Machapisho

RUVUMA YAPOKEA MAJIKO BANIFU 7,648 KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Songea- Ruvuma. MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, leo Mei 25, 2026 amepokea rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia kampuni ya Burn Manufacturing Company Limited. Mradi huo unalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia usambazaji wa majiko banifu yenye teknolojia ya kisasa kwa gharama nafuu kutokana na ruzuku inayotolewa na Serikali. Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo, Mkuu wa Mkoa ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati safi ya kupikia nchini, akieleza kuwa majiko banifu yana mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi pamoja na kulinda mazingira. Amesema matumizi ya majiko hayo yatasaidia kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya kuni na mkaa usio salama, ikiwemo moshi unaosababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji, hususan wanawake na watoto. Mheshi...

REA YASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WANGING'OMBE, YASAMBAZA MITUNGI YA GESI KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Wanging’ombe -  Njombe.  WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeshiriki katika sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 zilizofanyika Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, ambapo umesambaza na kuuza mitungi ya gesi ya kilo sita kwa wananchi kwa bei ya ruzuku ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza baada ya kutembelea banda la REA katika sherehe hizo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, ameipongeza REA kwa juhudi kubwa inazoendelea kuzifanya katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia nchini.  Amesema miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira. Ameeleza kuwa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ni hatua muhimu katika kuboresha afya za wananchi, kulinda mazingira pamoja na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira kwa kiwang...

NCHIMBI AAGIZA VIONGOZI WANAOWAKWAMISHA WAANDISHI WAENDESHA OFISI KUCHUKULIWA HATUA

Picha
  Na Happyness Hans, WAF - ARUSHA  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka viongozi na wakuu wa Idara wanaowazuia waandishi waendesha Ofisi kushiriki mikutano ya chama hicho kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Amesema hayo leo Mei 21, 2026 Mkoani Arusha kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa 13 wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA), unaoambatana na uchaguzi wa viongozi wapya wa chama hicho. “Tunatamani kila kiongozi awapende, awajali, awape safari, motisha na kuwapongeza pale wanapofanya vizuri,” amesema Dkt. Nchimbi. Mhe. Dkt. Nchimbi amesema Ofisi yoyote bila uwepo wa waandishi waendesha Ofisi ni sawa na gari lisilo na usukani, kwani wao ndiyo sura na lango la Ofisi. Amesema hakuna mtu anayeweza kuonana moja kwa moja na kiongozi bila kupitia kwa mwendesha Ofisi. Aidha amesema waandishi waendesha Ofisi wamekuwa msaada mkubwa katika Taasisi mbalim...

AFROMEDIA YAIPONGEZA "CAIRO 24" KWA KWA KUTWAA TUZO YA "TOVUTI BORA ZAIDI MASHARIKI YA KATI"

Picha
Na Mwandishi Wetu, Cairo.  HASSAN Ghazaly, Mwanzilishi wa Mpango wa “Afromedia kwa Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari vya Afrika”, ametoa pongezi zake za dhati kwa wahariri wa tovuti ya “Cairo 24”, wakiongozwa na mwanahabari Mahmoud El-Mamlouk, Mhariri Mkuu, kwa mnasaba wa kutunukiwa kwa tovuti hiyo na kutwaa tuzo ya “Bora zaidi Mashariki ya Kati” katika hafla ya utoaji wa tuzo za Trend Awards.  Mafanikio haya yanaakisi nafasi madhubuti ya kitaaluma na kimedia ambayo tovuti hiyo imefanikiwa kuijenga katika kipindi kifupi nchini Misri na barani Afrika. Ghazaly alieleza kuwa kutunukiwa kwa “Cairo 24” kunawakilisha mfano wa vyombo vya habari wenye ushawishi mkubwa katika medani ya habari barani Afrika na nchini Misri, ulioweza kuunganisha kasi, usahihi na uaminifu katika uwasilishaji wa habari, pamoja na mchango wake katika kufuatilia masuala ya kikanda na kimataifa, hasa yale yanayohusiana na bara la Afrika na mataifa yake. Aidha, Hassan Ghazaly alisifu mafanikio hayo, akib...

SIKU YA NYUKI DUNIANI’ YAADHIMISHWA KITAIFA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  MAADHIMISHO ya Siku ya Nyuki Duniani yanayoyohusisha utundikaji mizinga, maonesho ya bidhaa na mazao ya nyuki yameanza leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Vita Mjini Tabora na kuvuta umati mkubwa wa wananchi. Wakizungumza kwenye maadhimisho hayo wakazi wa Tabora wameeleza kufurahishwa na tukio hilo kwa kuwa linawapa fursa wageni kutembelea Mkoa huo na kuonja utamu wa asali inayozalishwa katika misitu ya Mkoa huo. Daud Elisha, mjasiriamali mkazi wa Kata ya Kanyenye, Halmashauri ya manispaa ya Tabora ameeleza kuwa zao la asali ni miongoni mwa mazao ya kujivunia yanayozalishwa katika Mkoa huo na kuuzwa kwa bei kubwa ndani na nje ya nchi. ‘Haya maadhimisho ni fursa muhimu sana kwa wana Tabora kuuza asali yao na kupanua wigo wa uzalishaji zao hilo katika Wilaya zote za Mkoa huu, hivyo kuwaneemesha zaidi kiuchumi’, amesema. Amina Madereka, mjasiriamali anayejishughulisha na utundikaji mizinga na uuzaji asali katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ame...

TANROADS YAENDELEA KULINDA BARABARA.

Picha
  Na Ahmed Ahmed - Dodoma.  WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kulinda miundombinu ya barabara ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuwa salama kwa watumiaji wakati wote. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega ameyasema hayo Mei 20, 2025 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2026/2027. "Kwa hakika haya ni mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi kwa upande wa miundombinu ya barabara na madaraka," alisema. Ulega amesema barabara zinaendelea kuwa miundombinu muhimu ya usafiri nchini kutokana na kufika katika maeneo mengi ikilinganishwa na miundombinu mingine ya usafiri na usafirishaji. Amesema katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026, ukarabati wa kawaida ya barabara zenye urefu wa kilomita 16,782.58 umefanyika pamoja na marekebisho maalum ya kilomita 1,101.12.