Machapisho

UMIKIDO WAJITAMBULISHA KWA WAZIRI KATAMBI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. MWENYEKITI  wa Umoja wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO), Benny Majata, amefanya mazungumzo mafupi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Katika mazungumzo hayo, leo Januari 28, 2026 Majata alimweleza Waziri Katambi juu ya malengo ya UMIKIDO katika kusimamia maudhui yenye weledi, kuhamasisha maadili ya habari mtandaoni na kuimarisha ushirikiano kati ya vyombo vya habari na serikali. Waziri Katambi amepongeza hatua ya umoja huo kujitambulisha, na ameuhimiza UMIKIDO kufika ofisini kwake ili kufanya mazungumzo ya kina kuhusu masuala ya kimaadili, matumizi salama ya mitandao, pamoja na namna vyombo vya habari mtandaoni vinavyoweza kushirikiana na serikali katika kulinda usalama na maslahi ya Taifa.

RADA ZA HALI YA HEWA NI MUHIMU KATIKA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA HALI YA HEWA NCHINI.

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dodoma. MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) iliandaa warsha ya mafunzo ya Rada za Hali ya Hewa na matumizi ya taarifa zinazotokana na Rada,  tarehe 26-27 Januari 2026, Dodoma. Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiufundi katika matumizi ya teknolojia Rada, hususan katika uchambuzi, tafsiri na matumizi ya taarifa ili kuboresha utoaji wa utabiri zikiwemo tahadhari za  hali mbaya ya hewa kwa wakati na kwa usahihi zaidi.           Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa warsha hiyo alikuwa ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt. Ladislaus Chang’a alisema “Kama mnavyofahamu, kwa sasa dunia inashuhudia ongezeko kubwa la matukio ya hali mbaya ya hewa yanayotokana na  kuchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, ikiwemo mvua kubwa, mafuriko, vipindi virefu vya ukame, pamoja na matukio ya vimbunga na upepo m...

VYANZO VYA MAJI KUENDELEA KUTUNZWA KUONGEZA UHAKIKA WA HUDUMA YA MAJI.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI Wa Maji  Mhe.  Jumaa Aweso  (Mb) amewataka wakurugenzi wa bodi za maji za  mabonde nchini kuonyesha umuhimu wa taasisi hizo kwa wananchi kwa vitendo kwa kutoa huduma sahihi.  Waziri Aweso ametoa maelekezo hayo katika kikao cha Bodi za maji za mabonde nchini katika ukumbi wa Jiji la Dodoma.  Aweso ambaye ndiye mgeni rasmi katika kikao hicho amewataka viongozi wa mabonde hayo kutambulika kwa utoaji wa huduma na si kutambulika kwa sifa mbaya kwa wananchi na serikali ikiwemo utozaji wa Kodi zisizi halali.  Aidha Serikali bado inaendelea na mpango mkakati iliyojiwekea katika kujenga mabwawa ya kimkakati kuendelea kupanda miti rafiki wa maji kwa mazingira Ili kuboresha vyanzo vya maji na kutoa huduma ya uhakika kwa wananchi.  Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewataka wakurugenzi na wenyeviti wa Bodi za maji za mabonde nchini kuendelea kutunza vyanzo vya maji Ili kuwa na uhakika wa huduma...

VIWANDA NA BIASHARA WAPANDA MITI KUMUUNGA MKONO RAIS, DKT. SAMIA KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA.

Picha
Na Mwandishi Wetu,  Dodoma. MITI imekuwa muhimili muhimu katika ukuaji wa Sekta ya Viwanda na Biashara kwani kupitia miti, viwanda hupata malighafi, biashara hukua, na uchumi huimarika. Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb.), Januari 27, 2026, akiwa ameambatana na Naibu Waziri,Mhe. Dennis Londo pamoja na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Needpeace Wambuya kushiriki zoezi la kupanda miti katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma.  Zoezi hilo ni sehemu ya kusherehekea kumbukizi ya  siku ya kuzaliwa ya  Mwanamazingira namba moja hapa nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye aliazimisha siku yake 27 Januari, 1960 kwa kupanda mti wa Muembe (Mangifera indica) katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 27 Januari, 2026. Aidha, Waziri Kapinga wakati akiongea na Watumishi wa Wizara hiyo baada ya kupanda mti, Altria rai kwa watumishi wa wizara ...

HALMASHAURI YA IGUNGA YAUNGANA NA WATANZANIA KUPANDA MITI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga. MKURUGENZI  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid ameiongoza Menejimenti ya Halmashauri hiyo kupanda miti kwa lengo la kuitekeleza 27 ya kijani iliyoasisiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Selwa ameungana na viongozi hao leo,  ikiwa ni ishara ya kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia katika kumbukizi ya kazaliwa kwake. "Kipekee ninaishukuru na kuipongeza Menejimenti kujindaa na kushiriki zoezi hili baada ya masaa ya kazi kuungana na 27 ya kijani ikiwemo kumpongeza na kumtakia kila la kheri Mheshimiwa. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan," ameshukuru.  Ameeleza kuwa wamepanda miche 70 ambapo miche 50  yakivuli huku 20 ikiwa ni ya  matunda ambayo yatawafaidisha vizazi na vizazi.

IGUWASA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS, DKT. SAMIA KWA KUPANDA MITI.

Picha
  Tabora, Januari 27, 2026. Na Lubango Mleka, Igunga. KAATIKA kuunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu upandaji wa miti kama sehemu ya utunzaji wa mazingira, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Igunga (IGUWASA) imefanya zoezi la upandaji wa miti mbalimbali katika eneo la ofisi zake. Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mheshimiwa Rais, ambapo taasisi hiyo imeeleza kuwa inalenga kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. Viongozi na watumishi wa IGUWASA wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Bi. Selwa  Abdallah Hamid wameshiriki katika zoezi hilo, wakisisitiza kuwa upandaji miti ni hatua muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali za maji. IGUWASA imewahimiza wananchi kuiga mfano huo kwa kupanda ...

MMOJA AFARIKI KATIKA AJALI YA GARI SHINYANGA 12 WAJERUHIWA

Picha
DEREVA wa Lori lenye namba za usajili RAE 848  Mali ya Kampuni ya Jaja ya nchini Rwanda amepoteza maisha baada ya kugongana uso kwa uso na basi la abiria namba T 229 EEL mali ya kampuni ya Kisire lililokuwa likitokea Kahama kwenda Mwanza na kusababisha Majeruhi 12. Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea Januari 27 katika eneo la Tinde Mnadani na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Basi la Kisire aliyetaka kupita mkokoteni uliokuwa umebeba matunda na kuhama upande mwingine na kugongana uso kwa uso na lori hilo.

SERIKALI YAZINDUA MFUMO "ONGEA NA WAZIRI, MWANACHI KUPEWA SAUTI YA MOJA KWA MOJA SEKTA YA AFYA

Picha
  Na WAF, Arusha. SERIKAL imetangaza mwanzo wa enzi mpya ya uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika sekta ya afya baada ya kuzindua rasmi kwa mfumo wa kidijitali wa “Ongea na Waziri wa Afya” unaomuwezesha mwananchi kuwasiliana moja kwa moja na Wizara ya Afya saa 24 kwa siku. Hayo yamesemwa na Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa  hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Januari 26,2026 jijini Arusha. Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, amesema mfumo huo ni utekelezaji wa vitendo wa dhamira ya Serikali ya kuisogeza huduma ya afya karibu na mwananchi na kuhakikisha sauti ya wananchi inatumika kama dira ya maboresho ya huduma. “Mfumo wa "Ongea na Waziri wa Afya" unatuma ujumbe ulio wazi kuwa sauti ya mwananchi si ya pembeni, bali ndiyo msingi wa maamuzi ya Serikali katika kuboresha huduma za afya,” amesema Waziri Mchengerwa. Amefafanua kuwa uzinduzi wa mfumo huo ni mapinduzi makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa unajenga utamaduni mpya wa uongozi unaosiki...

HABARI PICHA

Picha
WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, leo Januari 26, 2026 amefanya kikao kazi na Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) chenye lengo la kujadili mikakati ya kuimarisha na kuendeleza utendaji wa wakala huo. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesm Mramba, Mwenyekiti wa Bodi ya PBPA, Dkt. Lutengano Mwakahesya, Mtendaji Mkuu wa PBPA, Bw. Erasto Simon, pamoja na Wajumbe wa Bodi na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati.

WIZARA YA MADINI YAJENGA MAABARA KUBWA YA KISASA DODOMA

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. WIZARA  ya Madini imetangaza ujenzi wa Maabara kubwa ya kisasa katika eneo la Nala, mkoani Dodoma, kwa lengo la kusaidia upimaji na utoaji wa taarifa sahihi za sampuli za madini. Maabara hiyo inatarajiwa kuwa kitovu cha utoaji wa huduma za madini kusini mwa Jangwa la Sahara. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema hayo leo Januari 26,2026 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Siku 100 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha pili cha Awamu ya Sita ya Serikali. Amesema kuwa ujenzi wa maabara hiyo utaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa Tanzania na nchi jirani, sambamba na kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani.  Aidha, Wizara imeingia makubaliano na GST ili taasisi hiyo iwe kitovu cha utoaji huduma za maabara kusini mwa Jangwa la Sahara. Katika kuongeza thamani ya madini, Waziri Mavunde amebainisha kuwa Wizara inaendelea kwa kasi na ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani, ambapo hadi sa...

SERIKALI YASAJILI ZAIDI YA WAFABIASHARA NDOGONDOGO 119,000 NCHINI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. SERIKALI kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imesajili jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 119,595 katika Mfumo wa Usimamizi na Usajili wa Wafanyabiashara Ndogondogo (WBNMIS), hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kunufaika na fursa mbalimbali za maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa wizara hiyo, Mheshimiwa Dorothy Gwajima, amesema mafanikio hayo yamepatikana katika kipindi cha siku 100 za utekelezaji wa ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo Serikali imejikita katika urasimishaji wa wafanyabiashara, utoaji wa mikopo nafuu na uwezeshaji wa makundi maalum. "Kati ya waliosajiliwa wanawake ni 73,341 na wanaume 46,254, huku makundi yaliyosajiliwa yakijumuisha machinga 103,102, mama na baba lishe 12,384 pamoja na waendesha bodaboda na bajaji 4,109," Amesema Waziri Gwajima. Ameeleza kuwa katika ...

VIKUNDI 222 UYUI VYAWEZESHWA MIKOPO NAFUU YA BILIONI 1

Picha
   Na Allan Kitwe, Tabora. HALMASHAURI ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora imetoa mikopo nafuu isiyo na riba ya shilingi bilioni 1 kwa vikundi 222 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kuwainua kiuchumi. Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi za mikopo hiyo jana, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya hiyo Amoniche Mtweve amesema kuwa mikopo hiyo imetokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri. Ameongeza kuwa jumla ya wanachama 1,121 wanaounda vikundi hivyo wamenufaika na mikopo hiyo na kuwapa nguvu ya kuendeleza miradi yao ya biashara na uzalishaji mali katika maeneo yao. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Shabani Katalambula, amewataka wanufaika kurejesha mikopo hiyo kwa wakati ili kuwezesha wananchi wengine kunufaika na mikopo hiyo katika awamu zijazo. Amefafanua lengo la mikopo hiyo kuwa ni kusaidia vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kupitia miradi midogo midogo ya ujasiriam...