika Kata hiyo. Amefafanua kuwa tangu kuanzishwa kwake wakazi wa Kijiji hicho wameendeelea kunufaika na mambo mengi mazuri yanayofanywa na serikali yao ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo kudumisha umoja, amani na mshikamano.   Akielezea kiini cha sherehe hiyo, Diwani wa Kata hiyo Jackson Mbasha amesema kuwa utaratibu...

KAPINGA: DHANA YA TAKA SIFURI INAFUNGUA FURSA ZA BIASHARA NA VIWANDA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Istanbul-Ururuki.  WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa ni fursa muhimu ya kukuza sekta ya viwanda, kuongeza thamani ya malighafi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza katika kikao cha mawaziri kilichofanyika jijini Istanbul nchini Uturuki, Juni 5, 2026, kilichobeba mada ya Mageuzi ya Kijani ya Viwanda, Mtazamo wa taka sifuri na urejeshaji bidhaa, Kapinga amesema Tanzania inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta ya viwanda huku ikisisitiza matumizi bora ya rasilimali na uhifadhi wa mazingira. Ameeleza kuwa dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa inatoa fursa kwa nchi zinazoendelea kupitia matumizi endelevu ya malighafi, kupunguza upotevu baada ya mavuno, kupunguza uzalishaji wa taka na kuongeza thamani ya bidhaa zinazotengenezwa viwandani. Kapinga amesema Serikali ya Tanzania imeendelea kuunganisha masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika s...

OLE MILLYA AKEMEA UUZWAJI ARDHI SIMANJIRO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki James Ole Millya ambaye pia ni Mbunge wa Simanjiro Mkoani Manyara, amekemea vikali uuzwaji holela wa ardhi unafanywa baadhi ya viongozi wa vijiji. Ole Millya ameyasema hayo katika Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro, kwenye ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Laban Kihongosi alipohitimisha ziara yake ya siku tatu Mkoani Manyara. Amesema tatizo la uuzwaji holela wa ardhi katika wilaya ya Simanjiro, limekuwa kero kwani baadhi ya viongozi wa vijiji wenye tamaa wanagawa ardhi kwa maslahi yao  "Baadhi ya wenyeviti wanauza ardhi bila kushirikisha mkutano mkuu wa kijiji na baadhi ya wenyeviti wastaafu wanatembea na mihuri na mihutasari iliyopita katika uuzaji wa ardhi," amesema Ole Millya. Ameeleza kwamba wakati mwingine anaona ni vyema hata miradi ya maendeleo isifanyike kwa muda wa mwaka mmoja ili viongozi na jamii kwa ujumla ishuhulikie migogoro ya ar...