VYAMA 50 WANACHAMA WA SHIRECU VYAKABIDHIWA KOMPYUTA MPAKATO.




Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro akikabidhi kompyuta mpakato 50 zilizotolewa na SHIRECU kwa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) 50.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, ameipongeza SHIRECU kwa kutoa vifaa vya TEHAMAa kwa wanachama wake (AMCOS)

Kompyuta hizo zimekabidhiwa leo Jumatatu Desemba 15, 2025, wakati wa mafunzo maalum ya TEHAMA na uendeshaji wa ushirika yanayofanyika katika Ukumbi wa Lyakale, Manispaa ya Shinyanga, (Desemba 15-17,2025) yakihusisha viongozi wa AMCOS kutoka katika wilaya ya Kishapu na wilaya ya Shinyanga.

Kwa upande wake, Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoa wa Shinyanga, Ibrahim Kakozi, amesema ugawaji wa kompyuta umeanza na vyama 50 vilivyofanya vizuri, huku mpango ukiwa ni kufikia AMCOS zote 107 zilizopo mkoani humo ili kuhakikisha ushirika unajiendesha kwa mifumo ya kisasa ya kidijitali.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.