Machapisho

WAZIRI MCHENGERWA AZITAKA TAASISI ZA AFYA KUJITATHMINI KUELEKEA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Picha
  Na WAF, Dodoma. WAZIRI wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amezitaka Taasisi ambazo ziko chini ya Wizara ya Afya na Vituo vyote vya kutolea huduma kujitathmini utendaji kazi wake, mapungufu na changamoto na kuona namna gani ya kutatua changamoto hizo wakati Serikali ikielekea kwenye utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote. Waziri Mchengerwa amesema hayo Januari 14, 2026 jijini Dodoma katika kikao kazi kilichohusisha Wakurugenzi Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Waganga Wakuu wa Mikoa, Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa na Watumishi wote wa Sekta ya Afya. Mhe. Mchengerwa amesema Bima ya Afya kwa Wote italeta ongezeko la matumizi ya huduma za afya hivyo amevitaka vituo vyote vya kutolea huduma za Afya kuanzia ngazi ya msingi mpaka Taifa kuimarisha huduma wanazo zitoa. “Wananchi waliokuwa wanajizuia kufika Hospitalini kwa sababu ya gharama sasa watafika. Huduma zitahitajika kwa wingi zaidi, kwa kasi zaidi, na kwa ubora unaofanana”, amesema Waziri Mchengerwa...

SERIKALI YAPONGEZWA KUHARAKISHA MAENDELEO YA WANANCHI

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imepongezwa kwa kupeleka mabilioni ya fedha za miradi ya maendeleo katika halmashari ya manispaa Tabora ili kuchochea maendeleo ya wananchi. Pongezi hizo zimetolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa hiyo Ghullan Remtullah Dewj (diwani wa Kata ya Kanyenye) alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo jana. Ameeleza kuwa mabilioni yaliyoletwa katika halmashauri hiyo yamekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya wananchi ikiwemo kuboreshwa kwa miundombinu ya utoaji huduma za kijamii. Ghullam amesema kuwa mabilioni hayo yameendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa stendi mpya ya kisasa eneo la Inala, soko jipya la kisasa na ujenzi wa km 10 za barabara za lami. 'Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuwajali wananchi wa manispaa ya Tabora na kutuletea mabilioni ya fedha ili miradi inayotekelezwa ilete tija kubwa kwa jamii,’ amee...

DKT. KIJAJI AKUTANA NA TAASISI ZA WIZARA YAKE.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 14 Januari, 2026 ameongoza kikao kazi cha kupitia taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Taasisi za Wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026 zitakazojadiliwa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.  Kikao hicho kinafanyika Mtumba Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, Managementi ya Wizara na viongozi mbalimbali wa Taasisi zilizopo chini Wizara hiyo.

KONGAMANO LA KILIMO SIMANJIRO LAFANA

Picha
Na Mwandishi wetu, Simanjiro WILAYA ya Simanjiro mkoani Manyara, imejipanga kuhakikisha inafanya mageuzi makubwa katika mazao ya kilimo na mifugo ili wakazi wa eneo hilo wapate tija zaidi na kunufaika kiuchumi. Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, mwalimu Fakii Raphael Lulandala ameeleza hayo kwenye kongamano la kilimo la mwaka 2025/2026 lililofanyika mji mdogo wa Orkesumet  Lulandala amesema Simanjiro ina maeneo makubwa ya kilimo na yenye rutuba ikiwemo ya umwagiliaji ila bado hayajatumika ipasavyo katika kulima, hivyo wahitaji wachangamkie fursa hiyo. "Simanjiro imetenga kiasi cha hekta 17,000 kwa ajili ya kilimo ila hadi sasa zinatumia hekta 630 pekee kwa kulima, tunawakaribisha wakulima waje Simanjiro kwani tumejipanga kisawasawa maeneo ya kilimo yapo," amesema DC Lulandala. Mkuu huyo wa wilaya ametaja baadhi ya mazao yanayostawi kwenye eneo hilo ni pamoja na mahindi, maharage, vitunguu, mpunga na ufuta. Hata hivyo, amewaagiza maofisa ugani kuhakikisha wanahamia mashambani kwa le...

URAMBO WAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI

Picha
Na Allan Kitwe, Urambo. HALMASHAURI ya Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora imefungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali, kwa kuanzia wametenga eneo la ardhi lenye ukubwa wa hekari 72 kwa ajili ya kazi hiyo. Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Grace Quintine alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya halmashauri katika kikao cha baraza la madiwani. Amesema kuwa halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri zenye mazingira bora ya uwekezaji na ardhi nzuri inayofaa kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara. Amedokeza kuwa maboresho makubwa ya miundombinu ya huduma za kijamii ambayo yameendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kivutio muhimu kwa wawekezaji. Guintine amefafanua kuwa Urambo ni mahali salama kwa uwekezaji na kwa  mwaka huu wa fedha wameratibu maeneo maalumu yanayofaa kwa uwekezaji na kutenga eneo lenye ukubwa w...

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUZINGATIA KINGA NA TAHADHARI YA MAJANGA YA MOTO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Morogoro. WATUMISHI wa umma wametakiwa kutumia kikamilifu maarifa wanayoyapata katika kusimamia na kutekeleza kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto katika majengo na miradi yote ya serikali Wito huo umetolewa na  Dkt. James Henry Kilabuko akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Wenye Ulemavu) wakati wa semina ya usimamizi wa kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto iliyowakutanisha Wakurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Taasisi za umma  Amesema changamoto ya ukosefu wa fedha kwa ajili ya ununuzi na ukarabati wa miundombinu ya kujikinga dhidi ya moto haipaswi kuwa kikwazo kwa watumishi wa umma kusubiri bila kuchukua hatua, bali watumie ipasavyo fursa na rasilimali zilizopo kujilinda wao wenyewe pamoja na kulinda mali za serikali. Ameongeza kuwa maandalizi, tahadhari na ufuatiliaji wa mara kwa mara ni nguzo muhimu katika kupunguza athari zinazotokana na majanga ya moto, akisisitiza ku...

SHULE ZOTE 18055 ZA MSINGI ZIPO TAYARI KUPOKEA WANAFUNZI- PROF. SHEMDOE

Picha
  Na OWM - TAMISEMI  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe ameridhishwa na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza katika Shule ya Msingi Iyumbu jijini Dodoma, na kuuarifu umma kuwa maandalizi katika shule zote za msingi 18055 yamekamilika na zipo tayari kupokea wanafunzi kuanzia Januari 13, 2026. Prof. Shemdoe amesema, ameitembelea shule hiyo ya Msingi Iyumbu leo Januari 12, 2026, ili kujiridhisha na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wanaotarajiwa kuanza darasa la awali na la kwanza Januari 13, 2026 na amejionea mwenyewe kuwa maandalizi yamekamilika. “Tumeona maandalizi kwenye shule hii yamekamilika, kama ilivyo kwenye shule zote 18055 za msingi, hivyo natoa wito kwa wazazi wenye watoto walio na umri wa kuanza darasa la awali na la kwanza wawapeleke shuleni,” Prof. Shemdoe amesisitiza. Prof. Shemdoe amejionea madarasa ya awali mazuri ambayo yamejengwa kwa fedha za mapa...

SELWA AKAGUA MIRADI 19 YA ELIMU IGUNGA YENYE THAMANI YA BILIONI 3.39.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga. MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi 19 ya Afya na Elimu yenye tahamani ya sh. 3.39 bilioni. Selwa amefanya ziara hiyo ya siku tatu mfululizo katika kata zilizopo kwenye majimbo ya Igunga na Manonga wilayani Igunga. Amesema kukamilika kwa miradi hiyo ni muendelezo wa kuendelea kutoa huduma na furaha kwa wananchi.

SERIKALI YAONYA WATAALAMU WA ARDHI WASIO WAADILIFU

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuhakikisha migogoro ya ardhi iliyopo katika maeneo yao inatatuliwa kwa wakati ili kuepusha malalamiko ya wananchi. Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kaspar Kaspar Mmuya alipokuwa akiongea na watumishi wa sekta hiyo kutoka taasisi mbalimbali za umma Mkoani hapa. Ameeleza kuwa ni jukumu la wataalamu wa sekta hii kuhakikisha kero na migogoro yoyote inayohusiana na masuala ya ardhi inashughulikiwa ipasavyo na kwa wakati ili wananchi wapate haki zao. ‘Ninyi ni wawakilishi wa Mheshimiwa Rais katika sekta hii, onyesheni weledi wenu, fanyeni kazi kwa uadilifu mkubwa, kuweni na maadili mema, tendeni haki kwa wananchi wote ili wawaamini, wengi wenu mnaitwa wapiga dili’, amesema. Ameonya kuwa serikali haitamvumilia mtumishi yeyote wa sekta hii anayeendekeza vitendo vya upigaji dili badala ya kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia she...

IGEMBENSABO INAWATAKIA WANACHAMA WAKE WOTE HERI YA MIAKA 62 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Picha
 

WALIMU SIMANJIRO WAJENGEWA UWEZO SIS

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro WAKUU wa shule za sekondari na msingi wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamejengewa uwezo wa kuandaa taarifa za shule kutokana na kasi ya ukuaji na kuongezeka kwa matumizi ya sayansi na teknolojia ulimwenguni. Wakuu wa shule 23 za sekondari, 110 wa msingi wa shule za serikali na binafsi wamejengewa uwezo wa kuandaa taarifa za shule ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa wake kupitia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Elimu.  Afisa elimu ya awali na msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Darius Daudi Limandola amesema walimu hao wamepata mafunzo hayo ya uandaaji wa taarifa za shule kwenye vituo vitatu vya Orkesumet, Terrat na Mirerani. Limandola ameeleza kwamba mafunzo hayo ya mfumo wa utoaji wa taarifa za kielimu kupitia mfumo wa kidigitali (School Information System) una lengo la kurahisisha utoaji na upatikanaji wa taarifa za shule husika kwa wakati. Ameeleza kwamba mfumo huo unafanyak...