BABA AMICHINJA MTOTO WAKE MCHANGA
Na Allan Kitwe, Igunga MWANAUME mmoja mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamakona, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora amemchinja mtoto wake mchanga aliyekuwa na umri wa miezi miwili na kumjeruhi vibaya mke wake. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa , Richard Abwao ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 25 mwaka huu majira ya saa 3 usiku huko katika Kitongoji cha Ibindo, kijiji cha Imalanguzu. Amebainisha kuwa mwanaume aitwaye Bunzali Jidola (30) Msukuma, mkulima, mkazi wa Imalanguzu alimchinja kwa kutumia kitu chenye ncha kali mtoto wake aitwaye Dorcas Bunzali aliyekuwa na umri wa miezi miwili. Ameongeza kuwa baada ya mauaji hayo alimjeruhi pia mke wake aitwaye Jeni Ndaki (24) Msukuma, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Ibutamisuzi kwa kutumia kifaa hicho chenye ncha kali na kisha kutokomea kusiko julikana. Amesema majeruhi huyo aliokolewa na wasamaria wema na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyoko Wilayani humo ...