REA YASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WANGING'OMBE, YASAMBAZA MITUNGI YA GESI KWA BEI YA RUZUKU.
Na Mwandishi Wetu, Wanging’ombe - Njombe. WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeshiriki katika sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 zilizofanyika Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, ambapo umesambaza na kuuza mitungi ya gesi ya kilo sita kwa wananchi kwa bei ya ruzuku ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza baada ya kutembelea banda la REA katika sherehe hizo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, ameipongeza REA kwa juhudi kubwa inazoendelea kuzifanya katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia nchini. Amesema miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira. Ameeleza kuwa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ni hatua muhimu katika kuboresha afya za wananchi, kulinda mazingira pamoja na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira kwa kiwang...