NAIBU KATIBU MKUU MPYA WA WIZARA YA FEDHA, BW. NSUBILIN JOSHUA ALAKIWA OFISI NDOGO ZA WIZARA YA FEDHA DAR ES SALAAM
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, atakayekuwa anashughulikia masuala ya Utawala (Huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua, akipokelewa na Viongozi na baadhi ya Watumishi wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushika wadhifa huo. Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasili, Bw. Joshua alilakiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Naibu Waziri anaye simamia Sera za Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya, na baadae kukaribishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ambaye alifanya kikao kifupi na Naibu Katibu Mkuu mpya, pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Bw. Nsubuli Joshua, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu-Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Omolo, ambaye aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mpya ya Vijana.









Maoni