Na Hamida Ramadhan, Dodoma CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema mafanikio ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini ni kielelezo cha dhamira yake ya kweli katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, na kwamba kinaendelea kujipanga kuimarisha huduma muhimu za kijamii katika kila sekta. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jiji la Dodoma, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, amesema pamoja na mafanikio ya miradi kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, na barabara kuu za lami, CCM ina mpango kabambe wa kuwekeza zaidi katika elimu, maji, miundombinu ya afya na kukuza vipaji vya vijana. “Huduma bora kwa wananchi ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli. Tutaendelea kupeleka umeme kwenye vijiji vilivyobaki, kuboresha miundombinu ya shule na zahanati, na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama,” amesema Mavunde. Ameeleza kuwa serikali kupitia CCM inaendelea kutekeleza programu maalum za kuibua na ...