Machapisho

DKT SEIF- TUREJESHE TABASAMU KWA WANANCHI KWA KUTOA HUDUMA BORA

Picha
Na Lubango Mleka, Mwanza. VIONGOZI katika ngazi zote wametakiwa kuhakikisha wanarejesha tabasamu kwa watanzania kwa kuwapeleka huduma bora ikiwa ni sambamba na kusimamia na kutunza miundombinu iliyopo ili iweze kuleta tija na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi. Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Jafar Seif (MB) tarehe 16 Desemba, 2025 na) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Manispaa ya Ilemela ambapo lengo kuu la ziara ni  kutembelea miradi ya afya pamoja na kukutana na watumishi kwa ajili ya kujadili na kubaini changamoto zinazoikablili sekta hiyo katika utoaji wa huduma kwa wananchi. “Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunamsaidia Mhe. Rais kurudisha tabasamu kwa watanzania, ahadi ambayo aliitoa wakati akilihutubia bunge la 13 ambapo aliahidi kwamba ndani ya awamu ya sita kipindi cha pili tuhakikishe tunarejesha tabasamu kwa watanzania kw...

TASAC YAKUSANYA MAONI YA MAREKEBISHO YA NAULI ZA MV. BIJLEE NA MV. NYEHUNGE

Picha
  Na Lubango Mleka, Mwanza. SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), leo tarehe 16 Desemba 2025 limefanya mkutano wa wadau jijini Mwanza kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu maombi ya marekebisho ya nauli za meli za MV. Bijlee na MV. Nyehunge, zinazofanya safari kati ya Mwanza na Nansio- Ukerewe katika Ziwa Victoria. Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Dominic ulifunguliwa rasmi na Bw. Nahson Sigalla, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, waendeshaji wa meli, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri wa majini jijini Mwanza.  Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bw. Sigalla amesema kuwa maombi ya marekebisho ya nauli yamewasilishwa na Kampuni ya Manoj V. Mehta Investments Ltd., waendeshaji wa MV. Bijlee, na Said Mohamed & Brothers Co. Ltd., waendeshaji wa MV. Nyehunge. Alieleza kuwa kikao hicho kimeandaliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415, kinachotaka ushirikishwaji wa wadau ...

TANTRADE YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UBUNIFU SEKTA YA UMMA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. MAMLAKA ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeshiriki na kushinda tuzo ya Ubora katika Uhamasishaji Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Uchumi. Tuzo hizo za sekta ya Umma zinaangazia ubunifu unaofanywa na taasisi mbalimbali za umma kwa muktadha wa kutoa huduma bora zinazoakisi maendeleo endelevu ya uchumi wa Tanzania.  TanTrade imekua ikifanikisha hayo kupitia Maonesho ya Sabasaba, kuratibu Maonesho mbalimbali ya Kimataifa kama vile Expo's, Mifumo mbalimbali ya Kidigitali ya Biashara kama vile Trade Portal, Biashara App, nk. Hafla ya tuzo hizo zimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MENEJIMENTI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Picha
  Na Mwandishi Wetu. KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO), Dkt. Ladislaus Chang'a amefungua  mafunzo ya usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa menejimenti ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yanayoendeshwa na Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA),  ambapo mafunzo hayo yamejikita zaidi  katika usimamizi wa miradi ya uwekezaji wa miundombinu kama “Capital Expenditure (CapEx)”.  Dkt. Chang'a katika ufunguzi alisema kuwa TMA ikiwa ni Taasisi ya Serikali  iliyopewa majukumu ya kutoa huduma za hali ya hewa, kuratibu na kudhibiti shughuli zote zinazohusiana na masuala ya hali ya hewa nchini, Mamlaka inashiriki pia kutekeleza miradi mbalimbali yenye malengo yanayochangia kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TMA ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Aidha, alieleza kuwa miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa na TMA ni ikiwemo miradi ya uwekezaji wa miundombinu mbali...

SERIKALI, WHO ZAJIIMARISHA KUKABILI DHARURA ZA AFYA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeendelea kuimarisha jitihada za pamoja kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta pamoja na wadau mbalimbali, ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO), katika kukabiliana na dharura za kiafya. Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 16 Oktoba, 2025 Jijini Dodoma, na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Timu za Matibabu ya Dharura (Emergency Medical Teams – EMTs). “WHO wamekuwa wadau wakubwa katika kukabiliana na dharura na tumepiga hatua kubwa sana. Tuna sababu ya kuweka nguvu ya pamoja kuendelea kukabiliana na dharura, hususan kutokana na mabadiliko ya tabianchi, milipuko ya magonjwa na ajali,” amesema Dkt. Magembe. Aidha, Dkt. Magembe amesema kuwa uwepo wa Dawati la Afya Moja umechangia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uratibu na ufanisi wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. “Wenzetu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa. ...

VYAMA 50 WANACHAMA WA SHIRECU VYAKABIDHIWA KOMPYUTA MPAKATO.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga. MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50. Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, ameipongeza SHIRECU kwa kutoa vifaa vya TEHAMAa kwa wanachama wake (AMCOS) Kompyuta hizo zimekabidhiwa leo Jumatatu Desemba 15, 2025, wakati wa mafunzo maalum ya TEHAMA na uendeshaji wa ushirika yanayofanyika katika Ukumbi wa Lyakale, Manispaa ya Shinyanga, (Desemba 15-17,2025) yakihusisha viongozi wa AMCOS kutoka katika wilaya ya Kishapu na wilaya ya Shinyanga. Kwa upande wake, Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim Kakozi, amesema ugawaji wa kompyuta umeanza na vyama 50 vilivyofanya vizuri, huku mpango ukiwa ni kufikia AMCOS zote 107 zilizopo mkoani humo ili kuhakikisha ushirika unajiendesha kwa mifumo ya kisasa ya kidijitali.

TUZO YA JAFO YA UFANISI WA JUU KWA MRADI WA MAENDELEO KUANZA KUTOLEWA KILA MWAKA KWA MWENYEKITI WA KIJIJI

Picha
Na.Alex Sonna, Kisarawe. MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ametangaza kuanza kutolewa kwa Tuzo ya Jafo ya Ufanisi wa Juu kwa Mradi wa Maendeleo, ikiwa ni mpango wa kutambua na kuhamasisha utendaji bora, ubunifu na uwajibikaji miongoni mwa Wenyeviti wa Vijiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Akizungumza na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wilayani humo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kuwashukuru kwa kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dkt. Jafo amesema tuzo hiyo (JAFO’s High Perfomance Development Project Award), inalenga kukuza ufanisi wa juu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, kuongeza uwajibikaji na kuibua ushindani chanya miongoni mwa wenyeviti hao. Amesema tuzo hiyo itatolewa kila mwaka ili kumtambua na kumzawadia Mwenyekiti au Mwakilishi wa Kijiji aliyeonesha utendaji wa hali ya juu, ubunifu na matokeo yanayopimika katika kusimamia mradi ndani ya Halmashauri hiyo. “Tuzo hii ni kwa Mwenyekiti wa Kijiji au mwakilishi wa kijiji atakayeng’ara kwa...

WACHIMBAJI LEMSHUKU WAOMBA UTAFITI WA KINA MADINI YA GREEN GARNET

Picha
Ni moja ya madini vito yenye thamani kubwa sokoni, Madini vito yenye sifa ya ugumu (Hardness) Na Mwandishi Wetu, Simanjiro – Manyara WACHIMBAJI wadogo wa madini ya Green Garnet katika eneo la Lemshuku Wilaya ya  Simanjiro mkoani Manyara,  wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini na taasisi zake kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia ili kubaini kiwango, ubora na thamani halisi ya madini hayo yanayopatikana katika maeneo wanayofanyia shughuli za uchimbaji. Hayo yamebainishwa leo Desemba 16, 2025 na Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wadogo Mkoa wa Manyara (MAREMA) eneo la Lemshuku Swalehe Abdalah  wakati akizungumza na timu ya  Madini Diary  walipotembelea eneo la uchimbaji wa madini hayo.  Swalehe ameeleza kuwa , kwa muda mrefu wamekuwa wakichimba madini hayo kwa kutumia mbinu za jadi bila msaada wa tafiti za kitaalamu, hali inayowafanya kushindwa kutambua maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini na kukosa taarifa sahihi kuhusu thamani ya madini hayo katika ...