Machapisho

ZAIDI YA WANANCHI 1,500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJIKO BANIFU WILAYANI BABATI

Picha
  Majiko banifu 1,582 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200. Na Lubango Mleka, Babati. MKUU wa Wilaya ya wa Babati, Mheshimiwa Emmanuela Kaganda, leo Novemba 12, 2025 kwa niaba ya wakazi wa wilaya ya babati amezindua mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku.   Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga akiwataka wakuu wa wilaya wote wa mkoa wa manyara kuzindua na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika wilaya zao. Uzinduzi umefanyika katika kata ya Magugu wilayani babati, ambapo jumla ya majiko banifu  1,582 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Kaganda amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipat...

BALOZI PINDI CHANA AKIPA KATIKA KATIKA KIKAO CHA PILI CHA BUNGE LA TANZANIA

Picha
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Njombe,Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana akiapa rasmi kuwa mbunge katika Mkutano wa Kwanza, Kikao cha Pili cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Novemba 12,2025.

MTINDO BORA WA MAISHA _ LISHE ASILIA.

Picha
  Maelezo ya Kikundi (Group Description): MTINDO BORA WA MAISHA LISHE ASILIA ni jukwaa la kidigitali lililoanzishwa na Mtaala Mr Roghat Falme Robert kwa ushirikiano na wataalamu wa Lishe, afya na kilimo na kwa sasa tunao mabalozi tunaowaandaa.  Kauli Mbiu “Nourish to Flourish Lisha Mwili, Kuza Maisha.” Lengo kuu ni kuhamasisha ulaji wa chakula bora, kuboresha usalama wa chakula majumbani, na kukuza tabia njema za lishe kwa watu binafsi na jamii. Tunalenga kuwawezesha watu kupata maarifa na zana zinazowawezesha kufanya maamuzi sahihi ya lishe ili kuishi maisha yenye afya na ustawi. Malengo (Objectives) Kuelimisha na kuhamasisha kuhusu ulaji bora wa chakula. Kuboresha usalama wa chakula majumbani kwa kutoa rasilimali na msaada. Kukuza tabia njema za lishe kwa watu binafsi na jamii. Kutoa jukwaa la fursa halisi za ajira katika sekta ya kilimo na afya. Kutoa nafasi za matangazo kwa biashara zinazohusiana. Dira (Vision) Dunia ambayo watu na jamii wanapata chakula chenye lishe, elim...

SENDIGA AZINDUA MRADI WA USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MAJIKO BANIFU KWA BEI YA RUZUKU MANYARA.

Picha
 *Majiko banifu 7,914 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku, Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 11,200.  Na Mwandishi Wetu, Manyara. MKUU wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, leo Novemba 10, 2025 amezindua rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoani Manyara. Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa upatikanaji na uhamasisha wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia. Aidha,uzinduzi huu umefanyika katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara iliyopo wilaya ya Babati, ambapo jumla ya majiko banifu  7,914 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya kiasi cha  TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko. Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mheshimiwa Sendiga amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu. Aidha, amewaagiza Wakuu wa Wilaya...

SERENGETI BOYS YAWASILI ADDIS ABABA

Picha
  Timu ya Taifa U17 (Serengeti Boys) imewasili Addis Ababa, Ethiopia kwenye mashindano ya kufuzu AFCON 2026 Kanda ya CECAFA. @serengetiboystz

MWENYEKITI WA KAMATI YA USALAMA BARABARANI MKOA WA TABORA AKABIDHI GARI KWA JESHI LA POLISI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tabora. Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Tabora, Bw. Hamud Nasor,  leo Novemba 10, 2025 amekabidhi  gari aina ya Toyota Probox kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao kwa ajili ya matumizi ya kikosi cha usalama barabarani.

UTPC YAOMBOLEZA VIFO VYA WANANCHI WALIOPOTEZA MAISHA SIKU YA UCHAGUZI OCTOBA, 29,2025.

Picha
 

BABA LEVO KUTUMIA MABANGO YA KAMPENI KUTENGENEZA MEZA ZA WAFANYABIASHARA KIGOMA MJINI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. MBUNGE wa Kigoma Mjini Mheshimiwa Clayton Revocatus Chipando anayejulikana kwa jina la Baba Levo ameonyesha mfano wa ubunifu na uwajibikaji kwa kutumia mabango 80000 ya kampeni yaliyosalia baada ya uchaguzi kutengeneza meza zitakazotolewa bure kwa wafanyabiashara wadogo katika masoko ya Kigoma Mjini. Akizungumza na waandishi wa habari mbunge huyo Baba Levo amesema hatua hiyo inalenga kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na kuonyesha kwamba hata vifaa vilivyotumika kisiasa vinaweza kuwa na faida kijamii endapo vitatumiwa kwa ubunifu. Amesema badala ya mabango ya kampeni kubaki yakiharibu mazingira wameamua kuyageuza kuwa meza imara kwa ajili ya wafanyabiashara wa Kigoma ni njia ya kugeuza alama za siasa kuwa alama za maendeleo. Meza hizo zitatolewa rasmi wiki ijayo katika mkutano mkubwa wa shukurani utakaofanyika Kigoma Mjini ambapo Baba Levo atawashukuru wananchi kwa imani waliyoonyesha kwake na kueleza mwelekeo wa uongozi wake mpya. "Mpango wa kutu...

HABARI PICHA KUTOKA BUNGENI

Picha
WAHESHIMIWA wabunge wakijisajili katika viwanja Vya bunge leo Novemba 8 , 2025 kabla ya kuanza kwa mkutano wa kwanza wa bunge la 13 unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumanne, Tarehe 11,2025.

UTALII TANZANIA WAZIDI KUNOGA, MAWAKALA 120 WA MAREKANI WAVUTIWA

Picha
Na Lubango Mleka, Serengeti. MAWAKALA wa utalii 120 kutoka nchini Marekani wameonyesha kuvutiwa na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Tanzania, hususani mandhari ya kuvutia, wanyamapori, na urithi wa utamaduni wa kipekee. Tukio hilo limejidhihirisha katika usiku wa Novemba 7, 2025 kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kuwakaribisha mawakala hao waliowasili nchini kwa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Excellent Guide Tours and Safaris,  Justin Alfred, amesema; "Tumevutiwa sana na mandhari ya Tanzania, hasa wanyamapori kama tembo, twiga, simba na nyati. Nchi hii ni salama, wananchi wake ni wakarimu, watalii wasisite kuja kuitembelea."  Amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha Tanzania inatambulika zaidi duniani kama kitovu cha utalii barani Afrika kutokana na urithi wake wa asili, utamaduni na vivutio vya ki...

SALOME MNYAWI MITANO TENA KWAKE MIRERANI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani  MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salome Nelson Mnyawi, amewaomba wakazi wa eneo hilo kumpa kura nyingi za ndiyo kwani amefanikisha maendeleo mengi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Salome akizungumza kwenye eneo la Maduka Matatu, Mtaa wa Twiga, Kata ya Mirerani, amesema alichaguliwa kwa mara ya kwanza kipindi kilichopita hivyo anaomba kipindi kingine cha miaka mitano ili aweze kushirikiana nao kufanikisha maendeleo ya eneo hilo. Ameeleza baadhi ya mafanikio yaliyofanyika kwenye kipindi chake ni ujenzi wa kituo cha afya Tanzanite ambapo kimekamilika na sasa kinasubiria kufunguliwa na kutoa huduma kwa jamii. "Pia miundombinu ya barabara za lami kutoka soko la getini hadi lango la kuingia na kutoka ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite pamoja na taa na barabara kutoka transifoma hadi kituo cha mafuta cha Kibobo," amesema Salome. Amesema sekta ya elim...

WAPIGA KURA 273,076 WANATARAJIA KUPIGA KURA IFIKIPO OKTOBA 29, 2025 JIMBO LA IGUNGA NA MANONGA

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga. MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Majimbo ya Igunga na Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amesema wapiga kura 273,076 wanatarajia kupiga kura ifikapo Oktoba 29, mwaka huu katika majimbo hayo. Hamisi ameeleza hayo katika ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo katika wilaya hiyo mjini Igunga. Kwa mujibu wa kifungu cha 69, (1) cha sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Hamisi amewaeleza wananchi waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa uchaguzi utafanyika siku ya Jumatano Oktoba 29 mwaka huu. Amesema vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ndio vitatumika kupiga kura huku vikifunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na kwa upande wa vituo vilivyoko Magereza kufunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa tisa alaasiri. "Nitumie fursa hii kuwaomba na9999 kuwakaribisha wananchi wote wa majimbo ya Igunga na Manonga kujitokeza...