Machapisho

NUKUU KUTOKA UN.

Picha
WAKATI dunia inaendelea kutumia fedha nyingi zaidi kwenye silaha na maandalizi ya vita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anakumbusha kwamba, usalama wa kweli haujengwi kwa silaha, bali kwa imani, mazungumzo na utu wa binadamu. "Kupunguza silaha si jambo la kusubiri hadi amani ipatikane. Ni hatua ya kuzuia vita kabla havijaanza. Ni njia ya kujenga uaminifu kati ya mataifa. Ni kulinda maisha na mustakabali wa dunia yetu."  Sanamu ya Bunduki Iliyofungwa Fundo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York City inaendelea kuwa ukumbusho kwamba amani huanza pale vurugu zinapokoma. #UN #habarikamilitv #USA #IRAN #URUSI # CHINA

SERIKALI YA RAIS SAMIA YATANGAZA KUNUNUA NDEGE MPYA NANE KWA MWAKA HUU

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  MSEMAJI Mkuu wa serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa leo Alhamisi Februari 26, 2026 amewaambia waandishi wa habari Mjini Dar Es Salaam kuwa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa mwaka huu imepanga kununua ndege mpya nne kati ya nane walizopanga kununua ili kuongeza fursa kwa watanzania katika masoko ya kikanda na Kimataifa pamoja na kusisimua uchumi na Utalii wa Tanzania kama ilivyoahidiwa katika Kampeni za uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Dar Es Salaam, Msigwa amesema  ndege zitakazonunuliwa ni aina ya Bombardier Q400 kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa serikali katika kuimarisha mtandao wa huduma za usafiri wa anga ili kuwa kichocheo muhimu cha Utalii, biashara na usafiri. "Mimi nipo hapa kuwahakikishia kwamba katika lengo hili tumepata mafanikio makubwa, shirika letu sasa hivi tumepata mafanikio makubwa ambapo tumeanza kutajwa kama Shirika...

SERIKALI YATENGA BILIONI 5 KUFADHILI UZAMIVI DATA SCIENCE NA AI KUPITIA SAMIA SCHOLARSHIP

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  Serikali imetenga Shilingi bilioni 5 kufadhili wanafunzi 20 wa Shahada ya Uzamili katika fani za Sayansi Takwimu (Data Science), Akili Unde (Artificial Intelligence) na Sayansi Shirikishi kupitia mpango wa Samia Scholarship Extended (SSE DS/AI+), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa taifa kuimarisha rasilimali watu katika teknolojia za kisasa. Wanafunzi 10 tayari wameanza masomo yao katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), huku wengine 10 wakitarajiwa kuanza katika Indian Institute of Technology Zanzibar. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema mpango huo maalum wa ufadhili wa uzamili umeanzishwa kwa kuzingatia mahitaji makubwa ya taifa katika maeneo ya teknolojia, ubunifu na uchambuzi wa takwimu. “Vyuo tunavyopeleka wanafunzi wa Samia Scholarship AI/DS+ vinatoa fursa ya mafunzo kwa vitendo katika makampuni makubwa ya teknolojia na vinaendelea kud...

MGODI WA ITRACOM WACHANGIA SHILINGI BILIONI 1.29 MAPATO YA SERIKALI MANYARA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Manyara.  MGODI wa Itracom Fertilizer Limited unaojihusisha na uchimbaji na uchakataji wa madini ya phosphate uliopo  katika eneo la Vilima Vitatu, Wilayani Babati mkoani Manyara, umechangia Shilingi Bilioni 1.29 katika mapato ya Serikali tangu kuanza kwa shughuli zake mwaka 2023. Hayo yamebainishwa na Mjiolojia, Waziri Mkupe, akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Manyara, Godfrey Nyanda, ambapo amesema mapato hayo yametokana na mrabaha na ada ya ukaguzi wa madini. Amesema tangu kuanza kwa uzalishaji, mgodi huo umezalisha jumla ya tani 69,929 za madini ya phosphate zenye thamani ya Shilingi Bilioni 36.99, ambazo zimeuzwa katika soko la ndani na nje ya nchi, hususan Nala mkoani Dodoma na nchini Burundi. Kwa mujibu wa Mkupe, mchango huo umeimarisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuchochea maendeleo ya jamii inayozunguka mgodi kupitia utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Ameeleza kuwa tangu kuanza kwa shughuli zak...

MANISPAA TABORA YATOA TUZO KWA WADAU WA MAENDELEO

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora HALMASHAURI ya Manispaa Tabora imetoa tuzo maalumu kwa wadau zaidi ya 10 ambao wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na halmashauri hiyo ikiwemo kuchangia shughuli za kitaifa. Akikabidhi tuzo hizo jana kwenye kikao cha madiwani Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Ghullam Hussein Remtullah amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Dkt John Pima kwa kuandaa tuzo hizo. Ameeleza kuwa tuzo hizo ni muhimu sana kwa kuwa zinadumisha ushirikiano na mahusiano mazuri na wananchi wanaojitolea kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo matukio makubwa ya kitaifa yanayofanyika katika manispaa hiyo. ‘Hawa tunaowapa tuzo leo ni wakulima, wafanyabiashara na wafugaji ambao wamekuwa wakijitolea kwa hali na mali kuishika mkono halmashauri ili kufanikisha mambo mbalimbali, walitoa chakula, fedha na mifugo’, amesema. Mstahiki Meya amebainisha kuwa manispaa inatambua na kuthamini mchango wao ndiyo maana leo wamekabidhiwa tuzo hizo, aliwaomba kuendele...

MALALAMIKO YA VIWANJA MBADALA YAPATIWA UFUMBUZI DODOMA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeyapatia ufumbuzi malalamiko ya muda mrefu ya viwanja mbadala kwa wananchi wa jiji la Dodoma. Suluhisho hilo linafuatia malalamiko ya takriban wananchi 4000 wa jiji la Dodoma wanaodai viwanja na halmashauri ya jiji la Dodoma kuwapa ahadi bila kutekeleza mpaka sasa. Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 25 Februari 2026 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo wakati akizungumza na wananchi wenye migogoro ya ardhi katika eneo la Mahomanyika lilopo kata ya Nzuguni jijini Dodoma. Dkt Akwilapo amesema, eneo la Mahomanyika ni eneo la serikali hivyo lipangwe na kupimwa kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya meneo mbalimbali ya jiji la Dodoma pamoja na matumizi ya serikali. "Eneo hili lenye mgogoro hapa Mahomanyika ni eneo la serikali hivyo lipangwe na kupimwa kwa ajili ya utatuzi wa migogoro na siyo ya hapa tu na mingine ya jiji la Dodoma na matumizi ya serikali...

TAKUKURU MKOA WA MWANZA IMEFANIKIWA KUDHIBITI KIASI CHA TZS MILIONI 85.5

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kudhibiti kiasi cha Sh milioni 85.5 kupitia uchambuzi wa mfumo wa malipo ya fedha za kujikimu kwa walimu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Abnery Mganga, amesema kuwa katika utekelezaji wa majukumu ya kuzuia rushwa, taasisi hiyo ilifanikiwa kudhibiti kiasi hicho cha Sh milioni 85.5 na kuhakikisha kinalipwa kwa walimu waajiriwa wapya wa shule za sekondari waliokuwa na madai katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Aidha, Mganga amesema mafanikio hayo yametokana na uchambuzi wa mfumo uliofanywa na taasisi hiyo pamoja na halmashauri kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa katika kikao kazi kati ya TAKUKURU na wadau wa halmashauri. Hatua hiyo imewawezesha walimu 77 waliokuwa na madai kulipwa stahiki zao.

CCM: MAKAMPUNI YASIYOLIPA WAKULIMA YAPIGWE ‘STOP’

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka Bodi ya Tumbaku (TTB) nchini kuchukua hatua mara moja dhidi ya Makampuni yote yanayonunua zao la tumbaku na kushindwa kulipa wakulima kwa wakati, na kushauri wapigwe stop. Ushauri huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Komredi Saidi Nkumba alipokuwa akitoa salamu za chama katika Mkutano Mkuu wa 33 wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Tumbaku (WETCU) Mkoani Tabora. Amesema kuwa haingiii akilini kuona mkulima akihangaika kuandaa shamba lake mwaka mzima tena kwa gharama kubwa ili kuhakikisha anapata tumbaku nzuri inayokidhi viwango vya soko la ndani na nje lakini anapouza halipwi kwa wakati. ‘Chama Cha Mapinduzi hakifurahishwi na hali hii, Wanunuzi wote wanaokuja kununua mazao ya wakulima wanatambulika kisheria na wanapewa leseni, kama hawafanyi kile kinachotakiwa kuna haja gani ya kuwabembeleza’, ameeleza. Komredi Nkumba ameitaka Bodi ya Tumbaku kusimamia ipasavyo zao hilo ili mkulima anufaike na jasho...

SONGORO MARINE UBORA WA KIMATAIFA UJENZI MELI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  KAMPUNI ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania inatajwa ni kampuni inayojenga meli kwa viwango vya kimataifa. Kampuni hiyo, imekuwa ikipewa zabuni na serikali za ujenzi wa vivuko, kutokana na kuonyesha uzalendo katika kutekeleza miradi kwa viwango vya kimataifa. Kwa miaka zaidi ya 30 Tangu kuanza kwa kampuni hii ya kizalendo imeonyesha dira kwa kampuni za kizawa baada ya kuaminiwa na serikali katika ujenzi wa vivuko. Kampuni hii iliyoanza kazi mwaka 1993 kwa sasa imeendeleza mizizi ya ujenzi wa meli za kisasa zinazotumiwa ziwani na baharini kwa kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania. Inaelezwa kuanza kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania ni hatua iliyotokana na kazi iliyotukuka kwa kujenga meli na vivuko vya umma na binafsi kwa viwango vya kimataifa. Serikali ya Tanzania mara kwa mara imekuwa ikitangaza zabuni za ujenzi wa meli, ambapo kampuni hii ya kizalendo imekuwa ikiibuka kidedea. Songoro...

KAMPUNI YA SONGORO MARINE YAKABIDHI KIVUKO UGANDA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Uganda.  KAMPUNI ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa kivuko kikubwa kitakachokuwa na uwezo wa kubeba abiria 310. Kampuni hiyo imekamilisha ujenzi wa kivuko hicho kitakachokuwa kinafanya safari zake kati ya Bukungu - Kagwara - Kaberamaido nchini Uganda. Songoro marine ambayo imejikita na ujenzi wa vivuko, imeendelea kuaminiwa na serikali ya uganda katika ujenzi wa vivuko kadhaa nchini humo. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Meja Songoro akizungumza wakati wa kukabidhi kivuko hicho, amesema ujenzi wa kivuko hicho ulianza februari 2020 na kukabidhiwa Februari 20 mwaka huu.  Kampuni ya Songoro Marine, ilisaini  mkataba wa ujenzi wa vivuko viwili pamoja na mashine ya kuondoa uchafu ziwani (dredger) kwa fedha za Uganda shilingi, 41,974,226,085. Baada ya siku ya jana kampuni hiyo kukabidhi kivuko hicho kwa serikali ya Uganda, inaendelea na kivuko kingine kimoja ambacho kitakabi...

BINTI MCHOMA MAHINDI TABORA AWEZESHWA MTAJI WA LAKI 3

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka ameleta neema kwa kijana muuza mahindi ya kuchoma Hadija Seif (26) mkazi wa Kata ya Ng’ambo, Manispaa ya Tabora baada ya kumwezesha mtaji wa shilingi laki 3. Waziri amemwezesha mtaji huo leo alipokuwa akifungua Jukwaa la Vijana wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati vilivyopo Mkoani Tabora, katika ukumbi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Mjini hapa. Ameeleza kuwa jana akiwa katika pita pita yake mitaani baada ya kuwasili Mjini Tabora alimwona dada mmoja akichoma mahindi na alipomuuliza mradi huo unamsaidiaje akasema kuwa unampatia kipato kidogo cha kutunza watoto wake. Na alipomuuliza ndoto yake ni nini, akaeleza kuwa anatamani kuwa na biashara ya kuuza vyombo vya nyumbani na kuuza samaki wa kukaanga, ila mtaji hana na alipoulizwa anatamani kuwa na mtaji wa kiasi gani akasema laki 3. ‘Sikujitambulisha kuwa mimi ni Waziri ila nilimwambia aje ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kuna mkutano wa vijana, ...