Machapisho

MWELEKEO WA MVUA KWA TAREHE 1-10 OKTOBA, 2025

Picha
 

TDB KUWEKA VITUO VYA MAZIWA KATIKA SHULE ZOTE NCHINI IFIKPO 2026

Picha
  Na Hamida Ramadhani,  Dodoma BODI ya Maziwa Tanzania (TDB) imetangaza mpango wa kuhakikisha shule zote nchini zinakuwa na vituo vya maziwa ifikapo mwaka 2026 ikiwa ni jitihada za kuendeleza unywaji wa maziwa mashuleni na kuboresha lishe kwa watoto. Akizungumza na waandishi wa habari Goerge Msalya Msajili bodi ya Maziwa Tanzania TBD  katika ofisi za bodi kabla ya  kuelekea maadhimisho ya Siku ya Maziwa Duniani ambayo hufanyika kila jumatano ya mwezi wa tisa ambapo maadhimisho hayo mwaka huu yalifanyika  kitaifa mkoani wa Geita . Msajili huyo wa TDB amesema tayari shule 154 zinahudumiwa kwa kupewa maziwa mara tatu kwa wiki huku lengo likiwa ni kufikia shule 5000 katika kipindi kifupi kijacho. Amesema kupitia ushirikiano na Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi bodi hiyo inaendesha mpango wa kuhakikisha kila shule nchini inafikiwa na huduma ya maziwa ambapo zaidi ya shilingi bilioni 28 zinahitajika kufanikisha malengo hayo....

DKT.MWINYI : AJIRA KWA VIJANA KUWA SERA MAMA YA SERIKALI IJAYO.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Pangawe, Zanzibar. Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Sera Mama ya Serikali atakayoiongoza katika Awamu ijayo itakuwa ni ajira kwa Vijana. Akihutubia mamia ya Wanachama wa CCM na wananchi katika Uwanja wa Magirisi-Nyarugusu katika Jimbo la  Pangawe ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za Uchaguzi Mkuu, Dkt. Mwinyi amesema Serikali inalifahamu kwa undani changamoto ya ajira kwa vijana na imejipanga kulitafutia suluhisho la kudumu. Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendeleza mikakati ya kutoa ajira Serikalini, kuhamasisha ajira katika Sekta Binafsi, pamoja na kuwezesha Vijana kupata mikopo isiyo na riba kwa ajili ya kujiajiri na kuanzisha biashara zao wenyewe. Kuhusu miundombinu, Dkt. Mwinyi amesema Serikali tayari imesaini mkataba na mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara kuu na barabara za ndani katika J...

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Picha
  @taifastars_ @caf_online @ligikuu @bonwambura70 @ligikuu @taifastars_

KIKOSI CHA TAIFA STARS HIKI HAPA

Picha
Kikosi cha @taifastars_ kitakachoingia kambini kwa mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia 2026 vs Zambia.

BALOZI WA AFRIKA KUSINI UFARANSA AKUTWA AMEFARIKI NJE YA HOTELI YA HYATT REGENCY MJINI PARISI

Picha
BALOZI wa Afrika Kusini nchini Ufaransa, Nkosinathi Emmanuel Nathi Mthethwa, amekutwa amefariki nje ya hoteli ya Hyatt Regency mjini Paris.  Ripoti zinasema alikuwa amekodi chumba ghorofa ya 22 na dirisha lilionekana limevunjika. Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imethibitisha kifo chake, huku uchunguzi ukiendelea. Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeeleza huenda alijiua.

WANAFUNZI SHULE YA MSINGI NDALA "A" WAPATIWA MAFUNZO YA NAMNA YA KUZIMA MOTO.

Picha
Konstebo Erick Costantine akiwafundisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndala "A" iliyopo Mkoani Shinyanga namna ya kuzima moto kwa kutumia fire blanket, elimu hiyo imetolewa Septemba 30, 2035 (Picha na Jeshi la Zimamoto)

RC KATAVI, WANANCHI JITOKEZENI KWA WINGI KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Katavi. WANANCHI wa Halmashauri tano (5) za mkoa wa Katavi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma za matibabu ya kibingwa zinazoanza kutolewa leo na Madkatari Bingwa wa Huduma za Mkoba mkoani humo. Madaktari Bingwa wa Rais Samia wanaanza kutoa huduma leo Septemba 29, hadi Oktoba 3, 2025 mkoani katavi lengo likiwa ni kutoa tiba za kibingwa karibu na wananchi kutoka Halmashauri zote tano (5) za mkoa wa Katavi.   Mkuu wa mkoa wa Katavi Bi. Mwanavua Mrindoko ametoa wito kwa wakazi wote wenye changamoto za kiafya kujitokeza kupata huduma hiyo akisema hii ni ushuhuda mwingine wa kiutu kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.  Bi. Mrindoko amezitaja faida za uwepo wa huduma za Madaktari wa Rais Dkt. Samia kuwa ni pamoja na kutoa huduma hizo karibu kabisa na jamii, kujenga uwezo kwa watoa huduma wenyeji wa halmashauri ikiwemo kupunguza gharama za kupata huduma hizo nje ya mkoa wake. Huduma zitakazotolewa ni...

ROGHAT FALME ROBERT KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA CHAKULA DUNIANI UNAOTARAJIWA FANYIKA NCHINI ITALY

Picha
C  CEO wa Shirika lisilo la Kiserikali la Akili Platform Tanzania, anatarajia kuondoka hapa nchini hivi karibuni kuelekea nchini Italy kwenye Mkutano wa chakula duniani unaotarajiwa kufantika Octoba, 10 -17, 2025.

DK.MWINYI AAHIDI UWEKEZAJI MKUBWA BWAWANI NA KUIMARISHA MJI MKONGWE

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. MGOMNEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ina mpango wa kufanya uwekezaji mkubwa katika eneo la Hoteli ya Bwawani katika awamu ijayo ya uongozi wake. Akizungumza katika mkutano wa kampeni Jimbo la Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi, leo tarehe 29 Septemba 2025, Dkt. Mwinyi alibainisha kuwa eneo hilo ni muhimu kwa uchumi na utalii wa Zanzibar, na Serikali inalenga kulibadilisha kuwa mfano bora wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya awamu ijayo pia itatekeleza mpango maalum wa kuimarisha nyumba zote za Mji Mkongwe zikiwemo nyumba za wakfu, binafsi na za Serikali ili ziendelee kudumu kwa muda mrefu, kwa kutumia fedha za ndani. Kuhusu changamoto ya magari kuingia Mji Mkongwe, amesema Serikali imekamilisha mpango wa mabasi ya umeme ili kupunguza tatizo hilo na kulinda uimara wa majengo ya kihistoria. ...

DK.MWINYI AAHIDI KUJENGA MASOKO MAPYA 5 ZANZIBAR

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. MGOMBEA wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kujenga masoko makubwa mapya matano ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira bora zaidi. Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Mwanakwerekwe leo tarehe 29, Septemba 2025 katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi, Dkt. Mwinyi alisema masoko hayo mapya yatakayojengwa katika maeneo ya Kinyasini, Mwera, Kibandamaiti, Kisauni na Kwahajitumbo yataleta suluhisho la kudumu kwa changamoto za wafanyabiashara. Ameeleza kuwa kukamilika kwa masoko hayo kutapunguza msongamano unaotokana na uhaba wa nafasi, pamoja na kupunguza kodi kubwa zinazowakabili wafanyabiashara hivi sasa. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewaomba wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kumchagua tena yeye pamoja na wagombea wa CCM katika ngazi za ubunge, uwakilishi na udiwani, ili kutimiza dhamira...

UCSAF YAKAMILISHA MINARA 734, UJENZI WAFIKIA ASILIMIA 96.83.

Picha
  UJENZI wa minara 758 ya mawasiliano unaosimamiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umefikia hatua kubwa ya mafanikio, ambapo minara 734 tayari imekamilika na inatoa huduma za mawasiliano kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya vijijini nchini. Hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 96.83, hali inayodhihirisha dhamira ya Serikali kupitia UCSAF kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za mawasiliano, hususan wale wa maeneo ya vijijini na yenye changamoto za kijiografia. Minara iliyosalia ni 24 pekee, na inatarajiwa kukamilika hivi karibuni ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika katika maeneo yote yaliyopangwa. Mradi huu ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya Serikali na kampuni za simu nchini kwa lengo la kufikisha huduma za mawasiliano vijijini, zikiwemo huduma za intaneti na simu ambazo zimekuwa changamoto katika maeneo yaliyokuwa hayana mtandao wa uhakika. Wananchi wa vijiji ambavyo minara imekamilika wameshaanza kunufaika na mawasiliano bora...

MATHIAS CANAL AONGOZA UPATIKANAJI MIL 85 UJENZI WA KANISA KIOMBOI-IRAMBA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Iramba. MWANZIRISHI na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya WAZOHURU MEDIA Ndg Mathias Canal amewaongoza Viongozi wa dini, Wadau wa maendeleo na Waumini kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania-KKKT Usharika wa St George Kiomboi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida. Katika harambee hiyo iliyofanyika jana tarehe 28 Septemba 2025 katika eneo la Ujenzi wa Kanisa Mtaa wa Lulumba, Mgeni huyo rasmi amesimamia upatikanaji wa fedha taslimu Tsh 79,407,000 ambapo ahadi ni Shilingi Milioni 4,010,000 na jumla ya fedha zote zilizopatikana ni Shilingi Milioni 85,017,000. Mgeni rasmi Ndg Mathias Canal pamoja na marafiki zake waliomuunga mkono amechangia jumla ya Tsh milioni 3,835,000 na mifuko 10 ya Saruji. Akizungumza katika harambee hiyo Mathias amesema kuwa Kanisa ni nguzo muhimu ya maisha ya kiroho, kijamii na hata kiuchumi. Kupitia kanisa waumini wanajifunza misingi ya upendo, mshikamano, uadilifu na ujenzi imara wa taifa.  "Ujenzi wa kanisa si kwa aj...

TANGAZO.

Picha
OFISI YA MKUU WA WILAYA YA IGUNGA IKISHIRIKIANA NA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA, Hospitali ya Wilaya Igunga inategemea kupokea timu ya madaktari Bingwa wa Mh.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuanzia tarehe  29/09/2025  hadi tarehe 03/10/2025. Madaktari Bingwa watakaokuwepo ni 01. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wanawake( kinamam) 02. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani (mfano kisukari,pressure nk) 03. Daktari Bingwa wa Upasuaji  04. Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinywa na meno 05. Daktari Bingwa wa watoto  06. Daktari Bingwa wa Usingizi na ganzi 07. Muuguzi mbobezi. Wananchi wote wenye uhitaji wa huduma hizo wafike Hospitali ya Wilaya Igunga. Huduma zitatolewa kwa gharama nafuu kabisa. NYOTE MNAKARIBISHWA.

TANZANIA YAENDELEZA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA ICC MEN’S T20 WORLD CUP AFRICA QUALIFIER, 2025.

Picha
  Na Mwandishi Wetu,Zimbabwe. BALOZI wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP. Suzan S. Kaganda, ameongoza maafisa wa Ubalozi kushuhudia Timu ya Taifa ya Cricket ya Tanzania katika mchezo wa mashindano ya ICC Men’s T20 World Cup Africa Qualifier 2025, uliofanyika tarehe 28 Septemba 2025, kati ya Tanzania na Uganda. Katika mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya Takashinga vilivyopo mjini Harare, Zimbabwe, Timu ya Taifa ya Cricket ya Tanzania imeibuka mshindi baada ya kuifunga timu ya Uganda kwa runs 9, hatua inayofanya timu ya Tanzania kuendelea na ushindi baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Botswana siku ya Ijumaa, tarehe 26 Septemba 2025. Ushindi huu ni mafanikio muhimu katika ICC Men’s T20 World Cup Africa Qualifier 2025. Kufuatia ushindi huo dhidi ya Uganda, timu ya Tanzania kwa sasa imefuzu kuingia hatua ya nusu fainali. Mchezo wa nusu fainali utachezwa mnamo tarehe 02 Oktoba 2025, kati ya Tanzania na Namibia kwenye uwanja uliopo mjini Harare, Zimbabwe. Ubalozi wa Tanzania unaend...

WANAFUNZI ZAIDI YA 3000 WANYWA MAZIWA KUBORESHA AFYA GEITA

Picha
  Ma Mwandishi Wetu, Geita. WANAFUNZI wapatao 3,385 wa Shule za Msingi na Sekondari mkoa wa Geita wamekunywa maziwa kwa ajili ya ustawi wa Afya Bora na Lishe. Akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Unywaji Maziwa Shuleni yaliyofanyika Septemba 24, 2025 katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Mkoani hapo, Mwakilishi wa Msajili Bodi ya Maziwa Tanzania, Bi. Deorinidei Mng’ong’o alisema maziwa yaliyotolewa ni Pakti 3964 ambayo ni sawa na lita 1004.6. Mng’ong’o alisema kabla ya Siku ya kilele kumekuwepo na Matukio kadhaa yaliyokuwa yanaendelea kama vile kutembelea wanafunzi wenye uhitaji maalumu ambapo zaidi ya wanafunzi 3,385 walinufaika kwakupata Maziwa ili kuendelea kuboresha Afya zao. Alisema idadi ya lita za maziwa zilizotolewa kuanzia Septemba 22 hadi Septemba 24 mwaka huu ni lita 1004.6. “Maziwa ni mlo kamili hivyo natoa rai kwa Wazazi, Walezi na Walimu kuhakikisha watoto wetu wanapata maziwa kwa lishe bora, Afya nzuri na ukakamavu wa akili”alisema. A...

TAARIFA KWA UMMA

Picha
Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF @taifastars_ @caf_online @ligikuu @bonwambura70 @ligikuu

KATIBU MKUU WA MADINI ATEMBELEA BANDA LA GST KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Geita. KATIBU Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, ametembelea Banda la GST katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita. Katika ziara hiyo, Mhandisi Samamba ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo. Aidha Viongozi wengine waliotembelea banda la GST ni pamoja na Dkt. Mussa Budeba Mtendaji Mkuu wa GST,  Mwenyekiti wa Tume ya Madini Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini Mhandisi Theonestina Mwasha na Dkt. Theresia Numbi.  Kupitia maonesho hayo GST Imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Madini kuhusu teknolojia  na mashine mbalimbali zinazotumika kwenye utafutaji na uchenjuaji wa madini.

MELI KUBWA MPYA YA KISASA YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  MELI ya Grande Shanghai kutoka nchini China imetia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam usiku wa tarehe 20 Septemba, 2025. Meli hiyo maalum kwa ajili ya kubeba magari, ni mpya kabisa ambayo imetengenezwa mwaka 2025 inatumia nguvu ya umeme jua (solar power) ambayo ni teknolojia rafiki kwa mazingira badala ya kutumia mafuta katika uendeshaji wake. Meli hiyo ya ghorofa 14 na urefu wa mita 220 ina uwezo wa kubeba magari 9,000 kwa  wakati mmoja. Kwa sasa meli hiyo inaendelea na ushushaji wa magari 1624 katika Bandari ya Dar es Salaam. Wakizungumza wakati wa hafla fupi ya upokeaji wa meli hiyo, kwa niaba ya menejimenti ya meli hiyo, Bw. Girolamo Carignani amesema: “huu ni mwanzo kwa meli zetu kufika katika Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania." Amesema kuwa wataendelea kufanya safari za kuja nchini Tanzania ili kuboresha biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, na kuongeza kuwa hivi karibuni itaanza safari za kwenda Japan kutokea Ch...