NYANSAHO FOUNDATION YAZIDI KUHAMASISHA MAENDELEO BILLION 1.4 ZAKUSANYWA KWENYE HARAMBEE KIJIJI CHA MUSATI WILAYANI SERENGETI.
Na Jovina Massano, Serengeti. KATIKA kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu karibu na maeneo yao Nyansaho Foundation na wadau mbalimbali wachangia Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha upatikanaji wa huduma za afya na elimu Kijiji cha Musati. Harambee hiyo imefanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Musati wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo ilitanguliwa na uzinduzi wa kanisa la Waadventista wa Sabato- Musati Central na nyumba ya mchungaji ambavyo vyote kwa pamoja vimejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya Nyansaho kwa kiasi cha millioni 500. Akiongoza harambee hiyo Waziri wa Ujenzi ,Mh.Abdalah Ulega(MB) ameweza kukusanya jumla ya Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha kujenga Shule pamoja na Zahanati katika Kijiji hicho. Katika harambee hiyo Waziri Ulega na rafiki zake wamechangia shillingi millioni 100 na kuongoza uchangiaji kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo (wafanyabiashara) zikiwemo taasisi za fedha, wageni waalikwa na wananchi na kuweza kufikisha kiasi hicho ...