MAKAMU WA RAIS BALOZI DKT. NCHIMBI AMWAKILISHA RAIS. DKT. SAMIA KWENYE MAZISHI YA MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA MUNDE TAMBWE.
Na Mwandishi Wetu, Tabora. MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mbunge wa Viti Maalum Mstaafu, Marehemu Munde Tambwe, yaliyofanyika Mkoani Tabora, leo tarehe 04 Februari 2026. Akitoa salamu za rambirambi katika msiba huo, Makamu wa Rais amesema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pole kufuatia msiba huo mkubwa. Amesema mchango wa Marehemu Munde Tambwe ni wa kipekee sana ndani ya Taifa pamoja na Chama Cha Mapinduzi. Makamu wa Rais amesema marehemu Munde aliweka mbele maendeleo ya nchi na Chama Cha Mapinduzi na wakati wote alikuwa rafiki wa kila mtu alijali sana uhusiano mzuri. Ameongeza kwamba kufuatia marehemu Munde kuanzisha ujenzi wa msikiti ambao utahitaji ukamilishaji, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha shilingi milioni 30 zitakaz...