SERIKALI YAPONGEZWA KUHARAKISHA MAENDELEO YA WANANCHI

 


Na Allan Kitwe, Tabora

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imepongezwa kwa kupeleka mabilioni ya fedha za miradi ya maendeleo katika halmashari ya manispaa Tabora ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa hiyo Ghullan Remtullah Dewj (diwani wa Kata ya Kanyenye) alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo jana.

Ameeleza kuwa mabilioni yaliyoletwa katika halmashauri hiyo yamekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya wananchi ikiwemo kuboreshwa kwa miundombinu ya utoaji huduma za kijamii.

Ghullam amesema kuwa mabilioni hayo yameendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa stendi mpya ya kisasa eneo la Inala, soko jipya la kisasa na ujenzi wa km 10 za barabara za lami.

'Tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuwajali wananchi wa manispaa ya Tabora na kutuletea mabilioni ya fedha ili miradi inayotekelezwa ilete tija kubwa kwa jamii,’ ameeleza.

Amesisistiza kuwa kila diwani aliyechaguliwa mwaka huu yupo tayari kuwatumikia wapiga kura wake na kubainisha kuwa mwaka huu wamekuja kivingine, kila mmoja anataka matokeo chanya katika kata yake.

Ameomba Watendaji na Wataalamu wote wa halmashauri hiyo kuwapa ushirikiano wa kutosha waheshimiwa madiwani ili kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa na serikali katika kata zao inaleta matokeo chanya.

Aidha amemwagiza Mkurugenzi kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na miradi viporo itengewe bajeti kupitia mapato ya ndani ili utekelezaji wake uendelee ili kunufaishawananchi.

Naye Naibu Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo Hadija Nassoro Bunduki aliwashukuru madiwani wenzake kwa kumwamini na kumpa kura zote za ndiyo ili amsaidie Mstahiki Meya kufanikisha utekelezaji majukumu yake. 




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.