Machapisho

JAFO: MAONO YA RAIS SAMIA NI NGUZO YA MAENDELEO YA TAIFA

Picha
  Na Alex Sona, Kisarawe. MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, amewaomba wananchi wa Kisarawe na watanzania kwa ujumla kumuombea Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ana maono makubwa ya kuwatumikia Watanzania na kulisukuma Taifa mbele kimaendeleo. Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe, kilicholenga kuwashukuru wajumbe kwa mchango wao katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo. “Niwaombe wajumbe wa Halmashauri Kuu kuhakikisha tunamuombea Rais Dkt. Samia kwa kuwa ana kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo Watanzania na kuhakikisha Taifa letu linaendelea kusonga mbele,” amesema Dkt.Jafo. Ameongeza kuwa amani na usalama ni nguzo muhimu za maendeleo ya kiuchumi, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kumuombea Rais na Taifa kwa ujumla. “Bila amani na usalama, nchi yetu haiwezi kupata...

HABARI PICHA

Picha
Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia mada juu ya Haki za Binadamu na Misingi ya Utawala Bora zinazotolewa wakati wa mafunzo ya Sekretarieti ya Kusimamia Maadili na Kushughulikia Mrejesho ya Makao Makuu ya Polisi yanayofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Disemba 17, 2025.

DKT SEIF- TUREJESHE TABASAMU KWA WANANCHI KWA KUTOA HUDUMA BORA

Picha
Na Lubango Mleka, Mwanza. VIONGOZI katika ngazi zote wametakiwa kuhakikisha wanarejesha tabasamu kwa watanzania kwa kuwapeleka huduma bora ikiwa ni sambamba na kusimamia na kutunza miundombinu iliyopo ili iweze kuleta tija na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Jafar Seif (MB) tarehe 16 Desemba, 2025 na) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Manispaa ya Ilemela ambapo lengo kuu la ziara ni  kutembelea miradi ya afya pamoja na kukutana na watumishi kwa ajili ya kujadili na kubaini changamoto zinazoikablili sekta hiyo katika utoaji wa huduma kwa wananchi. “Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunamsaidia Mhe. Rais kurudisha tabasamu kwa watanzania, ahadi ambayo aliitoa wakati akilihutubia bunge la 13 ambapo aliahidi kwamba ndani ya awamu ya sita kipindi cha pili tuhakikishe tunarejesha tabasamu kwa watanzania kw...

TASAC YAKUSANYA MAONI YA MAREKEBISHO YA NAULI ZA MV. BIJLEE NA MV. NYEHUNGE

Picha
  Na Lubango Mleka, Mwanza. SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 16 Desemba 2025 limefanya mkutano wa wadau jijini Mwanza kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu maombi ya marekebisho ya nauli za meli za MV. Bijlee na MV. Nyehunge, zinazofanya safari kati ya Mwanza na Nansio- Ukerewe katika Ziwa Victoria. Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Dominic ulifunguliwa rasmi na Bw. Nahson Sigalla, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, waendeshaji wa meli, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa majini jijini Mwanza.  Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bw. Sigalla amesema kuwa maombi ya marekebisho ya nauli yamewasilishwa na Kampuni ya Manoj V. Mehta Investments Ltd., waendeshaji wa MV. Bijlee, na Said Mohamed & Brothers Co. Ltd., waendeshaji wa MV. Nyehunge. Alieleza kuwa kikao hicho kimeandaliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415, kinachotaka ushirikishwaji wa wadau ...

TANTRADE YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UBUNIFU SEKTA YA UMMA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki na kushinda tuzo ya Ubora katika Uhamasishaji Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Uchumi. Tuzo hizo za sekta ya Umma zinaangazia ubunifu unaofanywa na taasisi mbalimbali za umma kwa muktadha wa kutoa huduma bora zinazoakisi maendeleo endelevu ya uchumi wa Tanzania.  TanTrade imekua ikifanikisha hayo kupitia Maonesho ya Sabasaba, kuratibu Maonesho mbalimbali ya Kimataifa kama vile Expo's, Mifumo mbalimbali ya Kidigitali ya Biashara kama vile Trade Portal, Biashara App, nk. Hafla ya tuzo hizo zimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MENEJIMENTI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Picha
  Na Mwandishi Wetu. KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO), Dkt. Ladislaus Chang'a amefungua  mafunzo ya usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yanayoendeshwa na Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA),  ambapo mafunzo hayo yamejikita zaidi  katika usimamizi wa miradi ya uwekezaji wa miundombinu kama “Capital Expenditure (CapEx)”.  Dkt. Chang'a katika ufunguzi alisema kuwa TMA ikiwa ni Taasisi ya Serikali  iliyopewa majukumu ya kutoa huduma za hali ya hewa, kuratibu na kudhibiti shughuli zote zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa nchini, Mamlaka inashiriki pia kutekeleza miradi mbalimbali yenye malengo yanayochangia kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TMA ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Aidha, alieleza kuwa miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa na TMA ni ikiwemo miradi ya uwekezaji wa miundombinu mbali...

SERIKALI, WHO ZAJIIMARISHA KUKABILI DHARURA ZA AFYA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha jitihada za pamoja kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta pamoja na wadau mbalimbali, ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO), katika kukabiliana na dharura za kiafya. Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 16 Oktoba, 2025 Jijini Dodoma, na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Timu za Matibabu ya Dharura (Emergency Medical Teams – EMTs). “WHO wamekuwa wadau wakubwa katika kukabiliana na dharura na tumepiga hatua kubwa sana. Tuna sababu ya kuweka nguvu ya pamoja kuendelea kukabiliana na dharura, hususan kutokana na mabadiliko ya tabianchi, milipuko ya magonjwa na ajali,” amesema Dkt. Magembe. Aidha, Dkt. Magembe amesema kuwa uwepo wa Dawati la Afya Moja umechangia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uratibu na ufanisi wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. “Wenzetu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa. ...