TDB KUWEKA VITUO VYA MAZIWA KATIKA SHULE ZOTE NCHINI IFIKPO 2026
Na Hamida Ramadhani, Dodoma BODI ya Maziwa Tanzania (TDB) imetangaza mpango wa kuhakikisha shule zote nchini zinakuwa na vituo vya maziwa ifikapo mwaka 2026 ikiwa ni jitihada za kuendeleza unywaji wa maziwa mashuleni na kuboresha lishe kwa watoto. Akizungumza na waandishi wa habari Goerge Msalya Msajili bodi ya Maziwa Tanzania TBD katika ofisi za bodi kabla ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Maziwa Duniani ambayo hufanyika kila jumatano ya mwezi wa tisa ambapo maadhimisho hayo mwaka huu yalifanyika kitaifa mkoani wa Geita . Msajili huyo wa TDB amesema tayari shule 154 zinahudumiwa kwa kupewa maziwa mara tatu kwa wiki huku lengo likiwa ni kufikia shule 5000 katika kipindi kifupi kijacho. Amesema kupitia ushirikiano na Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi bodi hiyo inaendesha mpango wa kuhakikisha kila shule nchini inafikiwa na huduma ya maziwa ambapo zaidi ya shilingi bilioni 28 zinahitajika kufanikisha malengo hayo....