Machapisho

POLISI YAWASAKA WANAWAKE WALIOMSHAMBULIA MWENZAO KWA MWIKO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  JESHI la Polisi nchini Tanzania limesema limeanza kufanya uchunguzi kuhusiana na picha mjengeo inayosambazwa kupitia mitandao ya kijamii wakionekana wanawake wawili wakimpiga mwanamke mmoja kwa kutumia mwiko na kumshambulia kwa maneno kwa madai ya kudhalilishwa na mhanga wa tukio hilo kupitia mtandao Facebook. Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumatatu Februari 09, 2026 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, (DCP) David Misime imeeleza kuwa katika Picha hiyo mjongeo, wanawake hao wamesikika wakihoji sababu za mmoja wao kudhalilishwa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa amekuwa akiiba mabwana (Waume) za watu.  Jeshi la Polisi kupitia taarifa yake hiyo limetoa wito kwa yeyote anayewafahamu wanawake hao kuwasilisha taarifa zao kwa njia anayoona inafaa na rahisi kwake ili kuweza kuwafikia na kuwakamata ili kuwachukulia hatua za kisheria.

DHAMIRA YA RAIS SAMIA NI KUHAKIKISHA HUDUMA BORA ZA AFYA KWA WANANCHI

Picha
Na WAF-Dar es Salaam Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuhakikisha tabasamu la Watanzania linaendelea kuonekana kwa kuboresha huduma za afya nchini. Dkt. Samizi amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya anayeshughulikia Dawa na Vifaa Tiba, Bw. Emmanuel Tayari, aliporipoti katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Afya. Amesema kuongezwa kwa Bw. Tayari katika timu ya uongozi wa Wizara kutaongeza nguvu na uimara katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara, hususan katika kuhakikisha huduma bora za afya, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba unaimarika, na hivyo kuweka tabasamu kwa wananchi. “Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imelenga kuona Watanzania wanapata huduma bora za afya, jambo litakalowezesha tabasamu la wananchi kuonekana na kudumu, sambamba na kutekeleza azma ya Serikali na Dira ya Taifa ya Maendel...

JAMII YAHIMIZWA KUACHA UNYANYAPAA KWA WATU WANAOISHI NA KIFAFA

Picha
  Na WAF-Dar es Salaam  NAIBU Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi (Mb), ametoa wito kwa Watanzania kuacha unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kifafa na kuchukua hatua madhubuti za kuboresha upatikanaji wa huduma bora za matibabu kuanzia ngazi ya msingi. Dkt. Samizi ametoa wito huo leo Februari 9, 2026 jijini Dar es Salaam wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Kifafa Duniani pamoja na Mkutano wa Kifafa Nchini ulioandaliwa na Chama cha Kifafa Tanzania (TEA), uliofanyika katika Ukumbi wa Ummy Mwalimu, Hospitali ya Taifa Muhimbili. Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Naibu Waziri amesema ugonjwa wa kifafa bado umezungukwa na imani potofu katika jamii nyingi, hali inayosababisha wagonjwa wengi kuchelewa kupata matibabu sahihi na kukumbana na changamoto za kijamii, kisaikolojia na kiuchumi. “Katika baadhi ya jamii, kifafa huaminika kuwa ni ugonjwa unaoambukiza au unaosababishwa na uchawi, jambo linalopelekea wagonjwa kunyanya...

NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA WIZARA YA FEDHA, BW. NSUBILIN JOSHUA ALAKIWA OFISI NDOGO ZA WIZARA YA FEDHA DAR ES SALAAM

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, atakayekuwa anashughulikia masuala ya Utawala (Huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua, akipokelewa na Viongozi na baadhi ya Watumishi wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushika wadhifa huo. Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya kuwasili, Bw. Joshua alilakiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Naibu Waziri anaye simamia Sera za Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya, na baadae kukaribishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ambaye alifanya kikao kifupi na Naibu Katibu Mkuu mpya, pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam. Bw. Nsubuli Joshua, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu-Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Omolo, ambaye aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Su...

RAIS SAMIA APELEKA TABASAMU SIKONGE

Picha
  Na Allan Kitwe, Sikonge.  RAIS wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amepeleka tabasamu kwa wakazi wa Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora baada ya maji safi na salama kutoka Ziwa Viktoria kufika Wilayani humo. Shangwe na furaha za wananchi zimelipuka kwenye hafla ya kufungulia maji hayo iliyofanyika juzi katika Kata ya Misheni Mjini Sikonge kwenye eneo lilipojengwa tanki kubwa la kupokelea maji hayo ili yaanze kusambazwa kwa wananchi. Akizungumza na mamia ya wananchi, wadau wa maendeleo na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kwenye hafla hiyo, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ameeleza kufurahishwa na kazi nzuri ya utekelezaji mradi huo. Amesema kuwa mradi huo ambao unatekelezwa na Mkandarasi kutoka China kwa gharama ya shilingi bilioni 143 umelenga kufikisha huduma ya maji safi na salama katika Wilaya tatu za Urambo, Kaliua na Sikonge yenyewe. ‘Ndugu zangu wana Sikonge, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameleta tabasamu kwenu, alipoingi...

JIMMY LAI AFUNGWA MIAKA 20 JELA KWA KUUNGA DEMOKRASIA.

Picha
  Hong Kong - China. MAHAKAMA ya Hong Kong imemhukumu bilionea anayefahamika kwa kuunga mkono demokrasia, Jimmy Lai, kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya ukiukaji wa usalama wa taifa mwezi Desemba. Hukumu hiyo ndiyo kali zaidi kuwahi kutolewa chini ya sheria tata ya usalama wa taifa, ambayo China inadai ni muhimu kwa uthabiti wa jiji hilo. Lai, mwenye pasipoti ya Uingereza, alikuwa miongoni mwa wakosoaji wakubwa wa Beijing, akitumia mara kwa mara gazeti lake la kidemokrasia Apple Daily kama chombo cha kupinga utawala huo. Wakuu sita wa zamani wa gazeti hilo pia wamehukumiwa kifungo cha jela siku ya Jumatatu, kati ya miaka sita na miezi tisa hadi miaka 10. Kwa wanaharakati wa demokrasia, Lai anaonekana kama shujaa, lakini kwa Beijing anachukuliwa kuwa msaliti. Amekuwa akikanusha mashtaka yote dhidi yake, akisema alitetea kile alichoamini kuwa ni maadili ya Hong Kong, ikiwemo utawala wa sheria na uhuru wa kujieleza. Hukumu hiyo ina maana kuwa huenda aka...

WAZIRI AWESO APELEKA NEEMA URAMBO

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora. WAKAZI wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora wamelipuka kwa shangwe na furaha baada ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuagiza maji ya ziwa Victoria yafikishwe katika Wilaya hiyo ndani ya wiki tatu kuanzia sasa. Waziri ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na mamia ya wakazi wa Wilaya hiyo katika Kata ya Muungano baada ya kutembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika Wilaya tatu za Mkoa huo. Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 143 ili kuleta maji ya uhakika ya ziwa Viktoria katika Wilaya za Kaliua, Urambo na Sikonge ambazo zinashida kubwa ya maji. ‘Mradi huu utekelezaji wake unaenda vizuri sana, ujenzi wa tanki kubwa la kupokelea maji tayari umekamilika, na nimeambiwa kuwa kipande kilichobakia hakizidi hata kilometa moja maji yatakuwa yamefika hapa Urambo’, ameeleza. ‘Nitawaongezea shilingi milioni 500 za mabomba ili kazi hii ifanyike ha...

WAANDISHI KUCHUNGUZA SHOROBA NA MABADILIKO TABIA NCHI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arusha. Waandishi wa habari kanda ya kaskazini na kati, wamekubaliana kuandika uchunguzi wa uvamizi njia za wanyamapori (Shoroba) na athari za mabadiliko tabia nchi nchini. Mapito mengi ya wanyama nchini ikiwepo ya Kwakuchinja yaliyopo katikati ya  hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Manyara yanaendelea kuvamiwa na watu ajili ya shughuli za kibiaadamu na kuathiri wanyamapori kuhama na biolojia yao. Mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na uharibifu wa mazingira yameanza kusababisha kumezwa ardhi maeneo kadhaa ikiwepo eneo la pangaji mkoani Tanga na ukame maeneo mengi nchini ikiwepo ya jamii za asili na kupungua barafu mlima Kilimanjaro . Maamuzi ya kufanya uchunguzi hao yalifikiwa  katika mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira yaliyoandaliwa na mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu(THRDC) kwa kushirikiana na Taasisi ya waandishi wa habari ya kusaidia jamii za asili (MAIPAC) kwa udhamini wa shirika la Umoja wa Mataifa la UNESCO. Akizungumza katik...

WADAU WA BIASHARA WAELIMISHWA NAMNA YA KUPATA HAKI KUPITIA BARAZA LA USHINDANI

Picha
Na.Mwandishi Wetu- Mwanza. BARAZA  la Ushindani wa Soko (FCT)  limetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara jijini Mwanza, yakilenga kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya ushindani wa soko pamoja na taratibu za kupata haki katika shughuli za kibiashara. Mafunzo hayo yaliwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya biashara, ambapo waliipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa juhudi zake za kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji kupitia uwepo wa chombo huru cha kusimamia na kudhibiti ushindani wa soko. Akifungua semina hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Balandya Elikana, alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa wadau wa sekta ya biashara kwani yanawawezesha kuelewa kwa kina majukumu ya Baraza la Ushindani pamoja na umuhimu wa mshikamano katika utekelezaji wa sheria za ushindani. “Kupitia semina hii, wadau watapata uelewa mpana kuhusu Bara...