Na Mwandishi Wetu, Dodoma WANANCHI wa Tarime Mjini wametakiwa kuwa watulivu na kuendelea kuwa na mshikamano, kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliolenga kumpata mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao. Kauli hiyo imetolewa leo, Agousti 25 ,2025 jijini Dodoma na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Michael Kembaki ,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatima ya mchakato wa kura za maoni na mwelekeo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Kembaki, ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitano bungeni, amewashukuru wananchi wa Tarime kwa ushirikiano waliompa wakati wa uongozi wake, pamoja na wajumbe waliompa kura katika kura za maoni. Katika mchakato huo, Kembaki alipata kura ,5572, Hata hivyo, anasema kuwa chama kilifanya maamuzi yake kupitia ngazi mbalimbali kuanzia vikao vya kata, wilaya, mkoa hadi taifa na hatimaye kumpitisha mgombea mwingine kupeperusha bendera ya ...