ADAKWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJITEKA
Na Allan Kitwe, Tabora JESHI la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia Hadija Jimmy Mrijo (39) mpare, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na watu wasiojulikana ili ajipatie fedha isivyo halali kutoka kwa mume wake. Kamanda wa Polisi Mkoani hapa SACP Richard Abwao amethibitisha kushikiliwa mwanamke huyo ambaye ni mke wa Emanuel Peter Charles mkazi wa Tabora Mjini. Amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa mumewe kuwa alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akidai kuwa wamemteka hivyo awatumie fedha kiasi cha sh mil 2 ili wamwachie. Amedokeza kuwa mume wa mtuhumiwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kusikia mlio wa kuteswa aliingiwa na hofu na kuanza kutafuta kiasi hicho cha fedha ambapo alifanikiwa kutuma kiasi cha sh 1,385,800/-. Kamanda Abwao amefafanua kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina tumebaini kuwa mtuhumiwa hakuwa ametekwa ila alijiteka mwenyewe ili apate fedha hizo, akishirikiana na wenzake na wote wamekamatwa. Ametaja watuhumiwa wengine ...