DKT.MWINYI : AJIRA KWA VIJANA KUWA SERA MAMA YA SERIKALI IJAYO.
Na Mwandishi Wetu, Pangawe, Zanzibar. Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Sera Mama ya Serikali atakayoiongoza katika Awamu ijayo itakuwa ni ajira kwa Vijana. Akihutubia mamia ya Wanachama wa CCM na wananchi katika Uwanja wa Magirisi-Nyarugusu katika Jimbo la Pangawe ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za Uchaguzi Mkuu, Dkt. Mwinyi amesema Serikali inalifahamu kwa undani changamoto ya ajira kwa vijana na imejipanga kulitafutia suluhisho la kudumu. Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendeleza mikakati ya kutoa ajira Serikalini, kuhamasisha ajira katika Sekta Binafsi, pamoja na kuwezesha Vijana kupata mikopo isiyo na riba kwa ajili ya kujiajiri na kuanzisha biashara zao wenyewe. Kuhusu miundombinu, Dkt. Mwinyi amesema Serikali tayari imesaini mkataba na mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara kuu na barabara za ndani katika J...