Machapisho

BABA AMICHINJA MTOTO WAKE MCHANGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Igunga MWANAUME mmoja mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu, Kata ya Mwamakona, Tarafa ya Igurubi, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora amemchinja mtoto wake mchanga aliyekuwa na umri wa miezi miwili na kumjeruhi vibaya mke wake. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa , Richard Abwao ameeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 25 mwaka huu majira ya saa 3 usiku huko katika Kitongoji cha Ibindo, kijiji cha Imalanguzu. Amebainisha kuwa mwanaume aitwaye Bunzali Jidola (30) Msukuma, mkulima, mkazi wa Imalanguzu alimchinja kwa kutumia kitu chenye ncha kali mtoto wake aitwaye Dorcas Bunzali aliyekuwa na umri wa miezi miwili. Ameongeza kuwa baada ya mauaji hayo alimjeruhi pia mke wake aitwaye Jeni Ndaki (24) Msukuma, mkulima, mkazi wa Kijiji cha Ibutamisuzi kwa kutumia kifaa hicho chenye ncha kali na kisha kutokomea kusiko julikana. Amesema majeruhi huyo aliokolewa na wasamaria wema na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga iliyoko Wilayani humo ...

WAKULIMA TABORA WANUFAIKA NA MNADA WA KWANZA WA KOROSHO

Picha
  Na Lubango Mleka, Tabora.  WAKULIMA wa zao la korosho mkoani Tabora wameanza kunufaika na fursa ya soko baada ya kuanza kwa mnada wa kwanza wa zao hilo, ambapo zaidi ya kilo elfu kumi na tatu zimeuzwa katika siku ya ufunguzi. Mafanikio hayo yameelezwa kuwa ni ishara ya kukua kwa zao la korosho mkoani humo, huku matarajio ya awali yakiwa ni kuuza kilo elfu kumi pekee. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Shabani Katalambula, amesema mwitikio wa wakulima ni mkubwa na unaonyesha wazi kuwa zao hilo linaweza kuwa tegemeo jipya la kiuchumi kwa wakazi wa Tabora. Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa kampuni ya Mateak Holdings Ltd, Violet Mordichai, amesema wamejikita katika kuwajengea uwezo wakulima kupitia elimu ya kilimo bora cha korosho, akisisitiza matumizi ya pembejeo ili kuongeza uzalishaji na ubora wa mazao. Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora , Bi Upendo Wella, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, amewataka wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ili kuwa na nguvu ya pamo...

VIJANA ZAIDI YA 60 WALIOHITIMU FDC NZEGA WAPATA AJIRA

Picha
  Na Allan Kitwe, Nzega.  TAASISI, Mashirika ya Umma na makampuni binafsi yamepongezwa kwa kutoa fursa za ajira kwa vijana wa kike na kiume wanaohitimu mafunzo ya ufundi katika fani mbalimbali kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) . Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Nzega (Nzega FDC) Nichodemus Shirima alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliomtembelea Ofisini kwake jana ili kujionea maendeleo ya chuo hicho. Ameshukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuvifanyia maboresho makubwa vyuo vyote vya maendeleo ya wananchi nchini na kuvipatia vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia hali ambayo imechochea vyuo hivyo kutoa elimu bora. ‘Zaidi ya vijana sitini (60) waliohitimu fani mbalimbali katika chuo chetu hapa Nzega wamepata ajira rasmi katika taasisi mbalimbali za umma na makampuni ya watu binafsi na wengine wamejiajiri na wanapata kipato cha uhakika’, ameeleza. Shirima amefafanua vijana walioajiriwa kuwa ni wa fani za ufundi bomba (zaidi...

MMOJA AFARIKI, WAWILI WAJERUHIWA WAKIBISHANIA SIMBA NA YANGA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MTU mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kutokea ugomvi uliozuka kutokana na ushabiki wa mpira kati ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza. Kwa mujibu taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amesema tayari wameanzisha msako wa kumtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa) kwa tuhuma za kumuua Abel Mganga Mazuri (25) mkazi wa Nyamahengo, na kuwajeruhi watu wawili kufuatia ugomvi uliotokana na ushabiki wa mpira. Taarifa hiyo imesema tukio hilo limetokea Machi 24, 2026 majira ya saa 5:30 usiku katika kitongoji cha Nyamahengo, kijiji na kata ya Sumve, wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. "Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeanza msako wa kumtafuta kijana mmoja (jina limehifadhiwa kwa sasa) kwa tuhuma za mauaji ya Abel Mganga Mazuri, miaka25, mkazi wa Nyamahengo aliyeuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani kisha kuwajeruhi watu wawili kwa kutumia kitu c...

FDC URAMBO WAJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA

Picha
  Na Allan Kitwe, Urambo.  CHUO Cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Urambo kimeishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu na kukipatia vifaa vya mafunzo ambavyo vimekiongezea mapato. Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Chuo hicho Elias Niima alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake ambapo alieleza kufurahishwa na uamuzi wa serikali ya Awamu ya Sita kukifanyia maboresho makubwa chuo hicho.   Amesema kuwa kipindi cha miaka 4 ya Uongozi wa Rais Samia na siku 100 za awamu yake ya pili tangu aingie madarakani, chuo kimepata mafanikio makubwa ikiwemo kuzalisha samani za taasisi mbalimbali na kuingiza mapato. Ametaja baadhi ya samani zilizotengenezwa kuwa ni madawati, viti na meza zaidi ya 7,000 kwa shule za msingi na sekondari za halmashauri za Wilaya ya Urambo na 2,500 za halmashauri ya Wilaya ya Kaliua. ‘Miradi hii imetekelezwa na Chuo kwa kutumia nguvu kazi ya wanafunzi na walimu wao, ikiwa ni sehe...

TAKUKURU, TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA YASAINI MIKATABA YA KUDHIBITI RUSHWA.

Picha
  Na Hamida Ramadhan,  Dodoma.  TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika zimesaini makubaliano ya ushirikiano yatakayolenga kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa katika vyama vya ushirika nchini.  Hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji, uwazi na kurejesha imani ya wanachama wa ushirika. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Msajili na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, alisema sekta ya ushirika imekuwa ikikabiliwa na changamoto za usimamizi wa rasilimali, ambazo kwa kiasi kikubwa zimechangiwa na vitendo vya rushwa. Alieleza kuwa wanachama wengi wamekuwa wakiweka fedha, mazao na rasilimali zao katika vyama vya ushirika kwa matarajio ya kunufaika, lakini vitendo vya rushwa vimekuwa vikikwamisha malengo hayo na kupunguza imani yao. “Ushirikiano huu unalenga kukomesha vitendo vya rushwa na kurejesha matumaini ya wanachama tumejipanga kuhakik...

REA YAENDELEZA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KOROGWE.

Picha
  Wananchi Wanufaika na usambazaji na uuzaji wa Mitungi ya Gesi kwa bei ya ruzuku.  Na Mwandishi Wetu, Korogwe - Tanga.  WANANCHI wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga  wameanza kuona mwanga mpya wa maisha kufuatia kuendelea kwa mpango wa usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).  Mpango huo unaolenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, umeleta matumaini mapya kwa kaya nyingi zilizokuwa zikitegemea kuni na mkaa. Katika muendelezo wa zoezi hilo, REA imeendelea kusambaza mitungi ya gesi kwa gharama nafuu, hatua inayolenga kuhakikisha hata wananchi wa kipato cha chini wanapata fursa ya kutumia nishati salama na rafiki kwa mazingira.  Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Msimamizi wa mradi kutoka REA, Ndugu Abdulrazack Mkomi ameeleza kuwa jitihada hizo ni sehemu ya mkakati mpana wa serikali wa kupunguza utegemezi wa nishati za jadi ambazo zimekuwa zikichangia uharibifu wa mazi...

RAIS SAMIA ALETA NEEMA KWA MABINTI WALIOKOSA ELIMU SIKONGE

Picha
Na Allan Kitwe, Sikonge MABINTI zaidi ya 34 waliokosa fursa ya kupata elimu ya sekondari Wilayani Sikonge Mkoani Tabora wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwapa fursa ya kupata elimu hiyo kwa miaka miwili pasipo kulipa gharama yoyote. Mabinti hao ambao wengi wao walikatishwa masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo hali duni ya maisha ya wazazi wao, kupata ujauzito, kukatishwa masomo ili waozeshwe katika umri mdogo na mtizamo hasi wa wazazi wao kuhusu elimu. Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Wilayani humo jana walimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa kwa watoto wa kike waliokosa elimu kurudi shuleni. Watoto hao licha ya kupata fursa ya kusoma elimu ya sekondari bure kwa miaka 2 (QT) pia wanasoma masomo ya ufundi stadi ambapo kila mmoja anasoma fani anayopenda, hii inampa fursa ya kupata elimu ya sekondari na ujuzi wa ufundi pia. Miracle Mvungu (25) kutoka Kata ya Igigwa Wilayani humo ameeleza kuwa baada ya kumal...