Na Allan Kitwe, Tabora. ALIYEKUWA Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi kwa miaka 15, Munde Tambwe amezikwa jana katika makaburi ya Shehe Yahaya, Kata ya Ng’ambo Mjini Tabora na kuhitimisha safari yake hapa duniani. Msiba huo umevuta hisia za watu wengi wakiwemo vijana, akinamama, wana CCM, jamii, wabunge na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, kutokana na ushirikiano wake mzuri, ukarimu na kujitoa zaidi kwa jamii enzi za uhai wake. Akiongea kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye msiba huo, Makamu wa Rais Dkt Emanuel Nchimbi ameeleza kuwa marehemu alikuwa rafiki wa kila mtu. Ameongeza kuwa alikuwa mtu mwema kwa jamii, wanaCCM, wabunge na viongozi wenzake na katika nafasi zote azizowahi kutumikia alitanguliza maslahi ya nchi na chama chake, hakuwa na makuu. ‘Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa pole nyingi kwa wanafamilia, jamii, wabunge na wanaCCM wote kwa kuondokewa na mtu muhimu na Kada mwaminifu kwa ch...