Machapisho

MAKAMU MWENYEKITI WA ACT WAZALENDO TANZANIA BARA AKAMATWA NA POLISI

Picha
MAKAMU Mwenyekiti ACT Wazalendo   Bara, Ndugu Isihaka Mchinjita   amekamatwa na Polisi muda huu akiwa Lindi baada ya uzinduzi wa kampeni. Ukamatwaji wake ulihusisha na upigwaji wa mabomu ya machozi ili kusambaratisha watu.

RAIS MWINYI AHUDHURIA MAULID YA KITAIFA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa Kiislamu katika Maulid Makuu ya Kitaifa ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Mnazi Mmoja. Maadhimisho hayo yametimiza miaka 99 tangu kuanzishwa mwaka 1926, yakihusisha wananchi na waumini kutoka sehemu mbalimbali za Zanzibar. Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Mama Mariam Mwinyi, pamoja na viongozi wa dini.

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AZINDUA SOKO LA KISASA CHUINI ZANZIBAR

Picha
  RAIS wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua soko la kisasa la wafanyabiashara Chuini, lililopo Wilaya ya Magharibi A. Soko hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 43 na lina uwezo wa kutoa ajira kwa wananchi 4000 na kuchangia ukuaji wa uchumi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa soko hilo, Rais Mwinyi amesema malengo makuu ya serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira mazuri ya kufanya biashara, huku wakichangia maendeleo ya kiuchumi na kutengeneza fursa za ajira kwa jamii.  Ameahidi kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miradi inayoongeza tija na ustawi wa wananchi.

MRADI WA MAJIKO BANIFU WATAMBULISHWA KIGOMA

Picha
*Majiko banifu 8,424 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Kigoma *Wilaya Sita kunufaika na mradi.  *Kila Wilaya kupata majiko 1,404.  Na Mwandishi Wetu, Kigoma.  WAKAZI wa Kigoma waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia Wito huo umetolewa leo Septemba 04, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Simon Nyakoro Sirro wakati akipokea mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu unaosimamiwa na kuratibiwa  na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) . "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama katika kutunza mazingira na kuboresha Afya za wananchi" amesema Mkuu wa mkoa Mhe. Sirro, alipokuwa akipokea mradi huo. Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa, Mhandisi wa Miradi kutoka wakala wa Nishati Vijijini (REA), Raya Majallah amesema, “Mradi huu unalenga kusambaza majiko banifu ili kukuza upatikanaji wa Nishati safi na...

MRADI WA TACTIC KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA

Picha
Sekta ya uvuvi nayo yaguswa.  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  UJENZI wa Barabara ya Buhongwa-Igoma yenye urefu wa Km 14 kwa kiwango cha lami inayojengwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza inatajwa kuwa ndio mwarobaini wa changamoto ya msongamano wa magari jijini humo.  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba wakati akielezea hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Jiji la Mwanza kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji na Majiji Tanzania (TACTIC)  na manufaa yake kwa wananchi. Amesema barabara hiyo inayounganisha Kata nne ambazo ni Buhongwa, Lwanhima, Kishiri na Igoma ilikuwa na changamoto kubwa hali iliyopelekea magari yote yaliyokuwa yakitoka Buhongwa kwenda Igoma au Igoma kwenda Buhongwa kulazimika kuingia katikati ya jiji hivyo kuongeza msongamano wa magari.  Wakili Kibamba ameongeza kuwa  ujenzi wa barabara hiyo utasaidia kupunguza msongamano huo kwa kiasi kikubwa kwani magari yote yaliyokuwa yanatoka maeneo ...

HELKOPTA YAPOTEA NA WATU NANE

Picha
HELKOPTA yenye watu wanane imepotea kwenye kisiwa cha Borneo, Indonesia, na juhudi za uokoaji zimeanza, kwa mujibu wa maafisa wa uokoaji. Kiongozi wa shirika la uokoaji Banjarmasin, I Putu Sudayana, amesema helikopta hiyo ilikuwa na marubani wawili na abiria sita, na wanatarajia kuwapata wote wakiwa salama ndani ya siku saba za utafutaji. #indonesia #borneo #banjarmasin #indonesiahelicopter

CCM YAJIVUNIA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO, YA AHAIDI KUBORESHA ELIMU, MAJI NA VIPAJI VYA VIJANA

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema mafanikio ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini ni kielelezo cha dhamira yake ya kweli katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, na kwamba kinaendelea kujipanga kuimarisha huduma muhimu za kijamii katika kila sekta. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jiji la Dodoma, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, amesema pamoja na mafanikio ya miradi kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, na barabara kuu za lami, CCM ina mpango kabambe wa kuwekeza zaidi katika elimu, maji, miundombinu ya afya na kukuza vipaji vya vijana. “Huduma bora kwa wananchi ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli. Tutaendelea kupeleka umeme kwenye vijiji vilivyobaki, kuboresha miundombinu ya shule na zahanati, na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama,” amesema Mavunde. Ameeleza kuwa serikali kupitia CCM inaendelea kutekeleza programu maalum za kuibua na ...

ISRAELI YADUNGUA KOMBOLA KUTOKA YEMEN

Picha
WAASI wa Houthi wameapa kuiwajibisha #Israel baada Waziri Mkuu wao Ahmed Ghaleb Nasser Al-Rahawi na maofisa wengine 11 wa ngazi ya juu kuuawa katika shambulio la wanajeshi wa Israel wiki iliopita katika Mji wa #sanaa. #HouthiRebels Jeneza la Waziri Mkuu wa Houthi Ahmed al-Rahawi Sept. 1, 2025. 

WAAJIRI WATAKIWA KULIPA STAHIKI ZA MADEREVA KWA WAKATI

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka waajiri wa taasisi za umma kuhakikisha wanalipa stahiki za madereva kwa wakati, kutoa mafunzo ya mara kwa mara, kutekeleza ipasavyo miundo ya ajira na kuwapa motisha ili kuongeza tija katika utendaji kazi wao. Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kufungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST), Waziri Mkuu amesema madereva wa Serikali wana mchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali na hivyo wanapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa. "Waajiri mnapaswa kuhakikisha madereva wanalipwa stahiki zao kwa wakati, wanapewa mafunzo stahiki na kuzingatiwa katika motisha mbalimbali. Hii itawajengea morali na kuongeza ufanisi katika kazi zao," amesema Majaliwa. Aidha, amesisitiza kuwa madereva wanawajibu wa kufanya kazi kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kuhakiki usalama wa vyombo vya usafiri, abiria, mizigo na nyaraka za Serikali. “Madereva mnatakiwa kufanya...

TAARIFA KWA UMMA

Picha
 

MAJIKO BANIFU KUPUNGUZA MATUMIZI YA MKAA NA KUNI MBEYA

Picha
*Majiko banifu 9,330 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Mbeya.  Wilaya Sita kunufaika na mradi.  Kila Wilaya kupata majiko 1,555*  Na Mwandishi Wetu, Mbeya.  SERIKALI ya Mkoa wa Mbeya kupitia Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu, Rodrick Mpogolo leo Jumanne Septemba 2, 2025 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu 9,330 yenye ufanisi mkubwa katika utumiaji wake. Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mradi Mhandisi wa miradi kutoka wakala wa nishaji vijijini (REA), Raya Majallah amesema, Kupitia utafiti uliofanyika 2016 unakadiria kuwa takribani watu 33,024 hufariki kabla ya wakati kila mwaka hii ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini Tanzania, kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba wakati wa upikaji kwa kutumia nishati isiyo safi na salama. Hivyo kwa kutambua hilo, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imeaanda mpango wa uuzaji na usambazaji majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku ili kupu...

MICHEZO

Picha
RATIBA ya Michuano ya Kagame Cup 2025.   

DKT. LADISLAUS CHANG’A ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA 6 WA MAWAZIRI NA MAMLAKA ZA MAZINGIRA WA ASIA NA PASIFIKI

Picha
Nadi, Fiji.  KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a, kwa mwaliko wa Programu ya Umoja wa Mataifa uratibu wa Mazingira (UNEP) ameshiriki kikamilifu katika Mkutano wa 6 wa Mawaziri na Mamlaka za Mazingira wa Asia na Pasifiki (6th AP Forum) uliofanyika kuanzia tarehe 26–29 Agosti 2025 Jijini Nadi, Fiji. Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Fiji na UNEP ukiwa na kaulimbiu “Kutafuta Suluhisho Endelevu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi Duniani”. Sambamba na mkutano huo, Dkt. Chang’a alikuwa na vikao mbalimbali na waheshimiwa na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kikao na Mhe. Rupa B. K., Waziri wa Serikali ya Nepal, Wizara ya Misitu na Mazingira, ambapo alimpatia taarifa kuhusu mpango kazi wa IPCC unaotekelezwa hadi mwaka 2029.  Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kikan...

REA YAENDELEA KUTEKELEZA KWA VITENDO MKAKATI WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Picha
 *Majiko banifu 4,836 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe.  Jiko moja kuuzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 8,850 tu.  📌 *Kila walaya kupata majiko 1,209*  Na Mwandishi Wetu, Njombe.  KATIBU Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari amekutana na Timu ya Wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) leo Septemba 1, 2025 na kupata taarifa ya mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambao unatarajia kuanzia mapema mwezi wa 9, 2025. Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Mhandisi wa miradi Kutoka wakala wa Nishati Vijijini, Raya Majallah, amesema, Wakati Taifa likiwa kwenye mkakati wa kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi na salama ya kupikia, Wakala wa Nishati Vijijini umekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa  majiko banifu 200,000 kwa bei ya ruzuku yanayotumia kuni na mkaa mchache sana na yenye ufanisi mkubwa katika matumizi yake. Mradi huu umekuja kwa lengo la kuimarisha na kubor...