ZAIDI YA LESENI 700 ZATOLEWA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU
Na Mwandishi Wetu, Mahenge - Morogoro. KATIKA kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mwaka 2022 hadi 2025 zimetolewa leseni 714 katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mahenge zikijumuhisha leseni za utafiti, uchimbaji na biashara ya madini kwa wadau mbalimbali wanajishughulisha na uwekezaji katika Sekta ya Madini. Hayo yalielezwa Novemba 12, 2025 na Afisa Madini Mkazi , Mkoa wa Kimadini Mahenge Jonas Mwano wakati akielezea kuhusu mafanikio yaliyopo. Mwano alisema kuwa, mafanikio hayo miaka mitatu yamepelekea kufikia lengo la ukusanyaji wa maduhuli kwa asilimia 78.7 katika wilaya ya Ulanga, Malinyi na Kilombero. Aidha katika kipindi cha mwezi Julai mpaka Oktoba 2025 Ofisi imekusanya asilimia 61 ya lengo katika kipindi husika. Akielezea kuhusu aina ya leseni zilitolewa Mwano alifafanua kuwa, katika kipindi husika kulitolewa aina mbalimbali za leseni kama leseni za utafiti 15, leseni kubwa ya uchimbaji 2, leseni ndogo ya uchimbaji 277, leseni kubwa ya...