Machapisho

WANA MOMBA WAAHIDI KUICHAGUA CCM KWA KISHINDO MBELE YA CHATANDA

Picha
  Na Hamida Ramadhani,Songwe. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 11 Oktoba 2025 katika Wilaya ya Momba, Kata ya Kamsamba, Mkoani Songwe. Ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi, Huku akiwaomba Wananchi Kukichagua Chama Cha Mapinduzi ifikapo Oktoba 29,2025. Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, amemuombea Kura za Heshima Mgombea wa Nafasi ya Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Momba, Ndg. Condester Sichalwe na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo sambamba na hilo Wananchi wa Momba wamemuahidi Chatanda kuwa Watapiga Kura za Kishindo kwa Wagombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM ili kuitimiza furaha yao kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

UTAFITI MIAMBA BONDE LA EYASI WEMBERE WATHIBITISHA UWEZEKANO WA UPATIKANAJI MAFUTA

Picha
 *Dkt Mataragio akagua shughuli za utafiti na kutoa maelekezo kwa TPDC na AGS*   *Awamu ya  pili ya utafiti kukamilika Aprili 2026.*   *Asilimia 90 ya wanaotekeleza mradi ni watanzania*  Na Mwandishi Wetu, Arusha. UTAFITI unaofanyika katika  mradi wa kimkakati wa  Eyasi Wembere unaolenga kutafuta mafuta na gesi katika bonde la ufa la Afrika  Mashariki umeonesha matumaini makubwa ya kupatikana kwa Mafuta na Gesi katika bonde hilo. Hayo yamebainika wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa  mradi huo mkoani Arusha wilaya ya Karatu.  “Kazi za utafiti wa mradi huu zimeanza mwaka 2015,  tumekuwa tukikusanya data mbalimbali zinazohusiana na uwepo wa mafuta na gesi ambapo baada ya ukusanyaji, data hizo zilitumika kubainisha miamba tabaka ambayo ina mafuta na tukajiridhisha kwamba katika eneo hili la bonde  ipo miamba ambayo inaweza ikahifadhi m...

IGUWASA YATATUA KERO YA MAJI SHULE YA MSINGI CHIPUKIZI B IGUNGA.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA) imefanikiwa kutatua tatizo sugu la maji katika Shule ya Msingi Chipukizi B iliyopo eneo la Mtaa wa Sanzura, Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora. Zaidi ya Wanafunzi 200 pamoja na Walimu na Wakazi wanaozunguka Shule hiyo  wameanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama, hatua inayotarajiwa kusaidia kudhibiti milipuko ya magonjwa na kuboresha mazingira ya kujifunzia. Wananchi waliozungumza na blogu ya Habari Kamili wakati wa zoezi la uchimbaji mtalo kwa ajili ya kulaza bomba la maji wamesema huduma hiyo ni faraja kubwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu. Maria Luhende, Rajabu Juma, Aisha Mussa, Elias Kishiwa na Paul Joseph, ni baadhi ya wakazi wa mtaa wa Sanzura waliojitokeza katika zoezi la uchimbaji wa mtalo wameipongeza IGUWASA kwa kufanikisha mradi huo. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Stoo, Phabian Lushindika, amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa na amehamasisha wananchi kushiriki katika kulinda m...

CHATANDA - HAKUNA KUPITA BILA KUPINGWA,TWENDENI TUKAPIGE KURA ZA NDIYO OCTOBA 29,2025.

Picha
Na Hamida Ramadhani, Tanganyika. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 10 Oktoba 2025, akiwa katika Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi, ametoa wito kwa wanachama wa CCM na Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya ndiyo, licha ya uwepo kwa wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa. Aidha, Chatanda ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akieleza mafanikio makubwa yaliyofanyika Chini ya uongozi madhubuti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, alimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanganyika, Moshi Selemani Kakoso, pamoja na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo.

WANAWAKE WASISITIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA.

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Tanganyika. MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), amewataka Wanawake wa Wilaya ya Tanganyika kujibu upotoshaji mitandaoni unaojaribu kuvuruga amani na mshikamano wa nchi kwa kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025. Akizungumza baada ya kuwasili wilaya Tanganyika leo tarehe 10 Oktoba 2025, ikiwa ni muendelezo wa kampeni amesema watu hao hawapaswi kujibiwa kwa maneno bali ni kwa kuipa ushindi CCM ili  kuendelea kubaki madarakani. Katika mkutano huo pia alimuombea kura za ndio mgombea  wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja, kumnadi mgombea wa ubunge  Ndg.Moshi Selemani Kakoso, na Wagombea nafasi ya Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Tanganyika.