TAMASHA LA KILIMO LAHITIMISHWA MBEYA
REA Yapongezwa uhamasishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia, Umeme sasa ni kitongoji kwa kitongoji. Na Mwandishi Wetu, Iwambi - Mbeya. TAMASHA la Kilimo lililofanyika mkoani Mbeya limehitimishwa rasmi leo Jumatano, tarehe 29 Aprili 2026, kwa mafanikio makubwa huku likiwa limekusanya wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, nishati na maendeleo kutoka ndani na nje ya mkoa huo. Tamasha hilo limekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kuonesha teknolojia mpya na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu njia bora za kuboresha maisha yao kupitia kilimo na matumizi sahihi ya nishati. Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga tamasha hilo,mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu ameipongeza REA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya matumizi ya nishati safi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ina mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi na kulinda mazingira. Alieleza kuwa matumizi ya nishati safi kama majiko ya umeme, majiko y...