WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAPO TAYARI KWA MFUMO WA IDRAS
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. WAFANYABIASHARA wameukubali mfumo wa Usimamizi wa Kodi za ndani (IDRAS) ,huku wakijiandaa kuupokea Jumatatu ya tarehe 9 Februari mwaka huu. Akizungumza leo 6.2.2026 jijini Dar es salaam katika mafunzo ya mfumo mpya kwa wafanyabiashara wa Kariakoo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) Bw. Severin Mushi amesema wapo tayari kuanza kuutumia mfumo huo kwa ushirikiano wa karibu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Mwenyekiti huyo amesema kupitia mafunzo ambayo wamepatiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanaamini mfumo utakuwa msaada kwao na kuondoa changamoto mbalimbali ambazo zilikuwepo. Amesema mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara kwa kuwa yameondoa hofu iliyokuwepo awali na kuwapa uelewa wa pamoja kuhusu matumizi ya mfumo huo. Bw. Mushi amesema wamejiandaa kuupokea mfumo wa IDRAS, akieleza kuwa jambo lolote jipya huwa linaogopesha kwa wanaolipokea. Amebainisha kuwa mabadiliko ya kiteknolojia hayaepukiki ka...